Mchumba wangu kanisaliti!! Niko kwenye maumivu makali naombeni ushauri

Msamehe kaka, endeleen na safar ukisema utafute dem mwingne yaleyale tu.Mkae chin myajenge life linaendelea

Sent from my iPhone using JamiiForums
Hakuna familia isiyo na mapungufu. Hatuna wazazi wasio na mapungufu, sisi pia si wakamilifu, hatuoi au kuolewa na mtu asiye na mapungufu, kadhalika watoto wetu nao si wakamilifu. Tunayo manung'uniko au malalamiko kila mmoja dhidi ya mwenzake. Tumevunjana moyo na kukatishana tamaa. Kwa hiyo, hakuna ndoa iliyokamilika wala familia iliyoboreka bila kuwa na mazoea au utamaduni wa kusameheana.*

*Msamaha ni nguzo au msingi wa utulivu wa akili na uhai wa roho zetu. Kama hakuna msamaha, familia inakuwa uwanja wa migogoro na mlipuko wa ugomvi. Panapokosekana msamaha, familia inaugua. Msamaha unahuisha moyo, kwa kusafisha fikra na kuufanya moyo kuwa huru. Binadamu asiyesamehe hana amani moyoni na wala hana urafiki au muunganiko na Mungu.*

*Maumivu ni sumu inayodhuru na kuua. Hebu kiponye kidonda hicho cha moyo endapo kuna dalili za kujiumiza. Mtu asiyesamehe anajisababishia mwenyewe ugonjwa wa mwili, kiakili na kiroho. Ndiyo maana familia inapaswa kuwa sehemu ya uhai na si kifo; eneo la uponyaji na sio mahali pa magonjwa; jukwaa la msamaha na si la uovu. Msamaha huleta furaha pale uchungu ulipoleta maumivu; huleta uponyaji hata pale ambapo maumivu yalisababisha magonjwa.*

```Ujumbe huu mzuri umfikie kila mmoja wetu katika familia yake.

Jr

Jr
 
Samahani ndugu yangu kama nitakosea utaniambia.
Nimekusomasoma hata kwenye thread nyingine kuhusu Kuwashambulia wanaopata shida na kuhitaji msaada wetu na unatumia Eti kitunguu Swaumu kimekolea Mara unakuwa mtaalam wa lugha bila kujali maumivu ya mhusika.
Umeelewa mada why usijikite kushauri au ukapita kimya.Unaona fahari gani kumuongezea maumivu MTU ambaye wala hajasema baya lolote.
Nakusihi sana naomba uwe mwelewa na muungwana
Usitafute sifa kwenye maumivu ya watu .
Au kama mada zinakukera bora ukapita kimya.
Aksante.
Huwa nawaza kuna ulazima mtu kutumia neno 'mnoooo', 'sanaaa'..? Yaani ndio msisitizo au vitunguu swaumu vimekolea?

Uandishi wenyewe unanukia vitunguu swaumu tu eti 'nilimwambia kuhusu tabia za wanaume wenye tamaa'..mara 'tunawasiliana kwa siku mara tano'..hii ni ishara zaidi ya kula vitunguu swaumu huna shughuli nyingine. Crap!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakubwa zangu shikamooni, vijana wenzangu habari vipi?
Ndugu zangu, nipo serious sanaa katika ombi langu, nakuomba unipe muda wa kunisikiliza kidogo na unishauri kama inafaa.

Mimi ni kijana nina umri wa miaka 29, ni mwajiliwa serikalini idara ya Afya. Kuna binti nilianza nae uchumba 2017 mwanzoni yeye akiwa chuo flan cha afya, Mimi ni Mgogo yeye ni Mbulu ana miaka 24 sasa.

Tulianza mapenzi akiwa ameonesha msimamo wa kutoshiriki tendo lolote na mimi mpaka mwaka mmoja ulipopita ndo tukaanza kukutana kimwili. Ni binti ambae niliona huyu anafaa kuwa mke wangu kabisaa maana alikua ana msimamo sanaa hata kwa watu wengi waliokua wakimtongoza maana alikua ananionesha sms na calls zao, bas nikawa namshauri wajibu wewe ni mke wa mtu na unahitaji heshima, kiukweli nilijipa moyo hapa nimepata mke kweli kweli.

Basi akamaliza chuo 2017 mwishoni nikamtaftia ajira ya kujishikiza mahali flani mkoa wa Mwanza. Sasa nikawa nimeongea na mtu mmoja awe anafatilia nyendo zake wakati mimi nipo mbali.

Alipotimiza miezi miwili kazini nikapata taarifa kuna kabwana mdogo ka umri wa miaka 22 - 24 kanatembea nae hapo hapo alipopanga chumba, sikutaka kuamini, ikanibidi siku moja nifanye kusadiri kwenda kumtembelea kimya kimya bila taarifa, nikafika akanipokea vizuri. Ilipofika usiku nikamwambia sasa mpenzi unaweza kunihakikishia huku huna mchezo wowote mchafu wa kimahusiano? Akanijibu hapana kabisa mpenzi wangu naomba uniamini.

