Mchumba alitoroshwa akaolewa, sasa anataka nikamtoroshe

Wakuu,

Mimi ni mvulana (26) nimehitimu chuo kikuu cha UDSM fani ya Elimu na Sanaa (BAED). Mwaka 2011 nilimpa mimba mpenzi wangu nikiwa kidato cha sita naye akiwa cha tatu, akaacha shule nikamuahidi kumuoa, lakini baadaye akaona nimechelewa akawa ametoroshwa na mwanaume fulani kuja Dar.

Cha ajabu kwa sasa amezalishwa na ananitaka mimi nimtoroshe tena wakati nyumbani kwao mumewe anajulikana na wako naye hadi leo. Na mimi nimepata mchumba mwingine. Nifanyeje maana naheshimu ndoa yake na pia yeye anakuja hadi kwetu.

Elimu yako yoootee imeshndwa kuamua??? Mwambie huyo wa kidato cha 3 akupe mbinu stahikii maana yeye muelewa na msomi zaidi yakoo
 
Ni katabia kake mtoroshe tu mkuu na mimi nitakuja kumtorosha niambie tu mtakapoishi
 
Mimba kidato cha tatu? Tangulia tu jela mwenyewe
 
Uamzi ni wako na dalili zinaonesha uko serious kumtorosha ili utimize ahadi na ndoto ya kuishi naye...! Ni wazo nzuri lakini jitahidi wakati unamtorosha huyo uwe unaandaa wa kuja kumuoa kabisa.
 
una elimu ya chuo af unauliza mambo ya......haya basi mtoroshe mrudishe kwako na mie ntamtorosha kutoka kwako kuja kwangu af CHILUNDU ATAMTOROSHA KWAKNGU AMCHUKUE......CYCLE CONT.....
 
mapengo17, mwalimu mzima hujui cha kufanya...??
 
Last edited by a moderator:
Daah hovyo sana ww inavoonesha hata ukiulizwa swali hata jepesi unakimbilia google. Sasa kama una mwingine aliyeona unachelewa na kutoroka ili aolewe wa nn kwako? Acha kuyumbishwa na madem mwl.
 
Wakuu,

Mimi ni mvulana (26) nimehitimu chuo kikuu cha UDSM fani ya Elimu na Sanaa (BAED). Mwaka 2011 nilimpa mimba mpenzi wangu nikiwa kidato cha sita naye akiwa cha tatu, akaacha shule nikamuahidi kumuoa, lakini baadaye akaona nimechelewa akawa ametoroshwa na mwanaume fulani kuja Dar.

Cha ajabu kwa sasa amezalishwa na ananitaka mimi nimtoroshe tena wakati nyumbani kwao mumewe anajulikana na wako naye hadi leo. Na mimi nimepata mchumba mwingine. Nifanyeje maana naheshimu ndoa yake na pia yeye anakuja hadi kwetu.

Mwalimu..i hope una a b c za education psychology gudance and couseling....jibu liko wazi wewe hapo tambaaa achana naye!
 
Aaah! wee mbona kwanza unjdharirisha? huon kuw hukupaswa kupost kam ki2 kama hicho?wew c umemalza chuo kikuu au? wew c una stashahada ya elmu Tena mjanja kabxa uliepata elmu ktk sanaa? BADO unayo nafac jpange utapost tena kwahilo tumekuona!
 
Wakuu,

Mimi ni mvulana (26) nimehitimu chuo kikuu cha UDSM fani ya Elimu na Sanaa (BAED). Mwaka 2011 nilimpa mimba mpenzi wangu nikiwa kidato cha sita naye akiwa cha tatu, akaacha shule nikamuahidi kumuoa, lakini baadaye akaona nimechelewa akawa ametoroshwa na mwanaume fulani kuja Dar.

Cha ajabu kwa sasa amezalishwa na ananitaka mimi nimtoroshe tena wakati nyumbani kwao mumewe anajulikana na wako naye hadi leo. Na mimi nimepata mchumba mwingine. Nifanyeje maana naheshimu ndoa yake na pia yeye anakuja hadi kwetu.

anakujaribu mpumbavu tu
 
na akija kwako ataomba mwingine amtoroshe. wow! akili kumkichwa let the game continue
 
Suala hili nalo linataka ushauri ??????????????????????????????????????????.

Wakuu,

Mimi ni mvulana (26) nimehitimu chuo kikuu cha UDSM fani ya Elimu na Sanaa (BAED). Mwaka 2011 nilimpa mimba mpenzi wangu nikiwa kidato cha sita naye akiwa cha tatu, akaacha shule nikamuahidi kumuoa, lakini baadaye akaona nimechelewa akawa ametoroshwa na mwanaume fulani kuja Dar.

Cha ajabu kwa sasa amezalishwa na ananitaka mimi nimtoroshe tena wakati nyumbani kwao mumewe anajulikana na wako naye hadi leo. Na mimi nimepata mchumba mwingine. Nifanyeje maana naheshimu ndoa yake na pia yeye anakuja hadi kwetu.
 
Abortion doent make u UNPREGNANT only.....but a mother of dead babies.........am not sure the first kid is surviving
 
Unastahili kupandishwa kizimbani kwa kumpa mimba mwanafunzi na kumkosesha elimu
 
Back
Top Bottom