Mchumba wangu kanisaliti!! Niko kwenye maumivu makali naombeni ushauri

shija jr

shija jr

Member
Joined
May 21, 2016
Messages
40
Likes
23
Points
15
shija jr

shija jr

Member
Joined May 21, 2016
40 23 15
Huyo ulimkosea kuanzia mwanzo. Ulimuendea kistaarabu mno na ukawa mpole mno. Dalili mojawapo ni kukaa mwaka bila papuchi...

Wanawake hawapendi nice guys mkuu. Hata kama ni muoaji, be a man. Kuwa na misimamo. Usifuate matakwa yake muda wote, be a priority to yourself.

Muendeshe. Demand utmost respect. Usionyeshe kumuamini. Onyesha kuwa una options na sio kwamba yeye ndio kila kitu kwako. Mwambie kuwa she is highly replaceable hivyo akijiskia at any time anaweza kuondoka.

Mmiliki, lakini be confident. Usimfuatilie mawasiliano yake na nyendo zake. Na ukigundua kitu kwenye simu yake, usimwambie. Basically ingekuwa mahakamani tungesema whatever you find in her phone is inadmissible evidence.

Hakuna principle moja kwamba ukimpa mwanamke kitu flani atatulia. No man knows what women want. Neither do themselves. Neither does God, hata akasema tuishi nao kwa akili.

Hizo principles nilizokupa zitakukinga dhidi ya upuuzi wa hawa viumbe in the future. Your sanity is more important than sex and affection.

Huyo hata ukimsamehe, nakuasi usirudiane naye. Ameshakumark weakness yako. Alianza kukupush limits zako kidogo kidogo na ameshazisogeza sana. Hakufai tena.

Kila mtu ana namna yake ya kudeal na heartbreak. Do what a nigga's got to do.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeandika vitu vya msingi sana na hivi ndivyo tunapaswa kujua kuhusu wanawake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
G.T.L

G.T.L

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2012
Messages
301
Likes
166
Points
60
G.T.L

G.T.L

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2012
301 166 60
Nawashukuru sana wote mliolichukua swala langu kwa uzito, naamini wapo wengi nyuma yangu wamefaidika na mawazo yenu, Sasa naona imebaki mimi mwenyewe kufanya maamuzi. JF ni sehemu muhimu sanaaa katika maisha ya leo. Sijamshirikisha ndugu yangu yoyote hili jambo nikaona JF ni sehemu salama na madhubuti kwangu kupata ushauri. Much Appreciation

Sent using Jamii Forums mobile app
 
rikiboy

rikiboy

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Messages
6,070
Likes
6,306
Points
280
Age
41
rikiboy

rikiboy

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2017
6,070 6,306 280
Kwel umbali umechangia ila akifanya kosa la kumrudisha awe karibu naye atalia mara kumi zaidi kikubwa aachane naye kwanza ajamuowa siyo tatizo alafu ili tatizo la kubeba majukumu ya wazazi ndyo linalowaumiza wanaume cku wakiachana na mwanamke au kushindwa kuachana nao. Mtu hujamuowa wala kwao hujaenda ushaanza kumuudumia ada pesa ya kulipia chumba mara mavazi gharama zote zako na kazi ukaanza kutafuta yeye hana ata wasiwasi ametulia kwanni usiumie siku mkiachana.

Beba majukumu yako kwa mpenzi wako ila usiingilie majukumu ya wazazi wake icho ni kiherehere na kitakuliza

Sent using Jamii Forums mobile app
Na hilo ndo tatizoo.. Huyu jamaa alijivisha majukumu ya Baba yake na Binti...!! Inaumagaa sanaa hiyooo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
rikiboy

rikiboy

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Messages
6,070
Likes
6,306
Points
280
Age
41
rikiboy

rikiboy

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2017
6,070 6,306 280
Nawashukuru sana wote mliolichukua swala langu kwa uzito, naamini wapo wengi nyuma yangu wamefaidika na mawazo yenu, Sasa naona imebaki mimi mwenyewe kufanya maamuzi. JF ni sehemu muhimu sanaaa katika maisha ya leo. Sijamshirikisha ndugu yangu yoyote hili jambo nikaona JF ni sehemu salama na madhubuti kwangu kupata ushauri. Much Appreciation

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana mkuu... Najua utakuwa umepotezaa vingi sana kwake ndo maana unaumia mnoo na kweli ulimpendaa..!! Ilaa SONGAAA MBELEEEE...ACHANA NARE KABISAA FUTA KILA KITU CHAKEEE KAMA NI NAMBA YA SIMU...PICHA ZOTE FUTAA na Hata Msg na calls zake Usizijibuuu japo unaumia lakini ni bora uumie sasa kuliko Ukakomaa baadae yakakukuta tenaa ukawa umepoteza muda zaidi na pesaaa... Piga chini Watoto wazuri wengi sana wapoo!

