Mchumba nimempata ila...!!!

Dec 24, 2016
33
125
Heri ya mwaka mpya wana Jf wote..!
Nalileta kwenu hili nikiamini humu kuna watu wazima wenye kuweza kunishauri katika hili.

Ila kwa wale wadogo zangu ambao bado mko masomoni naomba muwaachie wakubwa wetu wanishauri na sio kuleta utani,matusi na kejeli.

Ni muda sasa nlikuwa natafuta mchumba ambaye badae aje kuwa mke, nilileta uzi humu lakini pia niliwashirikisha watu wa karibu ikiwemo viongozi wa kiroho na nilifikia uamzi huo baada ya kuona muda wangu wa kuoa umefika pia nlishachoka na maisha ya kihuni
Wengi niliokutana nao sikuvutiwa na tabia zao.

Lakini kuna binti nimempata ambaye kweli ana sifa zote nilizotaka.
Ni mcha Mungu,ana heshima kwangu na kwa jamii inayomzunguka pia anaonekana muwazi kwangu.

Nilimfahamu kupitia mama mmoja wanasali kanisa moja
Baada ya mazungumzo marefu nlimueleza nia yangu ya kumwoa akanielewa ila akaomba tusifanye sex mpaka ndoa nilipomuuliza kwa nini akasema alikuwa na mchumba ambaye alimfanya ayachukie mapenzi baada ya kumtenda.

Nilimwomba anieleze kwa kirefu akasema yeye ni mtoto wa kwanza kwa kati ya watoto watano ambapo mama yao amezaa kila mtoto na babake!
Hamjui babake na alipomaliza elimu ya msingi mama hakuwa na uwezo wa kumsomesha hivyo alipelekwa Dar kufanya kazi za ndani kwa mama mmoja ambapo amedumu mwaka 1.

kisha manyanyaso yalipozidi akapata kazi sehemu nyingine ambapo alikuwa analipwa pesa nzuri na kumtumia mamake kijijini lakn badae mtoto wa kiume wa bosi wake akamrubuni mpaka kumtoa bikra na kuanza mahusiano ambayo yalidumu kwa kificho na kijana alikuwa akimsaidia binti kwa mambo mengi lakn tatizo alianza kumlazimisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile ambapo alishindwa kumkatalia kwani hakujua kama kuna madhara pia aliogopa kupoteza ajira.

Anadai alikuwa anasikia maumivu ila alivumilia na kijana alimwahidi kumwoa lakini baada ya mwaka mmoja kijana alileta msichana mwingine na kumtambulisha kwa wazazi mbele ya huyu binti.

Kitendo kilimuuma sana ndipo aliamua kuacha kazi na kurudi kijijini kwa mamake.
Ukweli anaonekana ana nia ya kuolewa ila kinachonipa hofu ni hili la mapenzi kinyume na maumbile.

Je nikimwoa na mimi sifanyi uchafu huo ataweza kuacha kabisa?
Japo yeye anaahidi hatoweza kurudia na hapendi.
Je ni kweli inawezekana mtu aliyepitia mchezo huo akaacha?
Nawaza pia nisimwoe lakini yeye amekuwa mkweli kunipa historia yake kwa kuamini ntamwoa.

Wangapi wanawaficha wachumba wao historia zao za kimapenzi mpaka wanaolewa?
Kifupi binti huyu ni tofauti kabisa na wengine niliowahi kuwapata ambao wengi wao waliweka pesa mbele na uongo mwingi!
Huyu binti ni mdogo miaka 19 na jana nliamua kumpeleka hospital afanyiwe vipimo vyote vya zinaa na H.I.V.

Majibu yalionesha hana tatizo lolote ila sasa tatizo linaloniumiza kichwa ni hilo tu.!
Ikiwa ntamwoa nfanyeje asije kuniletea matatizo mbeleni?
Au nimwache?

Pia nikimwacha ntamwaminije mwingine kuwa hajafanyiwa mchezo huo maana wengi sio wakweli.
Mbarikiwe sana.!!!
 
naiman64

JF-Expert Member
Nov 22, 2013
5,757
2,000
Oa huyo binti ila Iwe kweli unampenda maana amekiri mwenyewe hatorudia upuuzi huo pia kumbuka alirubuniwa vile alikuwa bado mdogo ila na wewe isiwe ndio kiboko chake akifanya kosa badala yakumrekebisha na kumfundisha au kushauri unamkumbushia yaliyopita utakuwa unamuongezea machungu.
 
Trimmer

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,501
2,000
Kama hajawa addicted hamna tatizo muoe tu,, shida ni pale kama amekolea kwenye huo mchezo hawezi kuacha usipotumia lazima atafute watumiaji..
 
cheupe dawa

Senior Member
Apr 3, 2016
172
250
kwa vile amekuwa muwazi, na umesema ni mcha Mungu we muoe tu, ila jipe muda kwanza ili umfahamu zaidi usifanye haraka, wanawake tuna siri nyingi mno tungekuwa tunaziweka wazi hakuna ambae angeolewa hata mmoja, wapo waliotoa mimba zaidi ya kumi lakini kwa sasa ni wife materials, wapo waliokuwa machangudoa lakin kwa sasa wametulia na familia zao!, wapo yaani wengine hawaelezeki lakin kwa sasa ni mama bora kwa familia zao!! nadhani hata wewe una mabaya yako ya nyuma huko lakin kwa vile mnaanza moja hamtakiwi kuangalia ya nyuma,
 
mxsdk

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
3,592
2,000
Kwaiyo hakumwambia daktari ilo tatizo LA kuliwa Tigo?wewe wewe!ngoja niweke pause.
 
