Mchepuko anataka anizalie mtoto

Mkuu wakati unasema mlikuwa mkila na kunywa kabla ya kwenda kuoana au kuzini na huyo bidada wa 27yrs umenikumbusha hili andiko

Mathayo 24:37-39
37. Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
38 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,
39 wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

Kwa hiyo akili kichwani mwako.
 
Mkuu baada ya kusoma hiyo mistari imebidi nicheke tu
 
Maamuzi yanakuwaje magumu sasa., Una mke na watoto 3 unashindwa kufanya maamuzi ya issue ya kijinga kama hiyo. Kweli ndio maana tunaburuzwa na wanasiasa.
Wewe jamaa una akili sana. Kula Tano kama nyogeza ya like nilokupa.

Hapa watu wanakazana kuuliza ushauri issue za kijinga. Kuja na mawazo ya ujenzi wa nchi na kuongeza kipato hakuna
 
Wewe jamaa una akili sana. Kula Tano kama nyogeza ya like nilokupa.

Hapa watu wanakazana kuuliza ushauro issue za kijinga. Kuja na mawazo ya ujenzi wa nchi na kuongeza kipato hakuna
ha ha ha ha mahusiano ndio yanayowafanya watu wapate nguvu ya kutafuta pesa
 
Mkuu baada ya kusoma hiyo mistari imebidi nicheke tu
Yaani mkuu umenikumbusha hilo andiko wacha kabisa.

BTW, usimwamini mwanamke itakugharimu, fanya uamuzi ukijua nini unakifanya na matokeo yake.

Kuna sentesi moja umeandika mwenyewe kuhusu nini alikwambia. Umesema,

Ataheshimu familia yako ....ila utunze mtoto. HILO NENO ila LINA MAANA KUBWA NA UJUMBE MZITO SANA.
 
Ni kweli mkuu umakini unahitajika sana
 
Waume achane kuchepuka mtafilisika na kuishia kuwa na depression,kila mwanamke anataka akushike uwe wake na umuhonge 😅😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…