Mchepuko amtelekezea mtoto jamaa

Mchepuko amtelekezea mtoto jamaa

adden

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
7,032
Reaction score
15,721
Wanajamvi mu wazima?

Katika mambo yote usije kuomba likutokee kama lililomtokea huyu jamaa, jamaa ana mke na watoto 3 sasa kuna msichana alikuwa anatembea nae hapo mtaa wa jirani bahati mbaya au nzuri mwanamke akanasa.

Jamaa akamkoromea yule mwanamama kwamba mimba sio yangu sababu we mwanamke una mabwana wengi hivyo kila mtu ashike 50 zake.

Mwanamke akaona isiwe tabu akaondoka zake kwenda kwao huko akailea ile mimba hadi akajifungua mtoto katoka kopi matata sana ya jamaa.

Alivyorudi akanyoosha moja kwamoja hadi nyumbani kwa jamaa kamkuta anakunywa chai na familia yake.

Akamwambia haya mwanao huyo hapo ukatae tena na mie nakwenda zangu! Hakuna aliepata nafasi ya kuongea wala kujibu!Sio mke wala mume.

Yule mwanamke akamwacha mtoto hapo na begi lake la nepi akaishia kaacha chai imekuwa chungu! Jamaa jasho linamtoka ashindwe cha kufanya. Sijui huo msala wanaumalizaje huko na mke maana mke hataki kusikia mtoto wa mke mwingine hapo.
 
fresh tu mbona mtoto analelewa,

Namshangaa sana mwanaume anayekataa mtoto
Atampeleka wapi maana mke hataki mtoto anasema mume apambane na hali yake!we unadhani huyo mke wa jamaa atakubali kirahisi
 
Mmh raha ya mtoto ninavyoijua mim nitelekeze mwang kwa bab ake akalelewe na mam wa kambo ningali nipo hai mim! Hapana aisee kweli uchungu wa mtot tunatofautiana
 
Mimi siwezi kukubali hata kidogo kwakweli... Noooo! Raha wapate wao kinyesi nifue mie... Ni no... Ningekuwa nimemkuta ata akiwa na siku mbili nalea
 
Niliwahi kuletewa mtoto na mke kwa mchepuko na mchepuko haukuwa unajua nina mke,mkuu samaki nilimuita aki!Tulikuwa off tumejilaza kwenye kapet uwiii sitaki kukumbuka that was 2000 na mtoto alikuwa na kama miezi kama 6 usiombe ya kukute,sina ushauri natafuta ada za watoto.
 
Back
Top Bottom