Mchina ajinyonga, ni baada ya kuboronga katika kazi Morogoro

Mchina ajinyonga, ni baada ya kuboronga katika kazi Morogoro

babo

Senior Member
Joined
Apr 9, 2014
Posts
194
Reaction score
23
Mchina mmoja alikua mkandaras wa daraja la kilombero kaamua kujinyonga baada ya daraja hilo kusombwa na maji,kaacha ujumbe unasema kua yey kaburunda ktk kaz yake ss kaamua kujinyonga ili aondoe aibu
--------------------------------------------------------------------------------

hanging_rope-300x278.jpg

Morogoro. Raia mmoja wa China ambaye ni mhandisi katika Kampuni ya Ujenzi ya China Railway Bureu 15 Group inayojenga Daraja la Mto Kilombero, Qin Bao Feng amekufa kwa kujinyonga kwa kile kinachodaiwa ni baada ya kuboronga katika kazi.

Ilielezwa kuwa Feng aliamua kujinyonga baada ya nguzo za daraja alilokuwa akilisimamia katika ujenzi huo, kusombwa na maji, jambo ambalo aliona kuwa limemvurugia kazi yake.

Baadhi ya watu waliokuwa jirani na kambi hiyo, walisema baada ya kuharibika kwa kazi hiyo, wahandisi wenzake kutoka China, walianza kumtenga hali iliyomfanya ajione kuwa mpweke na hatimaye kuchukua uamuzi huo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alisema tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita ndani ya kambi ya kampuni hiyo.

Alisema mwili wa marehumu ulikutwa ukining'inia kwenye dari ndani ya chumba alichokuwa analala na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo.

Kamanda Paulo alisema baada ya kuchunguza mwili wa marehemu walikuta karatasi iliyokuwa imeandikwa ujumbe kwa lugha ya Kichina.

Alisema kwa kuwa hakuna mkalimani aliyekuwa jirani na eneo la tukio, polisi wanaendelea kumtafuta mtu wa kuutafsiri.

Alisema kwa sasa mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya St Francis iliyopo Kilakala, Morogoro.

Kivuko chazuiwa

Wakati huohuo, Halmashauri za Wilaya za Kilombero na Ulanga kwa pamoja zimeamua kusimamisha kwa muda usiojulikana matumizi ya Kivuko cha MV Kilombero Two kuvuka Mto Kilombero ambao umefurika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Kusimama kwa kivuko hicho kumesababisha baadhi ya wasafiri kukwama na wengine kulazimika kuvuka kwa kutumia mitumbwi.

Huduma pekee ya usafiri kwa sasa treni ya Tazara ambayo inafanya kazi mara moja kwa wiki.

Kamanda Paulo alisema uamuzi huo ulifikiwa Jumapili iliyopita baada ya kiwango cha maji kuongezeka.

Alisema ushauri wa kusitishwa kwa kivuko hicho ulitolewa na wataalamu wa vyombo vya usafiri wa majini na kwamba boti zinazotumia injini na mitumbwi ndizo zinazotumika kuvusha watu.

Chanzo;Mwananchi
 
Mchina mmoja alikua mkandaras wa daraja la kilombero kaamua kujinyonga baada ya daraja hilo kusombwa na maji,kaacha ujumbe unasema kua yey kaburunda ktk kaz yake ss kaamua kujinyonga ili aondoe aibu
Sie tukibolonga husema 'Liwalo na liwe, hata kujiuzuru hatujiuzuru' , kwetu hutafsiri huo ndo ujanja wa kuishi mujini.......
 
Safi!!! Hawa wapo makini na very serious na kazi yao!!! Sisi siasa 904 elfu. Ila daah!! Mungu amsamehe na ampokee mahali pema mbinguni.
 
Mchina mmoja alikua mkandaras wa daraja la kilombero kaamua kujinyonga baada ya daraja hilo kusombwa na maji,kaacha ujumbe unasema kua yey kaburunda ktk kaz yake ss kaamua kujinyonga ili aondoe aibu
babo ni vizuri kusema ukweli. Taarifa iliyotolewa jana na kamanda wa polisi ni kuwa mchina huyo alijinyonga. Ujumbe alioacha ambao umeandikwa kwa kichina na tafsiri ya haraka isiyo rasmi kama alivosema kamanda ni kuwa "mchina" alijinyonga kwasababu ya ugumu wa maisha. Sasa suala la kuburunda kazi umelitoa wapi? Si vizuri kufanya upotoshaji maana wapo wengine ambao hawakuona na wanaweza kukuamini wewe kumbe sivyo.