NB:KUWA BUSY NA MAMBO MENGINE NA KWA SASA USITAFUTE DEMU KABISAA UTAKOSEA TENAA...!! Kuwa busy na kazi ukiwa free angalia series ukiweza cheza games utamsahau kabisaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri wa Kaskazini

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2015
Messages
2,467
Likes
4,013
Points
280
Waziri wa Kaskazini

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2015
2,467 4,013 280
Wanawake bhana
 
H

happiness001

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2015
Messages
489
Likes
950
Points
180
H

happiness001

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2015
489 950 180
Hivi kwanini baada ya kuachwa boys wengi wanamaliziaga story zao kwa kusema nilipanga kumtambulisha kwetu mwezi/mwaka huu?
Yani binti amedumu nae miaka 5+ ila siku walatakapoachwa kwwnye story lazima aseme nilipanga kumtambulisha/kumuoa mwaka huu
 
rikiboy

rikiboy

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Messages
6,070
Likes
6,306
Points
280
Age
41
rikiboy

rikiboy

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2017
6,070 6,306 280
Hivi kwanini baada ya kuachwa boys wengi wanamaliziaga story zao kwa kusema nilipanga kumtambulisha kwetu mwezi/mwaka huu?
Yani binti amedumu nae miaka 5+ ila siku walatakapoachwa kwwnye story lazima aseme nilipanga kumtambulisha/kumuoa mwaka huu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
The Dark Father

The Dark Father

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2017
Messages
834
Likes
905
Points
180
The Dark Father

The Dark Father

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2017
834 905 180
Binadam ni binadam tu. Ni kiumbe aliye kiakili na kihisia. Haijalishi ametokea wapi, au nani, kubadilisha mawazo ni kitu cha kawaida na muhimu.

Ndo maana huwa nashangaa pale mtu anapolalamika kuwa 'lakini aliniambia ananipenda'. Ndio, alikwambia anakupenda, lakini sasa mambo yamebadilika. Yaliyopita yamepita.

Hivyo, usiangalie mmepitia mangapi au umemfanyia nini; bali angalia sasa (present). Obviously hana hisia kama mwanzo. Alikuwa wako (as far as we know) na sasa sio tena. Penyeza hii idea, uta-find peace.

Live in the moment brother. Because thats all you have.

Pole.
Siku nyingine, kumbuka chochote kinaweza tokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hon Dizzoh

Hon Dizzoh

New Member
Joined
Jan 12, 2019
Messages
3
Likes
5
Points
5
Hon Dizzoh

Hon Dizzoh

New Member
Joined Jan 12, 2019
3 5 5
Wakubwa zangu shikamooni, vijana wenzangu habari vipi?
Ndugu zangu, nipo serious sanaa katika ombi langu, nakuomba unipe muda wa kunisikiliza kidogo na unishauri kama inafaa.

Mimi ni kijana nina umri wa miaka 29, ni mwajiliwa serikalini idara ya Afya. Kuna binti nilianza nae uchumba 2017 mwanzoni yeye akiwa chuo flan cha afya, Mimi ni Mgogo yeye ni Mbulu ana miaka 24 sasa.

Tulianza mapenzi akiwa ameonesha msimamo wa kutoshiriki tendo lolote na mimi mpaka mwaka mmoja ulipopita ndo tukaanza kukutana kimwili. Ni binti ambae niliona huyu anafaa kuwa mke wangu kabisaa maana alikua ana msimamo sanaa hata kwa watu wengi waliokua wakimtongoza maana alikua ananionesha sms na calls zao, bas nikawa namshauri wajibu wewe ni mke wa mtu na unahitaji heshima, kiukweli nilijipa moyo hapa nimepata mke kweli kweli.

Basi akamaliza chuo 2017 mwishoni nikamtaftia ajira ya kujishikiza mahali flani mkoa wa Mwanza. Sasa nikawa nimeongea na mtu mmoja awe anafatilia nyendo zake wakati mimi nipo mbali.

Alipotimiza miezi miwili kazini nikapata taarifa kuna kabwana mdogo ka umri wa miaka 22 - 24 kanatembea nae hapo hapo alipopanga chumba, sikutaka kuamini, ikanibidi siku moja nifanye kusadiri kwenda kumtembelea kimya kimya bila taarifa, nikafika akanipokea vizuri. Ilipofika usiku nikamwambia sasa mpenzi unaweza kunihakikishia huku huna mchezo wowote mchafu wa kimahusiano? Akanijibu hapana kabisa mpenzi wangu naomba uniamini.

