Mchumba wangu kaanza katabia cha ajabu

Mchumba wangu kaanza katabia cha ajabu

mzaramo

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2006
Posts
6,371
Reaction score
5,191
Huko nyuma tulikuwa hatuna migogoro yoyote mimi na my wife wangu to be.Na kusema ukweli kama ilivyo desturi yetu watu wa kabila langu mimi ndio nilikuwa nimeyashika mahusiano yetu,Mchumba wangu hakuwa anasema kitu mbele yangu yaani ilikuwa hata ikiwa kosa nimefanya mimi kwa kutumia maneno yangu na kipaji chetu cha kuongea ningeweza kubadili kesi bila wasiwasi wowote na kuihamishia kwake na kuimaliza kwa kuzivunja vunja hoja zake.

Mwezi huu mwanzoni nilipeleka barua ya posa kwako na majibu nimeshapewa hapa nakichanga ili mwezi ujao nipeleke mahari kwao,huyu bibie ni mdigo wa huko Tanga

Tuna miaka 9 kwenye mahusiano yetu toka enzi zile tupo Secondary na msichana wangu kusema ukweli ni mpole na mwenye huruma mno ila mabalaa yameanza hapa juzi juzi tu amekuja na tabia mpya za tofauti kabisa mpaka naanza kumuogopa.

Kuna siku nilienda kumtembelea kazini kwake mida ya lunch nikamtoa kwenye hoteli ya karibu tukaagiza chakula pale mara akaanza kuniangalia kwa makini kwenye kola ya shati langu kabla sijajibu akaanza kufoka ile alama ya Lips shine imefikaje kwenye shati langu nikiwa nimepigwa na butwaa maana sikuwa na nimetoka kuchepuka siku hiyo mwezangu saa nyingi kumbe kishainuka na kurudi kazini kwao bila hata kumaliza chakula chake.Kurudi kwenye gari nikaangalia kwenye kioo hiyo sehemu aliyosema na kusema ukweli hakukuwa na kitu chochote cha tofauti.Zamani ili pambano ningeshinda kirahisi ila hapa akashinda yeye

Siku nyingine nilienda kumpitia kazini kwake ili twende kwangu maana ndio ilikuwa ahadi yetu.ghafla tukiwa njiani akaiona miswaki miwili mipya iliyokuwa juu ya Dash Board akaanzisha ugomvi mkubwa kuwa muda huo nitakuwa nimetoka Hotel na mwanamke ndio maana nimebeba ile miswaki kutoka hotel kwa hiyo hakubali na wala hawezi kwenda kulala na mwanaume ambae ametoka kulala na mwanamke mwingine gest kwa hiyo nimpeleke kwao akiwa kanuna na kuvimba kwa hasira.nikampeleka kwao kwa shingo upande maana sikuwa nimetoka huko aliposema hapa napo akanishinda

Jumapili iliyopita kaja kwangu kwa kustukiza kama Magufuli kanikuta natoka mazoezini mkononi nikiwa nimebeba hotpot lenye supu ambayo nimetoka kununua akaanza maneno kuwa ile supu nimetoka kuchukua kwa mwanamke wangu kwa usalama wangu nimpeleke kwa huyo malaya mwenzangu au nimwage ile supu la sivyo anaondoka zake.Nikagoma kumwaga supu wala kumpeleka nilipoitoa akaondoka zake hapa nikashindwa tena kwa mara ya tatu mfululizo

Kubwa zaidi jana akaja kulala kwangu baada ya kufanya ushawishi mkubwa mno.Usiku wakati tunajiandaa kuivunja amri ya 6 simu yangu ikaita ikabidi tusitishe kwa muda maana ilikuwa ni simu ya biashara mimi sio muajiriwa ni misheni town tu nikatoka mara moja kwenda kupiga deal yeye nikamuacha ndani.nilichelewa kurudi kidogo nilivyorudi nikamkuta kalala na akagoma kabisa kunipa Tunda kwa sababu nimetoka kwa mwanamke wangu mwingine kwa hiyo siwezi kuiweka dudu yangu kwenye papuchi yake.Nikamshawishi usiku kucha akagoma kabisa na vibao akanipiga mbali na vichambo nilivyopewa.Kwa mara nyingine tena akanishinda.

Kusema kweli nimeanza kupata na mashaka na muenendo wake wa siku hizi.Kabadilika huku nguvu yangu ya kumshawishi ikiwa imepungua kabisa kama sio kwisha yaani kutoka kumuongoza yeye mpaka kuongozwa mimi ameanza kuwa na tabia mpya za ubabe na utemi.Yote haya yameanza baada ya kupeleka barua ya Posa kwao.

Je,Niendelee na mipango ya kupeleka mahari kwao au niuchune maana kwa kabila letu ni mwiko kuoa mwanamke ambae atakwenda kukutawala kwenye nyumba.

Asante
 
Hiyo ndio tabia take halisi alikuwa ameificha vita muda mpime kwa makini
 
Itakua ulimroga mwanzoni, sasa tunguli azifanyi kazi unaanza kuchachawa. Pole sana!!
 
Hiyo ndio tabia take halisi alikuwa ameificha vita muda mpime kwa makini

inawezekana mkuu ila imenibidi niwe makini mno na hawa viumbe inawezekana vipi mtu kwa miaka 9 mfululizo afiche tabia yake halisi?!
 
Hivi tukisema muache utakubali? anyway hayo ndio maisha ya mapenzi, ni bora amekuonesha mapema hizo dalili za jeuri na kiburi sasa maamuzi unayo mwenyewe kama utaweza kuvumilia hizo tabia kwa maisha yako yote endelea naye ila kama unaona kabisa huwezi ni bora ubadili mawazo

Failure= few error in judgment repeats everyday, usije ukadharau tabia ndogondogo kwan baada ya muda ni majanga tupu

So be careful kaka ni bora kuvunja uchumba sio ndoa
 
maisha kutesa kwa zamu ni zamu yake kukuonyesha ubabe wake..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom