DCI ajitosa mchele wa plastiki

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,515

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Nipashe jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Rober Boaz, alisema kwa kuanzia, wanamtafuta kwa udi na uvumba mtu aliyerekodi video inayoonyesha kuwa amekutana na wali uliotokana na mchele wa plastiki kwa mamalishe maeneo ya Kariakoo, Dar es Salaam ili asaidie kutoa taarifa zaidi.


Alisema hadi sasa hakuna mahali popote palipothibitika kuwapo na mchele huo unaoelezewa kwenye kipande cha video inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.


Video hiyo inayomwonyesha mwanaume mmoja aliyevalia fulana nyekundu akielezea namna alivyolishwa wali wa mchele wa plastiki. Mtu huyo alijaribu kuthibitisha madai yake kwa kufinyanga tonge la wali, kisha akalipiga chini na likadunda kama mpira mdogo, maarufu kwa jina la ‘kitenesi’.


Video hiyo iliyoanza kusambaa kitambo kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, iliibuliwa tena juzi na kuongeza hofu kwa walaji. Wali ni miongoni mwa vyakula vinavyotumiwa na watu wengi jijini Dar es Salaam na kwingineko nchini.


Akieleza zaidi, DCI Boaz alisema wanaendelea kumtafuta mhusika wa video hiyo kwa udi na uvumba ili awasaidie katika uchunguzi wao.


DCI Boaz alisema wamelazimika kumtafuta mhusika wa video hiyo na wote walioshiriki kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu imekuwa ikiwapa hofu wananchi pasi na sababu.


Boaz aliwataka wananchi kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa kujiepusha na tabia ya kusambaza taarifa zisizokuwa na ukweli, akifafanua kuwa kufanya hivyo ni hatari kwa sababu huweza kusababisha madhara makubwa katika jamii.


“Kabla ya kuanza kusambaza taarifa kwanza uwe na uhakika na vyanzo vyako, wahusika wanaweza kuingia kwenye matatizo yasiyokuwa na msingi,” alisema Boaz na kuongeza:


“Tumeanza kuchunguza watu waliosambaza hiyo taarifa, lakini jambo la msingi ni kuujulisha umma (kwamba) wale wanaotumia hii mitandao wawe makini kwa kuweka taarifa zenye uhakika na siyo vinginevyo,” alisema DCI Boaz, akikumbushia kpande cha video cha kijana aliyejaribu kuuaminisha umma kuwa alikula wali wa mchele wa plastiki, ambao haushikani na mkono pindi unapofinyangwa na pia hudunda sakafuni kama mpira wa kitenesi.


WAZIRI UMMY ATOA ONYO
Akizungumzia kusambaa kwa taarifa zinazodai kuwapo kwa mchele wa plastiki wakati wa mahojiano yake na moja ya vituo vya redio juzi, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema ametaarifiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuwa hakuna mchele wa aina hiyo nchini.


Waziri Ummy aliwataka Watanzania kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii na taarifa wanazozipata kupitia mitandao hiyo ili kuepuka upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watu kwa nia mbaya.


"Hili la mchele wa plastiki, TFDA wameniambia haupo hapa Tanzania,” alisema Waziri Ummy.


MCHELE ‘FEKI’ NIGERIA
Desemba 21 mwaka jana, Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) liliripoti jana kuwa Nigeria imekamata shehena ya magunia 102 ya mchele wa plastiki ulioingizwa nchini humo na wafanyabiashara haramu ambao walitaka kuchangamkia soko zuri la wakati wa msimu wa sikukuu za Krismasi na mwaka mpya.


"Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mchele huo ulikuwa ni wa plastiki baada ya kuchemshwa, na kuoneka kuwa mkubwa zaidi ya mchele wa kawaida…ni Mungu tu anajua ni nini ambacho kingetokea kama ungeliwa na binadamu," Haruna Mamudu, Ofisa wa Forodha katika mji wa Lagos, alikaririwa na BBC akisema kuelezea shehena hiyo iliyotajwa kuwa ya chapa ya "Best Tomato Rice".


Chanzo: Nipashe
 
mchele wa plastic mbn tushauzoea
tokea enz izo skull

Sent from my Infinix HOT 3 LTE using JamiiForums mobile app
 
Sasa hapo kwenye kumtafuta kwa UDI na UVUMBA ndio kuna tatizo,mnamtisha Huyo jamaa kwani kakosea wapi???

Mseme tunamuomba aje.
 
Viongozi wetu bana wana shida sanaaa,badala ya kuanza upelelezi ili kujiridhisha na taarifa iliyopo wao ndio kwanza wanaanza vitisho juu ya matumizi ya mtandao

Hii nchi sinema haziishi hasa kwa viongozi wetu,kwa vitisho hivi sidhani kama watapata ushirikiano wa kutosha kwa wananchi
 
Halafu watu wanasema Tanzania njaa tupu wakati siku hizi fasheni mtu ananunua ubwabwa kwa mama lishe anakula akiona ameshiba, anachukua tonge anafinyanga na kudundisha eti plastiki kama kweli mtu amekula cha plastiki si ajitokeze kuisaidia isiloq.


sent from my Samsung smart tv using JamiiForums
 
Back
Top Bottom