Paspii0
JF-Expert Member
- Apr 10, 2020
- 638
- 1,038
"Akatupa vile vipande vya fedha hekaluni, akaondoka; akaenda akajinyonga."
(Mathayo 27:5)
Ni mstari mfupi, lakini wenye kishindo cha kimya kinachopasua nafsi.
Yuda hakusaliti kwa ujinga,alisaliti kwa kumeza ahadi ya muda na kupuuza kilio cha ndani.
Na leo, kivuli chake kinatembea katikati yetu.
Kizazi chetu kimejifunza kufunika aibu kwa marashi ya ustaarabu.
Tunaweza kuvaa tai za hekima huku dhamira ikiwa imechanika.
Tunaweza kushikana mikono kwa tabasamu, huku mioyo ikivuta visu vya hila.
Vipande vya fedha havibebwi tena kwa mikono,vinakuja kwa likes, ahadi, nafasi, au uzuri wa muda.
Wanaouza utu hawafanyi biashara sokoni,wanauza kwa ishara, vicheko, na miadi ya kimya.
Wengine huishi ndani ya ndoa lakini wamefungwa kwa pingu za tamaa,
huendesha familia kwa ratiba lakini si kwa moyo.
Na wengine ndiyo wanaketi kwenye viunga vya mamlaka, wamevaa suti za heshima lakini ndani yao kunalia njaa ya haki.
Sauti ya dhamira imegeuzwa mnong’ono.
Wachache wanaoisikia huonekana wazito, wa zamani, au wachochezi wa utulivu.
Lakini wao ndio walio hai kwa kweli,wale ambao bado hawajauza nafsi zao kwa bei ya sifa za muda.
Usaliti si tukio la ghafla,huanza kwa kucheka pale unapotakiwa kulia,
huanza kwa kukubali kile unachojua si halali,Huanza kwa kimya kinachogeuka kaburi cha nafsi.
Leo, kabla hujavua viatu hekaluni, jiulize,
Je, dhamira yako bado ina miguu?
Kabla hujapokea zawadi, uliza,
Je, nafsi yako itaweza kuilalia usiku?
Maana kuna kulala ukiwa umechoka, na kuna kulala ukiwa umejikwaa ndani.
Usijinyonge kwa kimya cha nafsi.
Rudi,hata kwa hatua ya huzuni,maadamu bado moyo unasikia.
Kwa sababu usaliti huua, lakini toba huponya.
~Chavalikungu