Rai yangu, kumekuwa na mfumo wa kuleta wachina kufanya kazi huku kwetu na wakati huo pesa malipo yao wanalipwa kwenye benki zao huko huko kwao. Hili linawafanya wakati mwingine waishi maisha magumu ambayo yanawafanya wawe na stress. Huku wanapewa pesa kidogo ya kujikimu na kuhifadhiwa kwenye makambi (Sites). Ingawa kwa sera ya kitaifa ni nzuri maana wanahakikisha mzunguko wa hela unabaki china. Lakini kwa upande wa nchi yetu, hili linakosesha ajira nyingi kwa wazawa ambao wangeweza kufanya kazi zinazofanywa na hao wachina au wangefungua biashara maana mzunguko wa hela ungeongezeka. Wizara ya kazi iwemakini hasa vibali wanavyotoa kwa wafanyakazi wa kigeni. Wengi wao hawana ujuzi bali inakuwa kama sehemu ya kutafutiana ajira kwa wachina wenzao. Ukiangalia reports za EIA za miradi hiyo wanasema positive effects ni ajira kwa wazawa ama wa maeneo inakofanyika miradi au watanzania wengine. Lakini wakati wa utekelezaji hata ile kazi amabayo ingefanywa na mzawa anawekwa mchina 'SHAME TO MY POOR COUNTRY" Mamlaka husika haziwezi kusimamia hilo! Wahusika wamekazana kupokea rushwa toka kwao ili kuwapatia permits. Niliwahi kumzuia project manager wa kichina kuniletea wachina wasiokuwa na vyeti akiwemo yeye mwenyewe. Unamweleza akuletee vyeti vya kuonesha qualification za wafanyakazi wake ili uwaruhusu kufanya kazi kama mkataba unavyosema yeye anakuletea barua za kampuni kuwa hao ni watu wao wenye ujuzi na wamethibitishwa na kampuni zao.
 
Last edited by a moderator:
Alisema kwa sasa mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya St Francis iliyopo Kilakala, Morogoro.

Hiyo Hospitali ipo mtaa upi Kilakala?! Kilakala niijuayo haina hospitali sanasana Dispensary ya Tuwaenzi wazee na wala haina mochuari, Huu ni upotoshaji, hivi inawagharimu kiasi gani kuhakiki habari kabla hamjaandika gazetini?
 
Sawa mkuu nimekuelewa,ila mim nilsikiliza kupitia vyombo vya habari kwamba kaona ugumu wa maisha na kaz. ndio imemsababishia kuboronga kaz yak,ndivyo nilivyo sikia wakuu
 
Laiti kama tungekuwa na watendaji wanaojitathimini wao wenyewe kama hao! Nafikiri katika taifa hili tusingekuwa na kiongozi hata mmoja kati ya hawa tulionao.
 
hawa viongozi wetu wangeiga wanapokosea waji2ndike. Tanzania ingekuwa kama hongkong china.
 
Ddaaaahh..

Mkandarasi Kajinyonga, ila walio lipokea daraja hilo huku wakiwa thibitishie wananch wao kwa mbwembwe kuwa lina ubora, wao bado wanazunguka zunguka na viti maofisini..
 
Vijamaa vina staili nyingi za uwajibikaji ndio maana kwao vimeendelea
 
babo ni vizuri kusema ukweli. Taarifa iliyotolewa jana na kamanda wa polisi ni kuwa mchina huyo alijinyonga. Ujumbe alioacha ambao umeandikwa kwa kichina na tafsiri ya haraka isiyo rasmi kama alivosema kamanda ni kuwa "mchina" alijinyonga kwasababu ya ugumu wa maisha. Sasa suala la kuburunda kazi umelitoa wapi? Si vizuri kufanya upotoshaji maana wapo wengine ambao hawakuona na wanaweza kukuamini wewe kumbe sivyo.

Rai yangu, kumekuwa na mfumo wa kuleta wachina kufanya kazi huku kwetu na wakati huo pesa malipo yao wanalipwa kwenye benki zao huko huko kwao. Hili linawafanya wakati mwingine waishi maisha magumu ambayo yanawafanya wawe na stress. Huku wanapewa pesa kidogo ya kujikimu na kuhifadhiwa kwenye makambi (Sites). Ingawa kwa sera ya kitaifa ni nzuri maana wanahakikisha mzunguko wa hela unabaki china. Lakini kwa upande wa nchi yetu, hili linakosesha ajira nyingi kwa wazawa ambao wangeweza kufanya kazi zinazofanywa na hao wachina au wangefungua biashara maana mzunguko wa hela ungeongezeka. Wizara ya kazi iwemakini hasa vibali wanavyotoa kwa wafanyakazi wa kigeni. Wengi wao hawana ujuzi bali inakuwa kama sehemu ya kutafutiana ajira kwa wachina wenzao. Ukiangalia reports za EIA za miradi hiyo wanasema positive effects ni ajira kwa wazawa ama wa maeneo inakofanyika miradi au watanzania wengine. Lakini wakati wa utekelezaji hata ile kazi amabayo ingefanywa na mzawa anawekwa mchina 'SHAME TO MY POOR COUNTRY" Mamlaka husika haziwezi kusimamia hilo! Wahusika wamekazana kupokea rushwa toka kwao ili kuwapatia permits. Niliwahi kumzuia project manager wa kichina kuniletea wachina wasiokuwa na vyeti akiwemo yeye mwenyewe. Unamweleza akuletee vyeti vya kuonesha qualification za wafanyakazi wake ili uwaruhusu kufanya kazi kama mkataba unavyosema yeye anakuletea barua za kampuni kuwa hao ni watu wao wenye ujuzi na wamethibitishwa na kampuni zao.

kweli kabisa hasa hilo suala la kulipiwa katika bank za nyumbani kwao sijui kwa nini linaachiwa tu au halina madhara kwenye uchumi wa nchi yetu?
 
pale kariakoo palifanyika ukarabatii wa mitaro ya maji taka ya chini ya ardhi, katika ukarabati ule yalitumika mabilioni ya shilingi nandio ukarabati mmbovu kuliko yote iliyowahi kutokea, hapa nchini lakini hadi leo wasimamizi wa huo mradi wanaendelea kula vijisenti vyao.
 
Back
Top Bottom