Mchepuko unataka nimuache wife

Mchepuko unataka nimuache wife

Matatizo hayo ingia Uislam, umemaliza. Waislam wanaoana mpaka wanne, wewe na uwezo wako tu.

Na hauna haja tena ya kufanya dhambi ya uasherati kama ilivyo sasa.

Utaratibu ukoje kuingia huko?
 
Nimejikuta naona aibu kama hii mada ameileta kaka yangu jukwaani, huo ni uvivu wa kutafuta na kupenda vya kupewa na mara nyingi ukipenda vya kupewa basi unakuwa hauna maamuzi unapelekeshwa tu, Ushauri wangu mimi tafuta kazi sio mashirika yote yanayolipa 700,000 kuna mengine yanalipa ata 7million kwa mwezi, kwa mfano Kampuni za gas hizi, pili tafuta mtaji fungua biashara, mke wako ataisimamia hiyo biashara akimaliza short course yake, Usije ukasingizia hauna pesa ya kufungulia biashara kuna bank kibao zinatoa mikopo, chukua ata 3million weka kibanda ya MPESA,TIGO PESA utaendelea kaka yangu, huyo mwanamke anaekuhudumia hujamuweka ndani anakuwa mcharo sababu yupo nje, ukimuweka ndani utamkumbuka mwanakijiji wako, matusi yote ya mjini utayapata wewe mfano usinibabaishe kwanza mjini unakaa kwa nguvu yangu, huo ni ushauri tu akili kumkichwa

Ndugu hanihudumii, Ananiongezea pale nilipoishia, Changamoto za maisha ni nyingi, MTU unajaribu kila buzzness inashindikana na majukumu yanakusubiri
 
Rejea kichwa cha somo hapo juu

Wakuu nimedumu kweñye ndoa kwa miaka 11 sasa,

Hivi karibuni mchepuko wangu Wa miaka mingi unataka nimuache wife ili niuchukue wenyewe kulingana na mkataba usio rasmi tulioingia miaka kama saba hivi iliopita

Wakuu ipo hivi:
Nilipoingia chuo mwaka 2000 nilikutana na binti mmoja ambae baada ya mapenzi kunoga tuliamua kuishi chumba kimoja nje ya chuo hii ilitokana zaidi na uwezo mdogo aliokuwa nao darasani ivo tukaishi pamoja ili tupate muda mwingi Wa mm kumsaidia kimasomo

Tulidumu hivyo kwa miaka yote mitatu hadi tunamaliza chuo ahadi yetu ikiwa no kuoana

Baada ya chuo nilipata kazi na kuanza maisha ya Mtaani, naye pia alipata kazi tena ya maana sana kuzidi yangu

Baada ya miaka miwili ya kazi nadhan ilikua 2005, mama yangu aliniletea binti kutoka nyumbani kwetu ili nimuoe
Kutokana na mama alivyohangaikia ada yangu ya chuo kipindi nasoma nilishindwa kumkatalia

Maana alihangaika sana pale kijjini ikiwa ni pamoja na kupitisha bakuli

Hivyo 2005 nikamuoa huyo binti Wa mama bila kumpenda
Yule mchumba Wa chuo nikamweleza ukweli wrote aliumia sana na kuniita majina tote mabaya

2007 naye akaolewa na jamaa mmoja mwenye pesa kiasi

2008 tukajikuta shetani ametupitia tukaendelea na uhusiano kwa siri kubwa ikafikia hatua akadai tuwataliki watu wetu ili tuishi pamoja

Kiukweli mdada huyu amekua msaada mkubwa sana kwangu kiuchumi
Hii ni kutokana na ukweli kwamba mshahara wangu haukutani nikilipwa Leo wiki tu umeisha na bado mahitaji ndani ni mengi, na ukizingatia Nina watoto watatu na mke ni mama Wa nyumbani

Hivyo basi huo mchepuko ndio umekua uki fill hiyo gap ya mshahara
Kila mwezi ninapolipwa laki saba ya mshahara mchepuko huniongezea million moja kutoka kwenye mshahara wake Wa 2.5 hivo anabaki na 1.5

Mimi nakua na 1.7 kwa utaratibu huu nimeweza kujenga nyumba ya vyumba vitatu

Pia mchepuko hunisaidia mambo mengi sana, mfano mama alikua na kidney problem huyu mdada alifanikisha gharama kubwa tu ya matibabu

