Njemba anasa kwenye dari akidaiwa kuiba

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,806
34,193
Mwizi-1.jpg
Njemba huyo akiwa juu ya paa.


Na Francis Godwin,

Risasi Jumamosi

IRINGA: NJEMBA mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi, amenaswa juu ya paa la duka la kuuza simu mjini hapa akidaiwa kutaka kuiba.

Tukio hilo lilitokea Jumatano iliyopita, majira ya saa 1 asubuhi baada ya wasafiri wa stendi ya mabasi yaendayo mikoani kushtushwa na sauti ya jamaa huyo aliyekuwa akiomba kuokolewa.


Mwizi-2.jpg


Akielezea tukio hilo, mmoja wa mashuhuda, Juma Ally, alisema akiwa anapita eneo hilo alishtushwa na sauti ya jamaa huyo aliyekuwa akiomba msaada wa polisi.

Alisema alikuwa akipaza sauti kuomba wasamaria wema kwenda kituo cha polisi kumuitia askari wa kuja kumkamata jambo ambalo walilifanya na polisi wakafika kumkamata.

Mmiliki wa duka hilo, Lusungu Matelephone alisema kuwa si mara ya kwanza kuibiwa katika duka lake hivyo ni dhahiri kijana huyo naye alikuwa anataka kuiba.


Mwizi-3.jpg


Baada ya kutiwa mbaroni.

“Huyu alikuwa anataka kuiba, wakati akijaribu kujirusha ili kuingia ndani alijikuta akinasa kwenye dari kutokana na paa la nyumba hiyo kuimarishwa kwa nondo.

“Alikuwa na wenzake na baada ya kuona kanasa hashuki chini wala kupanda juu waliamua kukimbia kutokana na kuona asubuhi imefika bila mwenzao kuchomoka,” alisema Lusungu.

Lusungu ambaye ni mkazi wa Kilolo, alisema mbali na jamaa huyo aliyenasa kuchukuliwa na polisi, pia mwenzake mmoja alikamatwa majira ya jioni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Peter Kakamba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa jina la mtuhumiwa limehifadhiwa kutokana na msako unaoendelea kupata washiriki wenzake.Njemba anasa kwenye dari akidaiwa kuiba
 
Back
Top Bottom