Mchumba wangu ana madeni balaa

hana madeni...stuka dogooo...huyo ana mabwana kila sehemu ndio maana hataki kuonekana na wewe anasingizia madeni. mwambie unataka mushuke kila sehemu anayodaiwa ukalipe hayo madeni ili kesho mupite kwa raha mustarehe.

stuka dogo....panya road huyooo.
 
mmmmh inawezekana ulipokuwa arusha alikuwa na michepuko mingi so anakuzuga kuwa anadaiwa kumbe anaogopa kugonganisha

umeliona kwa jicho la tatu kama mie nilivyoona....jamaa anaibiwa kimtindo na demu anamdanganya madeni...unajuwa inakuwaje vibwana vyake vikimpigia simu akiwa na mshkaji...demu anakuwa hapokei ukimuuliza vepee anakuambia huyu namjua ananidai ngoja nimchunie.

ahahahaha ... kweli kuishi kwingi kuona mengi na kujifunza vingi pia.
 
Huyo hakufai, ana maisha ya kuiga na hataki apitwe na kitu. Mwanamke mwenye kuendekeza tamaa na kushindwa kujizuia kwa mambo asiyoweza kuyamudu huwa ana sifa ya kukosa uvumilivu na huo ni udhaifu mbovu sana. Hebu Jaribu kumtenga kwa muda, maana pia inawezekana anahangaika kujiweka fresh kwa ajili ya mtu mwingine ambae ni mpya maana kama umekaa nae miaka 9 kwa mwanamke wa kawaida huwa na confidence kuwa unampenda kama alivyo na hawezi kujisumbua kwa ajili ya mwonekano wa nje kiasi cha kukosa amani kama huyo.
 
DMkuu huyo bibie ana tatizo la kisaikolojia na pengine linatokana na tamaa.
Anahitaji couselling ya uhakika na aelezwe madhara yake kinaga ubaga, na hata ikibidi umtishie kumwacha.
Tabia hii wanayo wanawake wengi tu.
 
inawezekana hayo maeneo hadaiwi ila ana minjemba yake haiwezekani ukae na mtoto wa watu miaka tisa hujamuoa we jamaa kiboko bado siku chache tu iwe miaka kumi uchumba gani huo nyie ndo mnaotafuta kurogwa ebu oa mkuu
 
Hahaha ujinga haunaga mwisho. Hata sie waswahili si tulikuwa tunasubiria amina chifupa afufuliwe na gwajima? sijui hadithi ikaishia wapi hii. Huwa nauliza hawa wachawi waangusha ndege wako bongo tu? Air Malaysia hawazifikii wala BA?

Bora wanawake sasa, ukikutana na mwanaume mjinga hutaamini macho yako. :A S 12:

 
Duuh mkuu huwa inaanza ugirlfriend na boyfriend, then nadhan baada ya muda automatically mnaenda uchumba...

Ila miaka tisa ya ugirlfriend?
Uchumba hauji automatically bana, kuna taratibu za kufuata. Au mi ndio sielewi haya mambo?

Halafu mnaweza kuwa kwenye mahusiano tangu wadogo. Wengine walianzia primary school kabisa huko. Hiyo miaka isikuogopeshe.
 
Uchumba hauji automatically bana, kuna taratibu za kufuata. Au mi ndio sielewi haya mambo?

Halafu mnaweza kuwa kwenye mahusiano tangu wadogo. Wengine walianzia primary school kabisa huko. Hiyo miaka isikuogopeshe.

Kweli ni lazima kuna vitu vifanyike ili kubadil status au kuiupgrade from uboyfriend tu uchumba.
 
mlete kwangu, sikopeshi wanawake, nawapa pesa bure..
 
Miaka 9? Kuna wanawake wavumilivu sana aise....kupunguza stress mwache akope tu
 
Mkuu mito, hivi mtu anakuwaje na mchumba kwa miaka tisa? Yani mfano walikutana wakiwa
25 kwa 23, hadi sasa wana 34 kwa 32. Tuwahurumie hawa wanawake bwana.

Yaani acha kabisa mkuu, mi mwenyewe hata sielewi vijana wanaogopa nini kuoa!!!!
 
Ngoja tupime uchumba wake na safari za vasco da gama kukaaa angani nafikiri vinashabihiana aiseeee

Point of correction. Vasco Da Gama hakuwahi kutumia usafiri wa anga.
 
Ha haa vasco da gama nadhana yeye ana 10+1 maana juz juz tu alikuwa southafrica

waambie madada wa jf walionifollow kule Instagram wapunguze kasi Zao hasa Yule Nuru Juma, Teacher flani na nanihii nimewaelewa sana.. Lakini kuna mmoja nadhani yule ni dada wa Mjini mjini lakini jina sikutajii
 
😂😂😂😂😂😂uchumba ni zaidi ya kugraduate udaktari,jamaniii hebu muoe ndio dawa ya kupunguza ukopaji
 
Yapo mapepo ya wizi.udokozi.kukopa.uzinzi.ushoga nk. Kama hii tabia hakuwa nayo na ukiongea nae huoni kama anajali au anasikitika ila hawezi kuacha ujue hayo inaerzekana kabisa yakawa mapepo.
Maombi ya nguvu ndio suluhisho.
Ila huo mlango wa uzinzi bila ndoa kwa kisingizio za urafiki ndio unaokaribisha hali hiyo.
Fanya maamuzi sahihi.
 
Ha ha ha...kuna jamaa mmoja mdau wa Bagamoyo aliniambia kuna waganga wawili Bagamoyo wateja wao zaidi ya 90% ni wanawake. Na matatizo yao ni ishu za mahusiano!!!


Yaani tusipokuwa makini tutalishwa mpaka kinyesi

Sio tu msipokuwa makini,bali ni mnalishwa mambo mengi,nyumba ndogo kwa nyumba kubwa ni mapambano tu ya kwa sangoma,mnajipatia cocktail za malimbwata....
 
Ndiyo raha yako Kuwa na mchumba mkopaji usikute hata wewe unamdai.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…