God bell
JF-Expert Member
- May 13, 2011
- 590
- 211
Za jiona wana MMU. Labda nianze hivi. Kuna dawa wanatumia baadhi ya wanawake za kutolea mimba pindi wanapojigundua wana ujauzito. Hawa wanawake wanakuwa hawana hofu ya Mungu kwani kitendo kama hicho ni cha mauji. Unaua kiumbe kisicho na hatia. Huyu rafiki yangu alikuwa na mchumba wake wakipendana sana, siku anampeleka kwao wazazi wa kijana walipomona walimkataa katu katu hadi kijana akachanganyikiwa (sijui ni mila za kwao) wakati huo bint wa watu tayari alikuwa mjamzito wa mwez 1. Namejua hili jambo manake nilikuwa rafiki yao wa karibu na walikuwa wananishirikisha baadhi mambo yao. Baada ya jamaa kuona mchumba wake amekataliwa ikabidi ampe ukweli kwamba haitakuwepo ndoa tena. Bint akajaribu kumkazia jamaa amwele ukweli kama kuna tatizo ajirekebishe, jamaa akamwambia ''wazazi wamesema nikikuoa nitapata laana kwa kuwa wameshanikataza''. Bint kuona hivo akanitaarifu nikajaribu kuongea na jamaa kadri nilivoweza lakini ikashindikana. Baada ya wiki moja yani jana bint akanipigia sm akaniambia 'shemeji nimeamua kuflash ile mimba, siwezi kutunza mimba nizae mtoto asiekua na malezi ya baba'. Nimesikitika nikamuliza umefanyaje?akanijibu nimeamua kunywa dawa nikaflash kiumbe chake, nitamuomba Mungu anisamehe. Hadi nimejiuliza ni dawa gani hizo wanazotumia? Je wanajiamini nini hawa wanawake juu ya kifo? Inauma sana!