Mchange: Sisi tunajua Lissu alifanya makosa, ndio maana familia ya Lissu iko tayari kufanya maridhiano

Mchange: Sisi tunajua Lissu alifanya makosa, ndio maana familia ya Lissu iko tayari kufanya maridhiano

"Sisi tunajua Lissu alifanya Makosa ndio maana Familia ya Lissu iko tayari kwa maridhiano lakini Heche anafanya kila namna kuzuia maridhiano hayo" Habibu Mchange

Maridhiano yanahusika nini na kesi ya uhaini? Heche ana mamlaka gani ya kumbakiza Lissu mahabusu? Kuna ajabu gani "ndugu" yake Lissu kumtaka atoke mahabusu? Mimi sitashangaa kama tukiambiwa kuwa ni dada wa kutafuta kama wale wakatoliki.

Huyu anakuwa kama Musiba. Shutuma nyingi bila substance. Anajaribu kuigawa Chadema lakini hatafanikiwa.

Amandla....
 
Du! kina Mchange ndo wenye kujua walio na makosa kuliko mahakama, ni lini na ni wapi familia ya Lissu imetaka maridhiano? Heche ana mamlaka gani juu ya familia na Lissu mwenyewe? Mchange asidhani watanzania ni watoto wake wakuwadanganya.
 
"Sisi tunajua Lissu alifanya Makosa ndio maana Familia ya Lissu iko tayari kwa maridhiano lakini Heche anafanya kila namna kuzuia maridhiano hayo" Habibu Mchange

Sisi waislam tunatakiwa muda mwingi kuutumia ktk kuwakumbusha watu ktk kheri na kuacha mabaya. Hilo ndio lengo la mwanadam kuja hapa duniani. Unaweza ukajikuta 99% ya maisha yako ya hapa duniani umetumia ktk kueneza propaganda
 
Alikua Chadema na aligombea ubunge pale Kibaha mjini 2010. Alihamia CCM akiwa na kina Juliana Shonza na Mtela Mwampamba.
Kweli kabisa, na hawa ndio masnitch wa mwanzo mwanzo ndani ya cdm. Ametumika sana na Mwigulu kuihujumu cdm yeye na wenzake, akiwemo Zito Kabwe. Hata sasa huwa anatumika kuishambulia cdm. Nahisi huyu ni mmoja wa mashahidi wa uongo kwenye kesi ya Lisu wanaofichwa.

Kama anajua Lisu amefanya makosa si akatoe ushahidi atiwe hatiani? Wameona hawana ushahidi wa kumfunga, sasa wanalazimisha maridhiano ili watoke kwenye aibu. Kama kuna mahali Lisu alicheza heko ni kujitetea mwenyewe, vinginevyo Lisu angeenda ikulu kwenye maridhiano kwa lazima.
 
Sisi waislam tunatakiwa muda mwingi kuutumia ktk kuwakumbusha watu ktk kheri na kuacha mabaya. Hilo ndio lengo la mwanadam kuja hapa duniani. Unaweza ukajikuta 99% ya maisha yako ya hapa duniani umetumia ktk kueneza propaganda
Hakuna dini imejaa wanafiki kama hiyo yenu. Sijutii kuachana na uisilamu. Kibaya zaidi wanaoongoza kwa unafiki ni wale wanaojifanya kujua hiyo dini. Mkianza kuongea jambo na kuweka kiirabu kisha kukisema kwa kiswahili mnajifanya watu rahimu kumbe upuuzi mtupu.
 
Baada ya kusoma majina hayo, nimekaa dakika tano nzima nkijaribu kuwaza niandike nini juu ya watu/viongozi wa aina hii.
Nimeshindwa kabisa kupata maneno sahihi sahihi.

Nashindwa kabisa kujuwa kwa nini CHADEMA ilikuwa kama kiwanda cha kuzalisha watu wa aina hii?
Na bado hujawaweka akina Yericko na wengine wengi wa aina hiyo.

Na bado sina njia nzuri ya kuwazungumzia waTanzania wenzetu hawa kwa sasa.

Na huko ndani ya CCM je? Hali itakuwa vipi endapo polisi wakiwatelekeza na kupoteza madaraka?
Ni wangapi watakimbilia CHADEMA au chama kingine kikishika madaraka hayo?

Hivi ni halali kusema watu wote hawa ni wasaka fursa tu, au kuna sababu nyinginezo zinazosababisha watu kuwa malaya kiasi hiki?

Binafsi naanza kujenga nadharia kwamba ubovu huu una misingi yake; hasa ndani ya vyama vya siasa vyenyewe.

CCM imewalazimisha waTanzania kuwa malaya.!
Chadema ya makengeza ilikua uozo mtupu
 
Lissu na Heche nao wameoza? Maana sio tu walikuwa sehemu ya Chadema ya Mbowe, walikuwa viongozi wakubwa wa chama hicho.

Amandla...
 
"Sisi tunajua Lissu alifanya Makosa ndio maana Familia ya Lissu iko tayari kwa maridhiano lakini Heche anafanya kila namna kuzuia maridhiano hayo" Habibu Mchange

Huyu jamaa hana akili nzuri na ni mpumbavu. Anatengeneza propaganda za kijinga kabisa.

Kama serikali inataka kufanya maridhiano na Lissu kwani ni lazima wapitie kwa Heche...!?
 
"Sisi tunajua Lissu alifanya Makosa ndio maana Familia ya Lissu iko tayari kwa maridhiano lakini Heche anafanya kila namna kuzuia maridhiano hayo" Habibu Mchange

Maridhiano ndiyo upuuzi gani? Kama kweli mnaamini yuko ndani kwa kosa la uhaini kwanini kesi isihukumiwe kimahaka? Kama mnataka maridhiano it proves that yuko ndani kwa sababu za kisiasa na si sababu ya kosa la uhaini.
 
Hakuna dini imejaa wanafiki kama hiyo yenu. Sijutii kuachana na uisilamu. Kibaya zaidi wanaoongoza kwa unafiki ni wale wanaojifanya kujua hiyo dini. Mkianza kuongea jambo na kuweka kiirabu kisha kukisema kwa kiswahili mnajifanya watu rahimu kumbe upuuzi mtupu.
Unafiki katika Uislamu umepigwa vita sana.

Surah An-Nisa (4:145):
"Hakika munafi watakuwa kwenye kiwango cha chini zaidi katika Moto, wala hawataweza kuokolewa."
(Maana: Munafi hawataingia Peponi, bali adhabu yao ni moto.)

Hadithi za Mtume Muhammad ﷺ zinathibitisha hili:
"Hakika moja ya alama za munafi ni: akapewa amani, anakupigia uso lakini moyo wake umelaghai."
(Sahih Bukhari & Sahih Muslim)
 
Back
Top Bottom