Heci
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 3,485
- 5,818
Mchungaji Wilibrod Mastai ambaye pia ni Kaimu Naibu Katibu Mkuu Wa KKKT Dayosisi ya mashariki na Pwani (Utawala,Utumishi na Milki) ametangaza mkakati wa kutoa mafunzo ya ziada ya bure kwa wanafunzi wa sekondari kwa kuwatumia walimu ambao ni washarika kanisani hapo.
Lengo la Mpango huo ni kuinua Kiwango cha Ufaulu kwa wanafunzi wa sekondari sambamba na ushauri nasaha.
Katika kile kinachoonekana kupata mwitikio Kwa Washarika walimu zaidi ya 30 walijitokeza huku mchungaji akielezea kuwa anaamini kutakuwa na matokeo mazuri .
Aliwataka Wazazi,Walezi na Washarika wa kanisa hilo wenye watoto wanaosoma kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne kuwaandikisha kwa ajili ya masomo ya muda wa ziada yatakayotolewa bure kila Jumamosi.
"Tumekuwa tunawaombea Wanafunzi Wetu kila inapofikia kipindi cha mitihani ya Taifa,Lakini nimeona kwamba kuna haja ya kutathimini na kusaidia maandalizi yao kwa kuwatumia walimu wetu ambao ni washarika hapa,pia kuna wataalam wa masuala ya ushauri nasaha watakuwepo ili kuwasaidi vijana kujitambua na kuendelea kuwa na maadili mazuri kwa manufaa ya kanisa na Taifa kwa Ujumla.