Mchawi akwama hapa Ilula Iringa

Ivi ni lazima wajipake masizi mwilini na kuvaa nguo nyeusi na red?
Wachawi nijibuni!!
cc mshana jr
 
Hakuna lolote huu ni usanii tu wa kutaka kupata wafuasi kwenye dini utasikia ameombewa ndio maana akakwama.Hakuna mtu anaweza kuruka angank kwa ungo.
 
Hii sayansi ajabu sana, yaani hako kaungo mtu ana move from one place to another.
Wakati wengine wanajipaka make up waende kwenye sherehe mbalimbali kuna wapumbavu wengine wanajipaka majivu ili wapae usiku.
 
Mwisho wa mwezi twende kwa babu
 
Huo ungo hapo umepaa??? Au mi nina makengeza?
Huyo amekwama akiwa katika safari zake.. Kuna vitu vingine hutakaa uvishuhudie mpaka unakufa kwa kupitia macho ya nyama, lakini unatakiwa uamini kama vipo.

Wapo watu waliopewa uwezo wa kuwaona wachawi wakifanya yao live lakini wewe usiweze kuwaona kwa sababu huna uwezo huo.

Usiyaamini sana macho yako kwa kudhani kwamba yanaweza kuona kila kitu. Macho yetu yana pazia mkuu ambayo linatuzuia kuona visivyoonekana. Kumbuka kuna ulimwengu wa nyama na ulimwengu wa roho.

Utaona bendera inapepea lakini kinachofanya bendera ipepee usikione, je hiyo inamaanisha kwamba hakuna upepo?
 
Hakuna cha mganga wala nn, huyo kapita anga lenye nguvu zaid yake , Gravitation force ikamvutia chini
Hakuna kitu kama hicho kwanza Mchawi akisafiri usiku mwili wake anauacha kitandani kwake roho ndio inayo paa..Hiyo ni cinema.hakunaga kitu kama hicho
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…