Nikamuuliza, Je, unaweza kunipa simu yako nikague chochote? Akapata kigugumizi sanaaaaa, nikamuuliza Unanipenda na unajiamini? Akajibu ndio, nikamwambia bas naomba simu yako, akapata kigugumizi kizito sanaaa.

Basi ikanibidi nichukue simu yake nipitie sms na whatsap, aseee niliyoyakuta ni mazito mnooooooo wallahi Nimepata simanzi kubwa sanaaa, ikanibidi niondoke usiku huo huo kwenda kutafta Lodge nikalala na kesho nikaondoka kurudi kazini.

Mchumba wangu huyu nilikua nimeshafahamiana na ndugu zake baadhi na mama yake mzazi alikua ananijua kwa picha tu na alikua tayari karidhia niwewe mkwe wake kabla hata sijaenda kujitambulisha maana matendo niliyomfanyia mwane ni mwanaume mwenye malengo mazuri wazi wazi. Kinachoniuma zaidi ni kwamba nimetumia muda mwingi sanaaa kumjenga kiimani, kumjenga juu ya tabia za wanaume wenye tamaa, kiukweli niliamini huyu mwanamke sasa hakuna atakae weza kumshawishi maana hata mimi binafsi nilikua nimebadilika sanaaa kitabia sikuwa nnahamu na michepuko tena niliona sasa huu ni muda wa kutulia na mwanamke mmoja sina haja ya kutanga tanga na dunia ya leo.

Ndugu zangu niko serious sanaaa, naombeni ushauri cha kufanya, mwanamke huyu alikua anatembea na kijana wa mwenye nyumba tena kwa kulala nae chumbani kwake karibu kila wiki.

Mwanamke alionesha sanaaa kunipenda tulikua tunawasiliana kila siku zaidi ya mara 5 kila siku ya Mungu. Leo naona dunia imenigeuka, nina maumivu makali sanaaaa, niliplan nije kumtambulisha kwetu mwaka huu December, na kwao ningeenda kujitambulisha November ili mwakani Mungu akijaalia tufunge Ndoa. Wakuu, niko gizani, nina msongo wa mawazo, mimi ni jasiri sanaaa lakini nakuomba wewe ndugu yangu ushauri wako katika hili, nakuomba usinitukane wala kunikejeli maana utaniongezea majonzi makubwa.

Naamini thread yangu hii itawafunza na wengine watakao kumbwa na mkasa kama wangu.
ASANTE kwa Muda wako

Sent using Jamii Forums mobile app
Natanguliza pole sana kwako.
Lakini pia nakushauri kuamini jambo linalotokea kuwa lilipangwa.

Haya yanweza kukusaidia kumsahau kimahusiano..
CKUSHAURI UTUMIE ULEVI ET. KUPOTEZA MSONGO..UTAATHIRIKA
fanya haya:
##kama bado una namba zake,picha,audio, na kumbukumbu zingne, nakuashauri uziondoe katika vihifadhio vyako,
Namba inaweza kuwa kichwan lakin baada ya kuifuta,inaweza kukupa uvivu wa kusave tena, pind ushikapo cmu yako.
## epuka kukaa pweke, jichanganye na wadau,ctori nao,
Lakini, kama ctori ztahusu mahuciano, bax jiondoe maeneo. Itakufanya uckumbke maisha yenu ya uhusiano.
## badilisha setting katika mazingira unayoish kam nyumban,, yaan chumba,jiko na sebule.
Kufanya hvo kutakufanya upoteze taswira yake katika maeneo hayo.
Ya kwang ni hayo pekee...
 
dingimtoto

dingimtoto

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2016
Messages
5,832
Likes
12,102
Points
280
dingimtoto

dingimtoto

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2016
5,832 12,102 280
Soma vizur alianza nae mahusiano mwaka 2017 hiyo miaka mi tano umeitoa wapi
Hivi kwanini baada ya kuachwa boys wengi wanamaliziaga story zao kwa kusema nilipanga kumtambulisha kwetu mwezi/mwaka huu?
Yani binti amedumu nae miaka 5+ ila siku walatakapoachwa kwwnye story lazima aseme nilipanga kumtambulisha/kumuoa mwaka huu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
ben milazo

ben milazo

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Messages
862
Likes
471
Points
80
ben milazo

ben milazo

JF-Expert Member
Joined Jan 18, 2015
862 471 80
nazidi kuyaogopa mapenzi kwa hizi shuhuda#nadhani ni heri ukawa treat harsh inasaidiaga sana ukijikuta mr lover lover#yajayo yanasikitisha
 
magombe junior

magombe junior

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Messages
1,777
Likes
217
Points
160
magombe junior

magombe junior

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2012
1,777 217 160
tatizo ni uo umburu mkuu,never trust mwanamke wakimburu na mrangi wengine wataongeza

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Billie

Billie

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2011
Messages
7,593
Likes
6,045
Points
280
Billie

Billie

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2011
7,593 6,045 280
Wakubwa zangu shikamooni, vijana wenzangu habari vipi?
Ndugu zangu, nipo serious sanaa katika ombi langu, nakuomba unipe muda wa kunisikiliza kidogo na unishauri kama inafaa.

