Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 505
- 887
Mgombea ubunge wa Rufiji wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mohamed Mchengerwa amewasilisha maombi ya wananchi wa jimbo hilo kwa mgombea mwenza wa urais wa chama hicho, Dk Emmanuel Nchimbi la Rufiji kuwa mkoa ili kurahisisha huduma.
Mchengerwa ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) amewasilisha maombi hayo leo Alhamisi, Oktoba 9, 2025 katika mkutano wa kampeni wa Dk Nchimbi uliofanyika Uwanja wa Soko la Tasaf, Nyamwage, Jimbo la Rufiji.