Mchango mzuri sana na kwa kiasi kikubwa nakubaliana nawe Zitto.
Hata hivyo napata shida na nimeshituka sana hili la 46% pekee ya walimu walioko shuleni kuwa ndiyo wanafundisha!!
Maana yake ni kuwa 54% ya hawa walimu wako kazini lakini hawafundishi. Nini maana ya hii kiuhalisia?
Je, wapo tu na ukiwaona wanaingia darasani lakini badala ya kufundisha wanapiga soga au.....?
Je, ni kwamba hawapo kazini kabisa na wanakuwa wapi ili hali wanalipwa mishahara kwa ajili ya kufundisha?
Je, sio kwamba kuna usimamizi kuanzia ngazi ya shule yenyewe, kata, wilaya, mkoa na hadi wizara ya elimu na pia wagakuzi? Wote hawa hawamwoni huyu mwalimu asiyefundisha watoto wetu?
Au hii ina maana tofauti na nilivyoelewa mimi kwamba, labda walimu wapo kazini lakini wakiwa ni watumishi waliokata tamaa kutokana na grievances zao mbalimbali na hivyo kukosa morali ya kazi kabisa?
Kama hili la mwisho ndilo, basi hili ni tatizo kubwa sana. Na tatizo haliko kwa walimu pekee wanaotakiwa kuingia darasani na kufundisha bali liko kuanzia kwa wasimamizi/viongozi wao kuanzia ngazi ya shule hadi wizarani kote ni tatizo na wanalalamika na kunung'unika tu na hii ndio inafanya 54% ya walimu kuonekana hafannyi kazi/ hawafundishi na hawasimamiwi kwa sababu hata wanaopaswa kuwasimamia nao wanalalamika!!
Hili ni tatizo tena kuuubwa sana...