Mchuma janga hula na wa kwao! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchuma janga hula na wa kwao!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by LD, Mar 4, 2011.

 1. LD

  LD JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wapendwa habarini za Ijumaa, natumaini, mnayo Ijumaa nzuri yenye furaha na amani.
  Hata wale ambao wanaiona sio nzuri kwa sababu mbalimbali, bado tuendelee kumshukuru Mungu madamu ametuachia uhai na afya.

  Kuna jambo nimeliona katika jamii inayotuzunguka, nikafikiria halafu nikaona tushirikishane mawazo mawili matatu huku tukisubiria jioni yenye baraka!!

  Ni hiviii!! Nimekuwa nikiona katika jamii binti anapoolewa na kuachana na wazazi wake, na kuungana na mume wake, na kuwa mwili mmoja, wanaishi kwa pamoja wakisaidiana katika raha, milima na mabonde na maisha yanaendelea. Na Mwanaume kadhalika ana achana na baba na mama yake...................

  Lakini inapotokea labda binti amepata tatizo la ugonjwa, utakuta ndugu zake wa damu, yaani mama, dada zake, kaka zake ndo wanajitokeza na kuchukua majukumu ya kumsaidia zaidi. Labda kumpa huduma hospitalini, kumuuguza nk nk..
  hata kama mume wake yupo na ndugu wa mume wake yupo.

  Wakati mwingine hata huyu mwanaume anaweza asihusike sanaaaa ktk jambo hilo, au akahusika kidogo tu. Na kuna wakati inabidi yule mgonjwa (Binti) apelekwe kwa wazazi wake au kwa ndugu zake wa damu kuuguzwa, mpaka atakapona anarudi kwa mume wake.

  Wakati mwingine hata binti akijifungua, atapenda zaidi kuhudumiwa na mama yake mzazi au ndugu zake wa damu, kuliko mama mkwe na ndugu wa mume wake.

  Kingine nilichokiona mwanaume aliyeoa, yeye akipatwa na matatizo kama hayo atahudumiwa kwa kiasi kikubwa na mke wake. Na hata kama alikuwa ni mkorofi kwa mke wake, pengine amehamia hata nyumba ndogo, lakini ikifika kwenye ugonjwa anahamia kwa mke wake, na mke atampokea, atamuuguza na kumtunza mpaka atakapopona au atakapoenda huko ambako hakuna hiari..............

  Sasa basi, ni kweli kwamba wazazi na ndugu zetu mabinti/wanawake wanahusika na sisi ktk matatizo na shida zetu kwa kiasi kikubwa hata kama tumeolewa?

  Je ni kweli kwamba nyumbani kwetu ndio kichaka cha matatizo yetu?

  Kwa nini mwanaume akipata tatizo anatafutwa mke wake anahusika zaidiiiiiiiii kuliko mama yake na ndugu zake wa damu?

  Kama ndo hivo, basi kina dada tuna kila sababu ya kuwajali ndugu na jamaa zetu kwa sababu kila janga tunalolipata tunakula nao pia.............!!!!
   
 2. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Naam malenga wetu. Ngoja tuwasikie wadau maana hapa mi sina nyimbo
   
 3. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  nakubaliana nawe kwa kiasi fulani, ila mambo mengine mnasababisha nyie wenyewe na ndugu zenu mwanamke akiolewa anakuja na ndugu zake wakike au kiume hata wazazi nao wanakuja wanahamia kwa mume sasa unategemea hata ukiumwa kidogo wataacha kuja?
  samahani kwa waluguru, kaka yangu ameoa mluguru hadi anakoma akitoka mama mzazi anakuja mama mdogo, madada, shangazi wanapishana basi mradi ndugu wa mke hawakosi wawili au watutu.
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mmh nadhani ni mazoea tu!Japo kwetu wanawake wote waliolewa kwetu hua wanakula uzazi kwetu na wakiumwa wanahudumiwa pia...wakwao wanakuja kusalimia tu!Hapo swala la upendo nadhani linahusu kwasababu kama wakwe hawapendani ni ngumu kuangaliana kwahiyo unakuta binti anaona bora kwenda kwao!Kuhusu wanawake kujali waume zao kipindi cha ugonjwa ni natural kwasababu ni nature ya mwanamke kujali na kuangalia..tofauti na mwanaume ambaye anahitaji msaada kwenye hilo!Mengine ngoja nitafakari!
   
