Mchango wa Zitto katika Wizara ya Eimu na Mafunzo ya Ufundi

Mchango wa Zitto katika Wizara ya Eimu na Mafunzo ya Ufundi

Walimu watafurahiiii, anyway Zitto yuko sahiii na binafsi yangu namkubali Sana.

Wakifanya hivyo vijana wengi wenyewe akili watakimbilia mashuleni fundisha tofauti na sasa ambako sekta ya Elimu imekumbatia Malofa wengi yaliyofeli eti kufundisha watoto wetu.
 
Wabunge walipwe laki tatu kwa mwezi.Sitting allowance zifutwe.Kama kweli wanampenda"Mama Tanzania.
 
Hakuna mfanyakazi atakaefanya kazi na kudeliver kwa ufanisi ikiwa mwajiri wake hamtimizii matakwa yake au "ananyonya" jasho lake.
Walimu ni watoa huduma, na wateja wao ni wanafunzi. Usitarajie wawaridhishe wanafunzi ikiwa wao hawakuridhishwa na mwajiri wao.Nani asiejua malalamiko ya walimu?imefika wakati mpaka wanafunzi wanajuwa malalamiko ya walimu wao,lakini anaelalamikiwa "ametia pamba" masikioni.
Elimu itaendelea kushuka na wala tusitarajie ipande hata kama mlalamikiwa ataamua kuweka "washika bunduki" kila shule wawasimamie walimu,HAITASAIDIA.
Mwalimu anapofanywa kuwa "second class" employee halafu unatarajia yeye atoe "first class" product, huu ni aina mojawapo ya "wenda-wazimu"

Yes, nakubaliana na wewe kwa asilimia zote, kwamba, walimu wana matatizo mengi sana na ya msingi na mwajiri wake ni aidha ametia pamba masikioni hataki kuyashughulikia/kuyatatua au hajui kuwa kuna matatizo kama hayo (jambo ambalo ni gumu kuliamini kama haijui)!!

Mfano ni aibu sana kwa serikali kutolipa madai halali inayodaiwa na walimu kama vile malimbikizo yao ya mishahara, fedha za matibabu au masomo, fedha ya likizo au kutowapandisha vyeo ili wapate increament ya mishahara yao.

Ukisikiliza sababu zinazotolewa na serikali wala hata hazi hit kwenye vichwa vya watu wanaofikiri vyema. Mathalani unakuta wanabishana na walimu kulipa madeni yao kwa visingizio kama uhakiki kwa sbb inakuwa haiamini kama inadaiwa kiasi fulani. Cha kushangaza uhakiki huu unakuwa unafanyika miaka na miaka huku madeni yakizalishwa!!

Hii ni wazi inashusha morali ya utendaji kazi wa walimu hawa na wakiamua kutotimiza wajibu wao kikamilifu, wanaweza na matokeo si rahisi kuyaona papo kwa papo bali taratibu yatajitokeza ktk jamii kwa aina ya wahitimu inayozalishwa kutoka ktk taasisi zetu za kielimu na baadaye tunaanza kutafura mchawi lakini ukweli ni kuwa mchawi ni serikali chini ya CCM ambayo haijaweka misingi na sera mathubuti za elimu na ualimu!!
 
Elimu na afya tufanye kama nchi jirani kwenye suala la elimu kusiwe na tofauti kubwa kati ya public na private school
 
Aijakosea kumwamini huyu jamaa.
Huwa anasoma saana kabla ya kuchangia... Huyu ni kichwa kwa kweli. Tuache uchamachama....
 
mawazo haya ya zitto ni sawa na wabunge 59 wa ccm. serikali ingefanyia kazi mchango huu wa zitto bungeni...
Hawawezi kwana hawana nia hasa ya kubadili ubora wa elimu ya Tanzania. Wanaleta usiasa tuu..
Kama ingekuwa wana nia hasa na elimu ya tanzania kuwa bora, ni rahisi sana,.
Ila hongera yake zito...
 
Mnafiki tu, hafai, pumba tu za kinafiki. Hawezi kuifundisha serikali.
 
AKILI KUBWA
Kweli mkuu nakubaliana na wewe Zitto Kabwe ni zaidi ya akili kubwa,kuna watu waliapa kwamba watafanya mbinu zote ili Zitto Kabwe asirejee bungeni lakini waliishia kuumbuliwa na wanakigoma.
 
Kuna mengine zitto yuko sahihi. lakini hajazungumzia ukosefu wa walimu wa masomo ya sayansi na hisabati katika sekondari zetu. shule nyingi hasa za kata hazina walimu wa kutosha wa kufundisha masomo hayo. hili linashusha ufanisi. sijaona jitihada za serikali katika kupambana na hili.
Hamna mtu anayeweza kuzungumza yote kwa dakika 10,ila lazima tukubali hotuba ya ZZK ni bora mara milioni ya waziri kivuli...badala ya kutoa hoja mbadala yeye kajaa upepo na uchaguzi 2015 ili amfurahishe Lowasa na uchaguzi wa Udom...amedhalilisha wanachadema sana...ni sawa tu na Mh.Kessy aliposema wabunge CHADEMA wana akili za kuku.
 
Matatizo yanayofanya elimu yetu izidi kushuka ni mengi mno ukimtaja mwalimu tu mchango wake katika kushuka kwa elimu utajaza kaunter book japo chanzo kikuu ni sera na maslahi toka serikalini, Zitto kasema ukweli serikali ishindwe tu kuyafanyia kazi.
 
Hongera zitto..najua watakao kupinga ni wale wa sanamu ya Diamond na yule aliyetumia miaka 26 kusoma la kwanza mpk form 4.
 
Back
Top Bottom