Wewe sio mbaguzi wa dini za wengine?Kama sio Dini mie nilikuwa Mtu mbaya sana.
Ila tangu nilipoanza kusali ,
Mambo yangu Mengi yalibadilika.
Nikaanza kuheshimika, kupenda watu, kuona shida za wenzangu kuwa ni zangu.
Kwa ufupi dini zina msaada mkubwa sana kwa mwanadamu kumtafuta MUNGU
Sali Sana brother, nina uhakika uhuni na maisha niliyoyaishi, hata nusu hutafika ila ni Mwenyezi Mungu anayejua, sali sana nasema tena sali sana.Dini ina mchango gani katika kuwatendea binadamu wenzako haki, kuwathamini na kuboresha maisha yao?
Dini yako inakuongoza au unaipa kipaumbele katika kuratibu matendo yako na binadamu wengine wanaokuzunguka?..
Mie sibagui Dini ya mtu, wote ni wa MunguWewe sio mbaguzi wa dini za wengine?
Dini imeleta mazuri na mabaya ila kimizania mazuri ni mengi zaidi.Sali Sana brother, ni nauhaukika uhuni na maisha niliyoyaishi,hata nusu hutafika,ila ni Mwenyezi Mungu anayejua,sali Sana nasema tena sali Sana...safari ya Kristo kuiomboa dunia siyo historia,na ni mwemdelezo, Nashukuru Kristo alitufikia,ingawa waliotuletea habari njema walikuwepo wazuri na wabaya pia(agents of colinialism).Ila tunashukuru ,Sali Sana na ukamuegemee Kristo Mfalme wa wafalme.
hata username lako limesadifu yaliyomo!!Kama hauna misingi ya Dini inayokuongoza. Utafanya .mambo ya Ajabu Sana..hata Mimi niliyofanya najutia Sana Sana Sana.. lakini namshukuru Mungu kwa kuniongoza nimeiona Nuru.
Japokua na dhambi zangu nyingi mfano wa bahari ya Hindi..bado Mungu amenivusha katika majaribu makubwa Sana..
Na kwaimani yangu ntavuka na hapa nilipo.
Unaelewa maana ya hiyo ID wewe..au unkurupuka tuhata username lako limesadifu yaliyomo!!
Naam, naam.Mjomba Kiranga tupe mawili matatu hapa
Kama si dini hii dunia pangekuwa ni uwanja wa vitaDini ina mchango gani katika kuwatendea binadamu wenzako haki, kuwathamini na kuboresha maisha yao?
Dini yako inakuongoza au unaipa kipaumbele katika kuratibu matendo yako na binadamu wengine wanaokuzunguka?
Kuna dhuluma na mambo maovu ungeweza kuwafanyia binadamu wenzako kama usingekuwa na Dini yako?
Dini gani iliruhusu utumwa?Huhitaji dini ili uwe mtu mwema, bali huruma
Ukikosa huruma, hata ukiwa na dini utafanya mabaya kwa wengine Kwa kutumia uhalalisho wa dini yako
Kama dini imehalalisha utumwa nawewe morality yako inaishi kwa misingi ya dini utajikuta unashindwa hata kumkosoa king leoplod wa ii aliyeua watumwa wake zaidi ya milion 10 kwa kutumia kitabu cha dini
Shukrani mkuuNaam, naam.
Nimejitahidi sana kusoma dini.Binafsi nyumbani kwa mzee wangu alipotokea ni kanisani. Kwa kuwa baba yake alikuwa mchungaji.
Kwa hivyo, yeye alikuwa si tu anaenda kanisani, bali aliishi kanisani.
Nimejitahidi kusoma Ukristo, Uislamu, Uyahudi, Uhindu, Ubuddha, na dini nyingine nyingi.
Dini kwa upande mmoja, ni kitu kizuri sana. Inarudisha watu kwenye mstari wa kuishi kwa upendo, kukataza mabaya, kuhimiza mema na kumtofautisha mtu na hayawani.
Upande huu wa dini naupenda sana.
Ila, pia, dini ina updane mwingine, mbaya. Wa kubaguana, kuona watu wa dini yako ndio wenye ukweli na wengine wapotofu, kuhalalisha mambo mabaya kwa kigezo cha dini, vita vya kidini, dini kutumika kama siasa, dini kutumika ku manipulate watu kwa uongo, dini kupinga maendeleo ya elimu na kudumaza fikra za watu kwa ujinga, na mambo kem kem kama hayo.
Kiukweli, dini ni nyenzo, kama moto.
Moto si mzuri wala mbaya. Moto upo tu.
Jinsi gani unautumia moto ndiyo inaweza kuwa nzuri au mbaya.
Unaweza kuutumi moto kupika chakula watu wakala wakashiba. Hapo moto umetumika vizuri.
Moto huo huo, unaweza kuutumia, ukaunguza nyumba, ukaua watu. Hapo moto umeutumia vibaya.
Vivyo hivyo kwenye dini.
Unaweza kutumia dini ukawaunganisha watu, ukapunguza uhalifu katika jamii. Hapo umeitumia dini vizuri.
Unaweza pia kutumia dini kuwagawanya watu, ukaanzisha vita ya kidini, watu wakauana kwa mamilioni. Hapo umeitumia dini vibaya.
Dini kama dini haina maana. Si mbaya wala nzuri. Maana ya dini unaipa wewe muumini.
Moto kama moto si mbaya au mzuri. Ubaya au uzuri wa moto unakuja kulingana na mtumiaji anavyoutumia.
Hakuna Dini imehalalisha utumwaHuhitaji dini ili uwe mtu mwema, bali huruma
Ukikosa huruma, hata ukiwa na dini utafanya mabaya kwa wengine Kwa kutumia uhalalisho wa dini yako
Kama dini imehalalisha utumwa nawewe morality yako inaishi kwa misingi ya dini utajikuta unashindwa hata kumkosoa king leoplod wa ii aliyeua watumwa wake zaidi ya milion 10 kwa kutumia kitabu cha dini
Hivi unapo sema umeusoma Uislamu umeusoma Uislamu gani? Maana naona huujui kabisa.Nimejitahidi kusoma Ukristo, Uislamu, Uyahudi, Uhindu, Ubuddha, na dini nyingine nyingi.