 5. LD

  LD JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wanakuja hata kama hakuna tatizo?
  Wanakuja kula, na kulala tu?
   
 6. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Kuna ukweli mkubwa kwenye hoja yako....ila nafikiri tumetofautiana....sijawahi kuona ndugu yangu akimuuguza mama yangu....waga ni baba na sisi wengine watoto wake.....nafikiri hiyo inategemea pia uhusiano alio nao mke na ndugu wa mumewe.....na mume pia ana uhusiano wa vipi na mkewe.....mimi hata nikiolewa ndugu zangu ni siwaachi nyuma.....nitawakumbatia kwa hali na mali,manake kwa lolote wao ndio wa kwanza pamoja na mume wangu na familia kunisaidia.
   
 7. LD

  LD JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo, ni kweli, kwamba bado tunawahitaji ndugu zetu/wazazi kwa karibu sana hata kama tumeolewa!!!
   
 8. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Sijui kama tabia hiyo ipo kwa kila familia. Lakini kama kweli ni tabia common, basi hiyo ni miongoni mwa athari za mfumo dume!
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wakati wowote ni vizuri kuwa karibu na ndugu!Ila kwasababu wao wapo tayari juhudi zinatakiwa kujiweka vizuri na ndugu wa mume...after all, kuolewa kwao kunawafanya na wao kua ndugu zako!
   
 10. LD

  LD JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa maana hiyo Michelle, tunatakiwa kujua kabisa majanga yetu tutakula na ndugu zetu siyo.
  Kwa maana ingine hatutakiwi kuachana na na ndugu zetu na kuambatana naye asilimia mia moja?..................sasa basi najaribu kupata jibu la kwa nini watoto wa kike wana roho ya kujali sana wazazi na ndugu zao wa damu................ni kwa ajili pia ya mambo kama haya au?
   
 11. LD

  LD JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hata mimi naona sio ktk kila familia au kila jamii.
  Lakini kuna kitu kama hicho nimekiona.
   
 12. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Liko wazi kabisa LD wala huitaji shule kujua hilo,give your husband family the best BUT never ever forget a bit where you come from and where you will always belong....wale wana damu yako my dear....wanaguswa sana na shida na raha zako.....
   
 13. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  kwa hiyo case yangu wanakuja tu kula kulala hakuna tatizo lolote na wameshazoea kama vile wapo kwao
   
 14. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Waswahili wanasema damu ni nzito kuliko maji!

  Pia kuna mtu mmoja alisema haya maneno wakati anauguza mke wake, na ndugu upande wa mwanamke wakawa hawajafika kumhudumia dada/mtoto wao; "Nyie wenye mtoto hamwonekani kuja kumuuguza, akifa mtampata wapi mwingine? Mie huyu ni mke wangu, akifa nitaoa mke mwingine". Kutokana na haya maneno ya huyu baba, ni rahisi sana kwa ndugu kuwa mstari wa mbele kumhudumia dada yao au mtoto wao, maana hakuna replacement yakitoea mengine! Kwa wengine inabidi wafanye kwa upendo tu, kama ni wifi; wanaweza kupata mwingine!
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa sijachunguza hiki kitu...
  Nafikiri ni moyo wa huruma tulionao na
  Ukisema nyumbani kwetu ndio kichaka cha matatizo nafikiri unakosea.
  Mwanamke ndio mhimili wa nyumba. Inabidi awe responsible kwa mambo yote ya kifamilia yanayotokea.
   
 16. Seto

  Seto JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 961
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hiyo ni kwa baadhi ya watu tu wala si tabia jumla ya jamii yoyote...
   
 17. charger

  charger JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 2,324
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Nafikiri mila,desturi,hali za maisha ya familia hizo kiuchumi ndio vinasababisha hayo.
   
 18. S

  Shauri JF-Expert Member

  #18
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mara nyingi inatokea,ila mimi nahisi ni upendo tu!
   
Loading...