Mimi ni kijana nina umri wa miaka 29, ni mwajiliwa serikalini idara ya Afya. Kuna binti nilianza nae uchumba 2017 mwanzoni yeye akiwa chuo flan cha afya, Mimi ni Mgogo yeye ni Mbulu ana miaka 24 sasa.

Tulianza mapenzi akiwa ameonesha msimamo wa kutoshiriki tendo lolote na mimi mpaka mwaka mmoja ulipopita ndo tukaanza kukutana kimwili. Ni binti ambae niliona huyu anafaa kuwa mke wangu kabisaa maana alikua ana msimamo sanaa hata kwa watu wengi waliokua wakimtongoza maana alikua ananionesha sms na calls zao, bas nikawa namshauri wajibu wewe ni mke wa mtu na unahitaji heshima, kiukweli nilijipa moyo hapa nimepata mke kweli kweli.

Basi akamaliza chuo 2017 mwishoni nikamtaftia ajira ya kujishikiza mahali flani mkoa wa Mwanza. Sasa nikawa nimeongea na mtu mmoja awe anafatilia nyendo zake wakati mimi nipo mbali.

Alipotimiza miezi miwili kazini nikapata taarifa kuna kabwana mdogo ka umri wa miaka 22 - 24 kanatembea nae hapo hapo alipopanga chumba, sikutaka kuamini, ikanibidi siku moja nifanye kusadiri kwenda kumtembelea kimya kimya bila taarifa, nikafika akanipokea vizuri. Ilipofika usiku nikamwambia sasa mpenzi unaweza kunihakikishia huku huna mchezo wowote mchafu wa kimahusiano? Akanijibu hapana kabisa mpenzi wangu naomba uniamini.

Nikamuuliza, Je, unaweza kunipa simu yako nikague chochote? Akapata kigugumizi sanaaaaa, nikamuuliza Unanipenda na unajiamini? Akajibu ndio, nikamwambia bas naomba simu yako, akapata kigugumizi kizito sanaaa.

Basi ikanibidi nichukue simu yake nipitie sms na whatsap, aseee niliyoyakuta ni mazito mnooooooo wallahi Nimepata simanzi kubwa sanaaa, ikanibidi niondoke usiku huo huo kwenda kutafta Lodge nikalala na kesho nikaondoka kurudi kazini.

Mchumba wangu huyu nilikua nimeshafahamiana na ndugu zake baadhi na mama yake mzazi alikua ananijua kwa picha tu na alikua tayari karidhia niwewe mkwe wake kabla hata sijaenda kujitambulisha maana matendo niliyomfanyia mwane ni mwanaume mwenye malengo mazuri wazi wazi. Kinachoniuma zaidi ni kwamba nimetumia muda mwingi sanaaa kumjenga kiimani, kumjenga juu ya tabia za wanaume wenye tamaa, kiukweli niliamini huyu mwanamke sasa hakuna atakae weza kumshawishi maana hata mimi binafsi nilikua nimebadilika sanaaa kitabia sikuwa nnahamu na michepuko tena niliona sasa huu ni muda wa kutulia na mwanamke mmoja sina haja ya kutanga tanga na dunia ya leo.

Ndugu zangu niko serious sanaaa, naombeni ushauri cha kufanya, mwanamke huyu alikua anatembea na kijana wa mwenye nyumba tena kwa kulala nae chumbani kwake karibu kila wiki.

Mwanamke alionesha sanaaa kunipenda tulikua tunawasiliana kila siku zaidi ya mara 5 kila siku ya Mungu. Leo naona dunia imenigeuka, nina maumivu makali sanaaaa, niliplan nije kumtambulisha kwetu mwaka huu December, na kwao ningeenda kujitambulisha November ili mwakani Mungu akijaalia tufunge Ndoa. Wakuu, niko gizani, nina msongo wa mawazo, mimi ni jasiri sanaaa lakini nakuomba wewe ndugu yangu ushauri wako katika hili, nakuomba usinitukane wala kunikejeli maana utaniongezea majonzi makubwa.

Naamini thread yangu hii itawafunza na wengine watakao kumbwa na mkasa kama wangu.
ASANTE kwa Muda wako

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa demu wa kimbulu hiyo sio sababu ya kumuacha hata kwao kijijini mbulu hawanaga kesi za kuchepuka ni jambo la kawaida kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forum statistics

Threads 1,250,497
Members 481,367
Posts 29,735,645