Mchanganuo wa bolt na Gari ya Aqua

Mchanganuo wa bolt na Gari ya Aqua

Clack-Sniper

Member
Joined
May 16, 2025
Posts
39
Reaction score
74
Habari wataalamu wa Magari humu ndani.
Hivi karibuni nimetaka kufanya utafiti wa kutumia gari ya Toyota aqua Hybrid kwa ajili ya Bolt, Nafanya part time tu.
kwa siku kama 10 nimepata mapato kama hayo hapa sijaweka gharama za service. Mwenye uzoefu wa kutumia gari ya Gesi na mafuta, kama unaweza kusaidia uzoefu wako.

Je hizi faida hapa ni nzuri au bado hazitoshi kuna kubwa zaidi?
1768627139385.png

Changamoto za hii Gari, Iko chini so kwenye matuta some how inaburuzika, ila nimeongeza tairi kubwa, some how imepunguza.
 
Unajua gari yako, angalia thamani yake, recovery, service, mda wako na unabakiwa na kiasi gani!

Wewe mwenye ndo unaweza jua faida kuliko mtu yeyote
 
Habari wataalamu wa Magari humu ndani.
Hivi karibuni nimetaka kufanya utafiti wa kutumia gari ya Toyota aqua Hybrid kwa ajili ya Bolt, Nafanya part time tu.
kwa siku kama 10 nimepata mapato kama hayo hapa sijaweka gharama za service. Mwenye uzoefu wa kutumia gari ya Gesi na mafuta, kama unaweza kusaidia uzoefu wako.

Je hizi faida hapa ni nzuri au bado hazitoshi kuna kubwa zaidi?
View attachment 3530944

Changamoto za hii Gari, Iko chini so kwenye matuta some how inaburuzika, ila nimeongeza tairi kubwa, some how imepunguza.
Hayo mafuta ya 92,000 yanakupa mileage ya kilometa ngapi toka kujaza hiyo full tank mpaka kuisha.
 
Inategemea. Safari za mjini na foleni unaweza pata 600km.

Ila safari nje ya mji inaweza kuwa kubwa
 
Kwa hiyo wanaposema ktk datasheet yake kwamba inaenda 800 KM kwa mjazo mmoja wa full tank ni uongo.
 
Zile ni hesabu za makadirio
Na mara nyingi huwa wanatumia hayo makadirio kwenye gari ambayo ni mpya kabisa ( Brand new )
NA ni latest years .

Hizi nyingine ni ngumu haziwezi kufikia hapo Lazima pawepo na utofauti fulani
 
Kwa hiyo wanaposema ktk datasheet yake kwamba inaenda 800 KM kwa mjazo mmoja wa full tank ni uongo.
Siyo kwa foleni za Dar. Ila ukiwa unaenda safari ambazo hazina foleni hiyo 800km inafika
 
Kwa hiyo wanaposema ktk datasheet yake kwamba inaenda 800 KM kwa mjazo mmoja wa full tank ni uongo.
Inaenda zaidi ya hapo. Maana full tank 1 aqua inatoka Dar mpaka Nakonde. Na ikiwa na abiria.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom