Mchango wa Mwenge ni lazima?

Kichwa Ngumu

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
1,726
312
Heshima kwenu
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe bwana Mrisho Gambo amewatangazia wananchi wa Korogwe kuchangia gharama za mwenge kama ifuatavyo
  1. Wafanya biashara sh. 5,000.00
  2. mwananchi wa kawaida sh. 1,000.00
watendaji wa kata wameanza kupita kwa wafanya biashara hao kwa kukusanya fedha hizo, kwa bahati mbaya watu hawapo tayari kuchangia kwa sababu hawana hela na watendaji hao wamekua wakichukua majina ya waliyokataa na kuyapeleka kwa DC na kuwatishia kuwa wataona moto wa wa DC huyo.

Je, Mchango wa Mwenge ni lazima?
 
sio lazima bali wananchi wanatakiwa kuhamasishwa kuchangia walionacho wanatoa wasionacho hawatoi...... hao ni matepeli katoeni taarifa kwa DC ili atoe kauli yake.
 
Wananchi hawajaupenda mwenge kwenda kwenye maeneo yao kwakuwa hauna maana kwao. Wananchi waachwe wahangaikie maisha yao ambayo ni magumu sana, mwenge ni wa nini wakati huu.
 
Kipindi cha kukimbiza mwenge "is another silly season". Nani ana-audit hizo fedha wanazonyang'anya watu? Ni swala la 'MWALIMU USINIBAINI WAJINGA NDIYO WALIWAO,NIKIPATA MBILI MOJA YAKO MOJA YANGU"
 
Back
Top Bottom