Mchongo pesa na Clouds wanajinufaisha na brand za Simba na Yanga

Mr. Marangu

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,565
1,516
Kuna katabia ambako huenda viongozi wa Simba na Yanga wananufaika wao binafsu nyuma ya Pazia. Iko hivi... toka Mwaka jana Clouds wamekua na tabia ya kukampenisha matangazo yao ya Bahati nasibu ya MCHONGO PESA kwakuhususha Simba na Yanga. Ieleweke unapotaja Simba au Yanga ni brand ambazo zimejengwa kwa muda mrefu nchini, tena brand hizi zinazokonga mioyo ya wafuasi wake mamilioni, hivyo Clouds kujikomboleza kwakutumia majina hayo nikama wanajinufaisha kwakutafuta kuungwa mkono kwa wingi na mashabiki watimu hizo.

Kibaya zaidi nikua hakuna taarifa rasmi zinazo onesha kuwa Simba na Yanga wanapokea kiasi gani cha fedha kutoka Mchongo Pesa, Viongozi wa Timu hizi kukaa kimya nikuhalalisha wizi huu ama laa hasha kuna mlungula wanaupokea nakuaamua kukaa kimya kumpisha mwanaharamu apite.

Timu hizi zimeendelea kuwa maskini kwakuongozwa na baadhi ya viongozi waliokosa maono yanayokwenda na wakati.

Nionavyo mimi Clouds kutumia jina la Simba na Yanga kwenye Kamari yao walipaswa kuzilipa timu hizo mamilioni.

Swali linalo umiza kichwa na kusikitisha ni "Timu hizi zikiwa na kampeni ya kuhamasisha mashabiki wakipeleka tangazo Clouds hawalipii?"Jibu ni wanalipia, Sasa kwanini Clouds ijinufaishe na majina ya timu hizi
Nihitimishe kwakusema viongozi waandamizi wa Simba na yanga ni MAMBULULA au wamekula mlungula.

Nb: hakuna taarifa yeyote ama press iliwahi kuonesha kuna mkataba kati ya Clouds na Simba au Yanga.
 
Back
Top Bottom