Mchecheto


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,977
Likes
5,351
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,977 5,351 280
pix.gif
1267855583_w.jpg

Na Mwandishi Wetu
Mchecheto wa Uchaguzi Mkuu 2010 umeanza kushika kasi, mpya yenye moto ni kuwa baadhi ya wagombea nafasi ya ubunge walioweka kambi yao Dar, wamechanga shilingi milioni 40 na kuita jopo la waganga wa jadi kwa lengo la kusafisha nyota zao...
Habari za ndani zinasema kuwa, mtandao wa wagombea hao, maskani yao ni wilaya ya Temeke, Dar na mara nyingi hukutana nyakati za usiku kwa ajili ya kuratibu mipango yao.

Mmoja wa waganga wanaofanya shughuli hiyo alisema kuwa timu yao inaundwa na wataalamu kutoka Sumbawanga mkoni Rukwa, Handeni na Lushoto mkoani Tanga, Kigoma, Tabora, Kagera na nchi jirani.

Mganga huyo kwa sharti la kutotaka jina lake ‘lichorwe’ gazetini alisema kuwa, timu ya waganga hao kutoka mikoani wameungana na wale wa nchi za Nigeria, DRC, Congo Brazzaville, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Senegal kwa lengo moja tu, kukamilisha kazi hiyo ya kusafisha nyota.

“Jumla tupo kama 23, mchana ni amani lakini mambo yetu ni usiku. Tumepewa kazi ya kuwatengeneza hawa wagombea ili wawe na nyota safi ambayo itasababisha wakubalike kwa urahisi mbele ya wapiga kura,” alisema mganga huyo.
Aliendelea kusema kuwa, mpaka sasa idadi ya mabosi wao (wagombea) hawajainyaka kwa sababu kila siku wanajitokeza wapya lakini akataka gazeti hili lielewe kwamba wapo wengi.

“Ni wengi kila siku wanajitokeza wapya ila mkuu wao ambaye yeye ni mfanyabiashara mmoja hapa Dar ametueleza kuwa ‘oparesheni’ nzima wameiandaa kwa shilingi milioni 40, tutakuwepo Temeke wiki mbili,” alisema.
Mganga huyo alisema kuwa, wagombea hao wanaosafishwa nyota mpaka sasa wengi ni wale wanaosaka majimbo kwa mara ya kwanza, yaani hawajawahi kuwa wabunge.

Hata hivyo, mganga huyo alisema kuwa, tangu alipoungana na wataalamu wenzake, amewahi kumshuhudia mbunge mmoja tu ambaye jimbo lake la uchaguzi lipo Kanda ya Ziwa.

“Wengi ndiyo kwanza wanataka majimbo kwa sababu wakija mbele yetu ni lazima tuwaulize maswali ili tuwajue na tujue jinsi ya kuwatengenezea dawa. Mpaka sasa nimemuona mbunge mmoja tu ambaye ni … (anataja jina) naye alikuja mara moja, hakurudi.

“Hatujui huko mbele watakuja wangapi ila bosi kabisa aliyetualika kwa ajili ya kazi hiyo alituambia kuwa, ni timu kubwa ambayo imejiandaa kimtandao na kwamba hata mawaziri wamo,” alisema mganga huyo.

Kutokana na hali hiyo, mganga huyo alisema kuwa, baadhi ya wabunge wapo shakani kwa sababu wao si kwamba wanasafisha nyota za wateja wao bali pia wanazichafua kama si kuzidhoofisha zile za wapinzani wa ‘wanene’ wao.
Aliyataja baadhi ya majimbo ambayo yanapigiwa mahesabu na wateja wao ambao wanautaka ubunge kwa mara ya kwanza kuwa ni Kinondoni, linaloongozwa na Idd Azzan huku kukiwa na fununu kwamba Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka na Meneja Uhusiano wa NMB, Shyrose Bhanji wanalihitaji.

Mbali na hao, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zubeir Kabwe hivi karibu alitengenezwa vichwa vya habari katika vyombo vingi baada ya kutangaza kwamba miongoni mwa majimbo ambayo anayapigia mahesabu 2010 ni Kinondoni.
Lingine ni Ubungo ambalo linanyatiwa kwa karibu na kijana wa CHADEMA, John Mnyika pamoja na wale wanaopiga hatua za chini kwa chini, bila kusahau Temeke linaloshikiliwa na Abbas Mtemvu.

Jimbo lingine linalotazamwa kwa jicho pembe na timu ya wabunge waliokodi waganga wa jadi hao ni Kawe linaloongozwa na Rita Mlaki, huku Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na ‘Strong Young Lady’ wa CHADEMA, Halima Mdee wakitajwa kulifukuzia.

Jimbo la Karatu linaloshikiliwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Wilbroad Slaa, Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, Mkuranga, Adam Malima nayo pia yanapigiwa ‘jeramba’.

Majimbo mengine ni Kigoma Kaskazini, linaloshikiliwa na Zitto, Kigoma Mjini, Peter Serukamba, Same Mashariki, Anne Kilango Malecella na Hai ambalo tayari Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amekwishaweka wazi nia yake ya kulitwaa.

Gazeti hili lilipozungumza na Mnajimu mwenye jina kubwa nchini, Sheikh Yahya Hussein kuhusu ukweli wa waganga hao kusafisha nyota ya baadhi ya wagombea, alisema kuwa, anavyoelewa hakuna mganga mwenye uwezo wa kusafisha nyota ya mtu Tanzania ispokuwa yeye tu.

“Kama hao wamekuja kwa ajili ya kazi hiyo basi shauri yao, lakini ninavyojua mimi hakuna mtaalam wa kusafisha nyota ya mtu nchi nzima hii ispokuwa mimi,” alisema Sheikh Yahya.
 
Injinia

Injinia

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
850
Likes
4
Points
0
Injinia

Injinia

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
850 4 0
Nonsense!! Kwanza wasafishe nyota zao wenyewe manake wao wenyewe wako katika hali duni!!

Wakimaliza wasafishe na nyota ya Tanzania basi
 
Fisherscom

Fisherscom

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2008
Messages
1,486
Likes
285
Points
180
Fisherscom

Fisherscom

JF-Expert Member
Joined Mar 13, 2008
1,486 285 180
'Tawire' wabunge watarajiwa. Naona mnazingatia ule usemi wa 'biashara asubuhi jioni mahesabu'. Uchaguzi 2010 kazi ipo tutaona na kusikia mengi.
 

Forum statistics

Threads 1,238,898
Members 476,226
Posts 29,336,070