Mchepuko huu ndoa yake ina halo mbaya sana, mume kwa miaka mingi huwa anakuja home kubadilisha nguo tu na kupotea wiki kadhaa kabla ya kurudi tena kuchukua nguo na hadi Leo hawana mtoto yangu 2007 waoane

Sasa mchepuko umechoka kunisubiri ni malalamiko 24/7 kwamba tulikubaliana tuwaache watu wetu tuishi pamoja
Kiukweli mke wangu mwanzo sikua nampenda ila baadae nikajifunza kumpenda
Na hii imetokana na tabia yake nzuri

Ni mcha mungu, amekua mama bora Wa familia, hajawahi kunikosea makosa makubwa kama uzinzi

Kwa upande mwingine msaada Wa huu mchepuko bado nauhitaji, hiyo milioni moja ikiondoka nitabaki na laki saba yangu ambayo haitoshi ukichukulia kuwa watoto wote watatu wanasoma, mama yao nilimpeleka University computing center, sasa amemaliza certificate, then aendelee na diploma

Pia kuna mdogo wangu ametimuliwa kazi na sasa karudi kuishi kwangu hali ni tete

Wakuu nipo njia panda
Mchepuko hautaki kuendelea na status quo
In fact hivi sasa umeondoka kweñye matrimonial home umeenda kweñye nyumba yake
Shida ipo kwangu
Nifanyeje wakuu?

usifikiri yule jamaa unaemgongea mke wake hajui!!………subir siku si nying utakiona kilichomnyoa kanga manyoya!!
 
Acha uzinzi na umario wakati unamke wewe, tafata njia mbadala ya kuongeza kipato ili ndoa yako isiyumbe, utamletea magonjwa mwanamke wa watu kwasababu ya tamaa tu.

Mama sio tamaa ni bond iliyopo kati yangu na huo mchepuko
 
wanaume kama mabinti. kwa mtaji huu etu wanalalamika wanawake hawaheshimu waume zao kisa wamesoma.
ujinga huu mtu mwenye japo certificate hatoukubali
 
Dunia haiishi vituko. Kwa hiyo unachukua pesa za mchepuko kuendesha familia yako na upo very comfortable?

Kwa nn mwanaume anapompa mwanamke ndo inaitwa kusaidiana but vice versa in marioo!!!
 
Wangu eeee we..endelea kujipigia na sio kumwacha Wife wako!!!
 
Muache mkeo!!!! kwani bei gani kumuacha
 
unakosa baraka za kipato cha kutunza familia kwa sababu ya huo mchepuko. achana nae uone kama maisha yatasimama.
 
Hakuna kitu kikubwa kama Mungu kukupa watoto alafu unataka kuwatelekeza utapata laana itakuja siku itokee utalamba miguu ya mkeo acha tamaa full stop
 
ulisema hawana mtoto mzalishe muendelee hivo hivo kama anapenda ila usimwe mke wako huyo mana anakupenda ila muwekee biashara utafidia hyo gap na mambo yatakuwa mazur
 
Inaonesha kabisa elimu uliyopata haijakusaidia na pia hujitambui kabisa,kwanza kuletewa mchumba na mzazi ni utoto kwa mtu yoyote aliyekuwa matured,pili mchepuko utakutoa kizazi wewe dnt trust anyone,you dnt know kwa nini ndoa yake inayumba,na kazi gani anafanya hadi akupe wewe milion kila mwezi,jiulize mara mbili mwisho wa siku atakushauri umtoe kafala mkeo au mtoto,umeniboa na kwa shida zako lazima utamtoa,jipange na utafute pesa kwa jasho lako
 
Fikria na magonjwa pia maana umesema huyo mume wake huwa anapotea kwa wiki kadhaa sasa utajuaje kama huko alipo naye ana mchepuko?
 
Kama ni kujali utu inatakiwa nimuonee huruma huyu tuliyetokanae chuo ambae amejitoa kwa hali na mali
Mkuu ... Malipo duniani.. !! wewe ushajaaliwa mke,watoto na baba nyumba, mkuu shukuru hilo....
Usianzishe kasheshe au moto usiyoweza kuuzimisha!! (huyo Mchepko atapata kismati chake kwa wakati wake, Asikuzingue ktk maisha yako)
 
Back
Top Bottom