Nikamuuliza, Je, unaweza kunipa simu yako nikague chochote? Akapata kigugumizi sanaaaaa, nikamuuliza Unanipenda na unajiamini? Akajibu ndio, nikamwambia bas naomba simu yako, akapata kigugumizi kizito sanaaa.

Basi ikanibidi nichukue simu yake nipitie sms na whatsap, aseee niliyoyakuta ni mazito mnooooooo wallahi Nimepata simanzi kubwa sanaaa, ikanibidi niondoke usiku huo huo kwenda kutafta Lodge nikalala na kesho nikaondoka kurudi kazini.

Mchumba wangu huyu nilikua nimeshafahamiana na ndugu zake baadhi na mama yake mzazi alikua ananijua kwa picha tu na alikua tayari karidhia niwewe mkwe wake kabla hata sijaenda kujitambulisha maana matendo niliyomfanyia mwane ni mwanaume mwenye malengo mazuri wazi wazi. Kinachoniuma zaidi ni kwamba nimetumia muda mwingi sanaaa kumjenga kiimani, kumjenga juu ya tabia za wanaume wenye tamaa, kiukweli niliamini huyu mwanamke sasa hakuna atakae weza kumshawishi maana hata mimi binafsi nilikua nimebadilika sanaaa kitabia sikuwa nnahamu na michepuko tena niliona sasa huu ni muda wa kutulia na mwanamke mmoja sina haja ya kutanga tanga na dunia ya leo.

Ndugu zangu niko serious sanaaa, naombeni ushauri cha kufanya, mwanamke huyu alikua anatembea na kijana wa mwenye nyumba tena kwa kulala nae chumbani kwake karibu kila wiki.

Mwanamke alionesha sanaaa kunipenda tulikua tunawasiliana kila siku zaidi ya mara 5 kila siku ya Mungu. Leo naona dunia imenigeuka, nina maumivu makali sanaaaa, niliplan nije kumtambulisha kwetu mwaka huu December, na kwao ningeenda kujitambulisha November ili mwakani Mungu akijaalia tufunge Ndoa. Wakuu, niko gizani, nina msongo wa mawazo, mimi ni jasiri sanaaa lakini nakuomba wewe ndugu yangu ushauri wako katika hili, nakuomba usinitukane wala kunikejeli maana utaniongezea majonzi makubwa.

Naamini thread yangu hii itawafunza na wengine watakao kumbwa na mkasa kama wangu.
ASANTE kwa Muda wako

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana Dogo, mapenzi ndivyo yalivyo hivo. Kama unampenda msamehe na mtoe huko aliko mlete karibu uishi nae mpaka hasira na maumivu yatakapokwisha. Kumbukuka "Kosa moja haliachi mke"

Hata ukiwa nae karibu naomba usipende kumkaguakagua sana wala kutaka kujua mambo mengi maana "Ukimchunguza sana bata humli"

Unatakiwa kuishi na mwanamke kwa akili sana, ni wadhaifu sana hawa. Kitendo cha mwanamke kuishi mbali na wewe lazima agongwe kwasababu ww ni " Fimbo ya mbali haiui nyoka"

Huyo mchumba wako ni lakuvunda halina ubani. ila kama ukijitahidi kumweka karibu vizur basi hakiki unamtimizia mahitaji yake ya kimwili na kifedha yaani "penye udhia penyeza rupia"

Ila ukimuacha na kuamua aende basi yule dogo mwenye miaka 24 mtoto wa mwenye nyumba yeye ataona kapata na ataendelea kujisitili maana "ganda la mua la jana chungu kaona kivuli"

ila kingine wewe ni mwanaume shababi, usiwe nyoronyoro pambana maana ungekuwa mjanja wa mademu la usingelialia. si unajua "Mgaaga na upwa hali wali mkavu" eeee

na kama hutaki kabisa kuonana nae tena jikaze kiume tafuta demu mwingine na ishi nae kwa akili na kumbuka busara zangu. na usimkumbuke kabisa wa zamani ww deal na huyo mpya utaempata maana "Mla mla leo mla jana kala nini"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika Wewe utakuwa Mwl wa kiswahili

Hivi kusinhekuwa na hizi simu. Kweli ndoa zingevunjika kirahisi kiasi hicho
Kuomba simu ya mwenza wako nikuonyesha humuamini na yeyr alishaomba yakwako na yeye ajue yako.
Wanawake mnaukorofi ambao haueleweki.
Hapo tuseme tuu chanzo ni wewe
