Mcharuko: Mke awa housegirl...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Katika hali isiyo ya kawaida,mke wa ndoa wa jamaa mmoja mtaani kwetu hapa amegeuka kuwa House girl ghafla.

Ilikuwaje?
Jamaa mwenye mke pamoja na mke wote ni wafanyakazi wa Maofisini-mume ni wa Serikalini na mke ni wa Kampuni binafsi.

Hawana mtoto kwa sasa kwakuwa watoto wao wawili wako shule za Bweni. Wanaye Housegirl tu nyumbani. Siku ya tukio na mwanzo wa kituko,mume alianza kutoka mapema mno nyumbani kuwahi kazini.Mke naye alifuata wakimwacha Housegirl akiendelea na shughuli zake za kila siku. Kiujanjaujanja, mume alirudi nyumbani majira ya saa tatu asubuhi hivi.

Katika hali isiyotegemewa, mke alisahau Document muhimu sana nyumbani. Akapewa na Bosi wake muda mfupi wa kukimbia nyumbani ili ailete Ofisini. Alipofika nyumbani, alimkuta live mume akila raha na Housegirl barazani huku wakisikiliza vipindi vya DSTv. Mke alijifanya kama hawaoni, alielekea iliko document, akaichukua, akarudi ofisini.

Tangu siku hiyo, mke amekuwa ndo Housegirl kwa ridhaa yake na hajawahi kuuliza. Mume anatishwa na msemo: Kimya kingi kina mshindo mkuu. Anaweweseka,hajui afanyeje.

Msaidieni kwa mawazo...
 
adisi adisiiiiiiii, adisi njoo , uwongo njoo utamu koleaaaaaaaaaaaaa.
Apo dhamani dha kale, alikuwepo mtoto mmoja, akaenda, akaenda akaenda, akendaaaaa weeeeeeeeeeee. Na adisi yangu imeisha.
 
Hii story kama ni ya kweli basi huyo mke ni mjinga sana kujifanya housegirl.
Asijiadhibu kwa sababu ya ufirauni wa mumewe. Ampe fundisho lingine na siyo hilo.

Huyo bwana naye ni mjinga kusumbuliwa na hicho kimya.avunje ukimya ajue kinachoendelea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom