Mchango wa Dini katika ustawi wa maisha ya Binadamu

Mchango wa Dini katika ustawi wa maisha ya Binadamu

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
57,386
Reaction score
90,789
Dini ina mchango gani katika kuwatendea binadamu wenzako haki, kuwathamini na kuboresha maisha yao?

Dini yako inakuongoza au unaipa kipaumbele katika kuratibu matendo yako na binadamu wengine wanaokuzunguka?

Kuna dhuluma na mambo maovu ungeweza kuwafanyia binadamu wenzako kama usingekuwa na Dini yako?
 
Kama sio Dini mie nilikuwa Mtu mbaya sana.
Ila tangu nilipoanza kusali,
Mambo yangu mengi yalibadilika.
Nikaanza kuheshimika, kupenda watu, kuona shida za wenzangu kuwa ni zangu.

Kwa ufupi dini zina msaada mkubwa sana kwa mwanadamu kumtafuta MUNGU.
 
Kama sio Dini mie nilikuwa Mtu mbaya sana.
Ila tangu nilipoanza kusali ,
Mambo yangu Mengi yalibadilika.
Nikaanza kuheshimika, kupenda watu, kuona shida za wenzangu kuwa ni zangu.

Kwa ufupi dini zina msaada mkubwa sana kwa mwanadamu kumtafuta MUNGU
Wewe sio mbaguzi wa dini za wengine?
 
Dini ina mchango gani katika kuwatendea binadamu wenzako haki, kuwathamini na kuboresha maisha yao?

Dini yako inakuongoza au unaipa kipaumbele katika kuratibu matendo yako na binadamu wengine wanaokuzunguka?..
Sali Sana brother, nina uhakika uhuni na maisha niliyoyaishi, hata nusu hutafika ila ni Mwenyezi Mungu anayejua, sali sana nasema tena sali sana.

Safari ya Kristo kuikomboa dunia sio historia na ni mwendelezo, nashukuru Kristo alitufikia, ingawa waliotuletea habari njema walikuwepo wazuri na wabaya pia(agents of colinialism).Ila tunashukuru, sali sana na ukamuegemee Kristo Mfalme wa wafalme.
 
Sali Sana brother, ni nauhaukika uhuni na maisha niliyoyaishi,hata nusu hutafika,ila ni Mwenyezi Mungu anayejua,sali Sana nasema tena sali Sana...safari ya Kristo kuiomboa dunia siyo historia,na ni mwemdelezo, Nashukuru Kristo alitufikia,ingawa waliotuletea habari njema walikuwepo wazuri na wabaya pia(agents of colinialism).Ila tunashukuru ,Sali Sana na ukamuegemee Kristo Mfalme wa wafalme.
Dini imeleta mazuri na mabaya ila kimizania mazuri ni mengi zaidi.

Hizi Dini zimesaidia watu wajue kuna nguvu kuu iliyo juu yao (Mungu/mwenye enzi/God/Mulungu) na mwishowe kila mtu atawajibika kutoa majibu kwa yale aliyofanya hapa duniani.

Imani hii ndo muhimili wa Amani tuliyonayo duniani leo hii. Vinginevo dunia ingekuwa sehemu hatari sana.
 
Kama hauna misingi ya Dini inayokuongoza. Utafanya .mambo ya ajabu Sana..hata Mimi niliyofanya najutia sana sana sana.. lakini namshukuru Mungu kwa kuniongoza nimeiona Nuru.

Japokua na dhambi zangu nyingi mfano wa bahari ya Hindi..bado Mungu amenivusha katika majaribu makubwa Sana..

Na kwa Imani yangu nitavuka na hapa nilipo.
 
japo sina hakika ila Dini ni msingi ya matendo ya mtu kuwa na hofu ama woga!!
 
Kama hauna misingi ya Dini inayokuongoza. Utafanya .mambo ya Ajabu Sana..hata Mimi niliyofanya najutia Sana Sana Sana.. lakini namshukuru Mungu kwa kuniongoza nimeiona Nuru.

Japokua na dhambi zangu nyingi mfano wa bahari ya Hindi..bado Mungu amenivusha katika majaribu makubwa Sana..

Na kwaimani yangu ntavuka na hapa nilipo.
hata username lako limesadifu yaliyomo!!
 
Huhitaji dini ili uwe mtu mwema, bali huruma

Ukikosa huruma, hata ukiwa na dini utafanya mabaya kwa wengine Kwa kutumia uhalalisho wa dini yako

Kama dini imehalalisha utumwa nawewe morality yako inaishi kwa misingi ya dini utajikuta unashindwa hata kumkosoa king leoplod wa ii aliyeua watumwa wake zaidi ya milion 10 kwa kutumia kitabu cha dini
 
Mjomba Kiranga tupe mawili matatu hapa
Naam, naam.

Nimejitahidi sana kusoma dini. Binafsi nyumbani kwa mzee wangu alipotokea ni kanisani. Kwa kuwa baba yake alikuwa mchungaji.
Kwa hivyo, yeye alikuwa si tu anaenda kanisani, bali aliishi kanisani.

Nimejitahidi kusoma Ukristo, Uislamu, Uyahudi, Uhindu, Ubuddha, na dini nyingine nyingi.

Dini kwa upande mmoja, ni kitu kizuri sana. Inarudisha watu kwenye mstari wa kuishi kwa upendo, kukataza mabaya, kuhimiza mema na kumtofautisha mtu na hayawani.

Upande huu wa dini naupenda sana.