Usingekaa mbali na huyo mwenza wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanamke hata akupendajeee...!! Yani Lolote linaweza kutokeaaa mkuu.. Usimwamini mwanamkw hata siku mojaa kuwa hawezi kugongwaa aisee... Hilo kosa usirudiee kabisaaa... Umbali wenu piaa umechangiaa sanaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwel umbali umechangia ila akifanya kosa la kumrudisha awe karibu naye atalia mara kumi zaidi kikubwa aachane naye kwanza ajamuowa siyo tatizo alafu ili tatizo la kubeba majukumu ya wazazi ndyo linalowaumiza wanaume cku wakiachana na mwanamke au kushindwa kuachana nao. Mtu hujamuowa wala kwao hujaenda ushaanza kumuudumia ada pesa ya kulipia chumba mara mavazi gharama zote zako na kazi ukaanza kutafuta yeye hana ata wasiwasi ametulia kwanni usiumie siku mkiachana.

Beba majukumu yako kwa mpenzi wako ila usiingilie majukumu ya wazazi wake icho ni kiherehere na kitakuliza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia brother hata ukioana naye hutamuamini kamwe, na hata ukijifanyisha kumuamini bado hutamuamini. Je, angefanya haya tayari mpo kwenye ndoa? Yaani kama umemsaidia hayo yote, umempa msingi wa maisha na bado akakusaliti maana yake hafai. Kwa nini uingie kwenye ndoa na mwanamke ambaye humuamini? Kwani kuanza upya ni kosa? Umeyajua haya kwa sababu pia ulipanga uyajue na sasa umeyajua. Naamini unaweza kuanza upya na umejifunza na huwezi kurudia kosa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nashukuru Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ni hatua tu unapitia katika mambo ya mahusiano utazoea tu ili hata utapoamua kuoa usije kuona ni jambo geni, jipe muda tu maumivu yote yatapoa.
 
Hakuna familia isiyo na mapungufu. Hatuna wazazi wasio na mapungufu, sisi pia si wakamilifu, hatuoi au kuolewa na mtu asiye na mapungufu, kadhalika watoto wetu nao si wakamilifu. Tunayo manung'uniko au malalamiko kila mmoja dhidi ya mwenzake. Tumevunjana moyo na kukatishana tamaa. Kwa hiyo, hakuna ndoa iliyokamilika wala familia iliyoboreka bila kuwa na mazoea au utamaduni wa kusameheana.*

*Msamaha ni nguzo au msingi wa utulivu wa akili na uhai wa roho zetu. Kama hakuna msamaha, familia inakuwa uwanja wa migogoro na mlipuko wa ugomvi. Panapokosekana msamaha, familia inaugua. Msamaha unahuisha moyo, kwa kusafisha fikra na kuufanya moyo kuwa huru. Binadamu asiyesamehe hana amani moyoni na wala hana urafiki au muunganiko na Mungu.*

*Maumivu ni sumu inayodhuru na kuua. Hebu kiponye kidonda hicho cha moyo endapo kuna dalili za kujiumiza. Mtu asiyesamehe anajisababishia mwenyewe ugonjwa wa mwili, kiakili na kiroho. Ndiyo maana familia inapaswa kuwa sehemu ya uhai na si kifo; eneo la uponyaji na sio mahali pa magonjwa; jukwaa la msamaha na si la uovu. Msamaha huleta furaha pale uchungu ulipoleta maumivu; huleta uponyaji hata pale ambapo maumivu yalisababisha magonjwa.*

```Ujumbe huu mzuri umfikie kila mmoja wetu katika familia yake.

Jr

Jr
Heshima kwako Bro, nautambua upeo wako tanguz enzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nikupe pole sana na katika mapenzi hayo yapo katika kujifunza. Luck enough umejua before hujaoa.

Ushauri wangu kung'uta mavumbi songa mbele no need to come back even if u fall in love at the maximum. Lakini pia ukiweza badili namba ya simu au block namba yake. Kiujumla mpotezee kabisa. Kuna wanawake wengi wenye hitaji la kuolewa na wametulia.

Mi nilipitia kwenye tatizo kama lako ila sikuumia sana na mwisho wa siku niwaendea wazazi wake nikawambia ukweli na nikawambia huwa sirudii matapishi nikasonga mbele kiume.

Remember mwanaume ni Lulu isiyoisha thamani yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom