Kuna kipindi M/kiti alijaribu kubalance Ukabila akamleta kijana toka Tarime na kumweka pale makao makuu Kama Msaidizi wake Lakini kwa kutojua Yule kijana akaandika kitabu cha kumbukumbu cha Maisha ya Chacha Wangwe kimya kimya pasipo kujua kuwa Mkiti Kuwa hapendi Msaidizi wake amkumbuke Chacha Wangwe yule kijana Siku alipotaka kukizindua kitabu tu M/kiti akajua ni Siku hiyo hiyo akamfukuza toka makao makuu na kupata Misuko suko ambayo haifai kuhadithia kwani hadi lap top yake iliporwa huyo kijana amehamia NCCR ukitaka akupe story nenda pale NCCR muulizie Yule kijana aliyetunga kitabu cha Maisha ya Chacha Wangwe watakuonyesha muulize maswali yote utapata jawabu.
kwan zito akibaki kuwa mwanachama wa chadema na mbunge wa chadema kuna tatizo gani.......kauli zenu za zito kashinda na uongoz umeshindwa hazina mantiki ...kwan kulikua na mashindano gani?
Nzilo
Hukohuko fb ukiangaliA magroup na page za maana zina watu wachache sana, Lakini Magroup na page za kipuuzi zinawafuasi wengi sana.
Mfano page ya Zitto ina watu 30,000 lakini page ya Mzee wa Utamu ina watu 100,000.
Hope kuna cha kujifunza hapo.
ipo siku utaufahamu umuhimu na ushawishi wa ZZK siyo sasa..... kipindi chama kitakapokuwa kimepoteza mwelekeo na si muda mrefu.... labda tu hali hiyo CDM wainusuru kwa kutomfukuza uanachama ZZK..... "Maumivu ya kidonda cha mtu ayajua mwenye nacho..."
Kuna tatizo kubwa Chadema, weledi umeenda safari, weledi utakaporudi utakuta chama kiko chali. Sasa angalia wapenzi wa Mbowe na Hoja zao very low. CC ya chama ndio utafikiri walilewa kwanza ndio wakaingia kwenye kikao.
Hakuna mtu mwenye uelewa wa kawaida tu anaweza kukubali mashtaka ya uongo na ya kutunga kama haya. Naamini hata akina Dr. Kitila na Mwigamba wakienda mahakamani watashinda pasi na shaka.
Wanashabikia dhuluma chama kinaanguka. Mbowe na Dr. Slaa wanakiua chama mchanamchana sijui ----------!
Khaa!!!! ZZK hapiganii uanachama bali anapigania haki itendeke. Siyo mnakurupuka tu kama mlivyozoea mkidhani ndiyo utaratibu. Mbowe, Slaa, Lema na vijibwa vyao walaumie kwa kuua demokrasia nchiniThen what? atafanyakazi na katibu yupi? M/Kiti yupi?...wajumbe wepi? kwanini msiwe wakweli wa nafsi zenu kuwa amefanikiwa kutetea posho zake za ubunge na uenyekiti wa PAC? Mlarushwa mkubwa kama Zitto kuwa M/Kiti wa kamati ya Bunge i.e watch dog committee inayochunguza mashirika ya umma huoni kuwa kuna walakini?...kweli wajinga ndio waliwao...Mahakama ilikuwa haina namna zaidi ya kuitikia wito wa Rais na Mwenyekiti wa CCM... Ukweli huu utasimama mpaka siku ya mwisho wa dunia kuwa Zitto si Msafi na CCM wako nyuma yake kujaribu kudhoofisha upinzani... After all in saltation Zitto atasubutu kumwangalia Mbowe na Viongozi wake kweli...Kijana aliechukuliwa kibohehe secondary alikokuwa anashindwa hata kwenda likizo kwa kukosa nauli leo anauwezo wa kuingia kwenye propaganda chafu ya kumchafua master wake ? Anazuia harakati za kuokoa Tembo, Madini na Gesi mali halali ya Watanzania? ama kweli kizazi cha nyoka itaendelea kuwa kizazi cha nyoka hadi mwisho wa dunia...
Kwani lengo la CDM ni nini hasa....?
Mchawi wa CHADEMA ni UOngozi wa CHADEMA
Metahli ya "mfa maji haachi kutapa" ndo yanatimia.....
sasa mara CCM mara CUF hivi hata kwa akili ya kawaida hatuwezi kuyaona haya matatizo yaliyopo kwenye uongozi wa juu au tunafumba macho na kushabikia ujinga.....
hakuna mchawi nje ya CHADEMA, mchawi yumo ndani ya kamati kuu na baraza la ushauri wa CHADEMA... mi nashauri wakae chini na kujitathimini ndani ya chama na ikiwezekana matatizo yao wayamalize kwa kushirikisha watu wenye busara nje na ndani ya chama na wenye uwezo wakuona mbali na ikiwezekana Viongozi wapate msasa wa elimu ya Sayansi ya siasa (Political Science.....)
Ninachokiona ndani ya CHADEMA ni Poor management of the Organization... Mtaalamu mmoja wa mambo ya Utawala Maxwell katika kitabu chake cha "The 21indispensable laws of a Leader" anashauri kuwa kama Kiongozi (Leader) unatakiwa kujifunza namna ya kuongoza kupitia migongo wa watu wenye ushawishi katika Taasisi yeyote suala hili kwa CHADEMA naona kama halipo....
Umesema ukweli mkuu lakini unadhani ni nani atakaeye kusikiliza maana viongozi wa juu wote wapo kwenye maslahi zaidi na ukabila ni ukweli usiopingika
Kwa uelewa wangu mdogo.... lengo la chama chochote duniani kinachokua ni pamoja na kuongeza wanachama ili kiweze kushinda uchaguzi na si kupunguza wanachama.... sijui kama unalielewa hili?
haina maana yoyote kuwa chama chenye wanachama wapuuzi kama Zitto
You are rigid bro...!!! Jifunze kuukubali ukweli hata kama unaumiza.... coz kumbukumbu zangu zinaonesha kuwa kuna siku Mbowe aliwahi kumkubali Rais na kumuita Mh. Rais kwa mara ya kwanza baada ya kusema hamtambui baada ya uchaguzi wa 2010.... na siku hiyo alisema hivi "mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpe..." hivi ni mtanzania gani aliyeshuhudia jitihada za ZZK anaweza kumuita mpuuzi????