Ila, pia, dini ina upande mwingine, mbaya. Wa kubaguana, kuona watu wa dini yako ndio wenye ukweli na wengine wapotofu, kuhalalisha mambo mabaya kwa kigezo cha dini, vita vya kidini, dini kutumika kama siasa, dini kutumika ku manipulate watu kwa uongo, dini kupinga maendeleo ya elimu na kudumaza fikra za watu kwa ujinga, na mambo kem kem kama hayo.

Kiukweli, dini ni nyenzo, kama moto.

Moto si mzuri wala mbaya. Moto upo tu.

Jinsi gani unautumia moto ndiyo inaweza kuwa nzuri au mbaya.

Unaweza kuutumi moto kupika chakula watu wakala wakashiba. Hapo moto umetumika vizuri.

Moto huo huo, unaweza kuutumia, ukaunguza nyumba, ukaua watu. Hapo moto umeutumia vibaya.

Vivyo hivyo kwenye dini.

Unaweza kutumia dini ukawaunganisha watu, ukapunguza uhalifu katika jamii. Hapo umeitumia dini vizuri.

Unaweza pia kutumia dini kuwagawanya watu, ukaanzisha vita ya kidini, watu wakauana kwa mamilioni. Hapo umeitumia dini vibaya.

Dini kama dini haina maana. Si mbaya wala nzuri. Maana ya dini unaipa wewe muumini.

Moto kama moto si mbaya au mzuri. Ubaya au uzuri wa moto unakuja kulingana na mtumiaji anavyoutumia.
 
Dini ina mchango gani katika kuwatendea binadamu wenzako haki, kuwathamini na kuboresha maisha yao?

Dini yako inakuongoza au unaipa kipaumbele katika kuratibu matendo yako na binadamu wengine wanaokuzunguka?

Kuna dhuluma na mambo maovu ungeweza kuwafanyia binadamu wenzako kama usingekuwa na Dini yako?
Kama si dini hii dunia pangekuwa ni uwanja wa vita
 
Huhitaji dini ili uwe mtu mwema, bali huruma

Ukikosa huruma, hata ukiwa na dini utafanya mabaya kwa wengine Kwa kutumia uhalalisho wa dini yako

Kama dini imehalalisha utumwa nawewe morality yako inaishi kwa misingi ya dini utajikuta unashindwa hata kumkosoa king leoplod wa ii aliyeua watumwa wake zaidi ya milion 10 kwa kutumia kitabu cha dini
Dini gani iliruhusu utumwa?
 
Naam, naam.

Nimejitahidi sana kusoma dini.Binafsi nyumbani kwa mzee wangu alipotokea ni kanisani. Kwa kuwa baba yake alikuwa mchungaji.
Kwa hivyo, yeye alikuwa si tu anaenda kanisani, bali aliishi kanisani.

Nimejitahidi kusoma Ukristo, Uislamu, Uyahudi, Uhindu, Ubuddha, na dini nyingine nyingi.

Dini kwa upande mmoja, ni kitu kizuri sana. Inarudisha watu kwenye mstari wa kuishi kwa upendo, kukataza mabaya, kuhimiza mema na kumtofautisha mtu na hayawani.

Upande huu wa dini naupenda sana.

Ila, pia, dini ina updane mwingine, mbaya. Wa kubaguana, kuona watu wa dini yako ndio wenye ukweli na wengine wapotofu, kuhalalisha mambo mabaya kwa kigezo cha dini, vita vya kidini, dini kutumika kama siasa, dini kutumika ku manipulate watu kwa uongo, dini kupinga maendeleo ya elimu na kudumaza fikra za watu kwa ujinga, na mambo kem kem kama hayo.

Kiukweli, dini ni nyenzo, kama moto.

Moto si mzuri wala mbaya. Moto upo tu.

Jinsi gani unautumia moto ndiyo inaweza kuwa nzuri au mbaya.

Unaweza kuutumi moto kupika chakula watu wakala wakashiba. Hapo moto umetumika vizuri.

Moto huo huo, unaweza kuutumia, ukaunguza nyumba, ukaua watu. Hapo moto umeutumia vibaya.

Vivyo hivyo kwenye dini.

Unaweza kutumia dini ukawaunganisha watu, ukapunguza uhalifu katika jamii. Hapo umeitumia dini vizuri.

Unaweza pia kutumia dini kuwagawanya watu, ukaanzisha vita ya kidini, watu wakauana kwa mamilioni. Hapo umeitumia dini vibaya.

Dini kama dini haina maana. Si mbaya wala nzuri. Maana ya dini unaipa wewe muumini.

Moto kama moto si mbaya au mzuri. Ubaya au uzuri wa moto unakuja kulingana na mtumiaji anavyoutumia.
Shukrani mkuu
Upo deep Sana kwenye upambanuzi wa mada tofauti tofauti
Binafsi nakukubali sana Jf,najiulizaga huu uwezo sijui uliupatia wapi!
 
Huhitaji dini ili uwe mtu mwema, bali huruma

Ukikosa huruma, hata ukiwa na dini utafanya mabaya kwa wengine Kwa kutumia uhalalisho wa dini yako

Kama dini imehalalisha utumwa nawewe morality yako inaishi kwa misingi ya dini utajikuta unashindwa hata kumkosoa king leoplod wa ii aliyeua watumwa wake zaidi ya milion 10 kwa kutumia kitabu cha dini
Hakuna Dini imehalalisha utumwa
 
Nimejitahidi kusoma Ukristo, Uislamu, Uyahudi, Uhindu, Ubuddha, na dini nyingine nyingi.
Hivi unapo sema umeusoma Uislamu umeusoma Uislamu gani? Maana naona huujui kabisa.

Nacho kushauri usiwe muongo.
 
Back
Top Bottom