Queen Kan

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
3,458
2,000
Oa huyo binti ila Iwe kweli unampenda maana amekiri mwenyewe hatorudia upuuzi huo pia kumbuka alirubuniwa vile alikuwa bado mdogo ila na wewe isiwe ndio kiboko chake akifanya kosa badala yakumrekebisha na kumfundisha au kushauri unamkumbushia yaliyopita utakuwa unamuongezea machungu.
Hamna kitu kibaya kwenye mahusiano kama mtu ukiri makosa yako ila ukikosea kidogo tu uanze kusimangwa na yaliyopitaa...yani inaumizaa mnoo
 
mashishanga

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
612
500
Heri ya mwaka mpya wana Jf wote..!
Nalileta kwenu hili nikiamini humu kuna watu wazima wenye kuweza kunishauri katika hili.
Ila kwa wale wadogo zangu ambao bado mko masomoni naomba muwaachie wakubwa wetu wanishauri na sio kuleta utani,matusi na kejeli.
Ni muda sasa nlikuwa natafuta mchumba ambaye badae aje kuwa mke, nilileta uzi humu lakini pia niliwashirikisha watu wa karibu ikiwemo viongozi wa kiroho na nilifikia uamzi huo baada ya kuona muda wangu wa kuoa umefika pia nlishachoka na maisha ya kihuni.
Wengi nliokutana nao sikuvutiwa na tabia zao
Lakn kuna binti nmempata ambaye kweli ana sifa zote nilizotaka.
Ni mcha Mungu,ana heshima kwangu na kwa jamii inayomzunguka pia anaonekana muwazi kwangu.
Nilimfahamu kupitia mama mmoja wanasali kanisa moja
Baada ya mazungumzo marefu nlimueleza nia yangu ya kumwoa akanielewa ila akaomba tusifanye sex mpaka ndoa nilipomuuliza kwa nini akasema alikuwa na mchumba ambaye alimfanya ayachukie mapenzi baada ya kumtenda.
Nilimwomba anieleze kwa kirefu akasema yeye ni mtoto wa kwanza kwa kati ya watoto watano ambapo mama yao amezaa kila mtoto na babake!
Hamjui babake na alipomaliza elimu ya msingi mama hakuwa na uwezo wa kumsomesha hivyo alipelekwa Dar kufanya kazi za ndani kwa mama mmoja ambapo amedumu mwaka 1 kisha manyanyaso yalipozidi akapata kazi sehemu nyingine ambapo alikuwa analipwa pesa nzuri na kumtumia mamake kijijini lakn badae mtoto wa kiume wa bosi wake akamrubuni mpaka kumtoa bikra na kuanza mahusiano ambayo yalidumu kwa kificho na kijana alikuwa akimsaidia binti kwa mambo mengi lakn tatizo alianza kumlazimisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile ambapo alishindwa kumkatalia kwani hakujua kama kuna madhara pia aliogopa kupoteza ajira.
Anadai alikuwa anasikia maumivu ila alivumilia na kijana alimwahidi kumwoa lakini baada ya mwaka mmoja kijana alileta msichana mwingine na kumtambulisha kwa wazazi mbele ya huyu binti.!
Kitendo kilimuuma sana ndipo aliamua kuacha kazi na kurudi kijijini kwa mamake.
Ukweli anaonekana ana nia ya kuolewa ila kinachonipa hofu ni hili la mapenzi kinyume na maumbile.!
Je nikimwoa na mimi sifanyi uchafu huo ataweza kuacha kabisa?
Japo yeye anaahidi hatoweza kurudia na hapendi.
Je ni kweli inawezekana mtu aliyepitia mchezo huo akaacha?
Nawaza pia nisimwoe lakini yeye amekuwa mkweli kunipa historia yake kwa kuamini ntamwoa,
Wangapi wanawaficha wachumba wao historia zao za kimapenzi mpaka wanaolewa?
Kifupi binti huyu ni tofauti kabisa na wengine niliowahi kuwapata ambao wengi wao waliweka pesa mbele na uongo mwingi!
Huyu binti ni mdogo miaka 19 na jana nliamua kumpeleka hospital afanyiwe vipimo vyote vya zinaa na H.I.V
Majibu yalionesha hana tatizo lolote ila sasa tatizo linaloniumiza kichwa ni hilo tu.!
Ikiwa ntamwoa nfanyeje asije kuniletea matatizo mbeleni?
Au nimwache?
Pia nikimwacha ntamwaminije mwingine kuwa hajafanyiwa mchezo huo maana wengi sio wakweli.
Mbarikiwe sana.!!!
Muoe kabisa huyo bint kumbuka amekiri ukweli ambao angeweza kuuficha, pili alifanyiwa hicho kitendo kwa kurubuniwa kwa kua alihofia kufukuzwa kazi, na kama alikua anapenda huo mchezo tayar ata sasa angeendekeza uzinz na ww, pia nikusih ukija kumuoa isiwe fimbo yakumchapia kwa kumkumbusha ya nyuma ambayo yalishapita, mwanamke akisema kaacha kama amedhamimiria kweli anaacha, kweli mabint wanapitia changamoto nying
 
Mrigariga

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
1,693
2,000
Huyu binti ni mdogo miaka 19 na jana nliamua kumpeleka hospital afanyiwe vipimo vyote vya zinaa na H.I.V
Vipimo vya zinaa ndio vipi?!!! Zinaa inafanywa name walio katika ndoa tu. Pale wanapokutana na wenzi wao Annapurna sio mkewe au miners.

Huyu binti kaamua kuwa mkweli kwako inaweza ikatokana na hofu ya Mungu au ni utoto tu. Sasa wewe rejea
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom