Mchana wa kutisha

Judithkaunda

Member
Aug 21, 2022
90
228
Mwaka jana nikiwa naishi mtaa fulani nilishuhudia tukio la ajabu ambalo halikusisimua tu mwili wangu bali ulipata ganzi kwa dakika nikashindwa kuamua nini chakufanya.

Naitwa Judith nimeolewa na nimejaliwa watoto wawili wa kiume. Ndani ya geti la nyumba niliyoishi kulikuwa na eneo la wazi siku hiyo wapangaji wenzangu hawakuepo, nilikuwa ndani nafanya shughuli zangu kwa amani tele kwa sababu watoto wangu walikuwa nje wanacheza na nilikuwa nawasikia.

Baada ya kumaliza kazi yangu ndani nikatoka nje huku najinyoosha
Lahaula! Nilichokiona sio kwamba niliogopa tu lakini sikuamini macho yangu.

Kulikuwa na pikipiki iliyopakiwa pale nje na watoto wangu walipenda kuchezea wanakaa na kufanya kama wako safarini, sasa wakati natoka hawakuwa peke yao alikuwepo na mtoto wa jirani yangu mtaa wa pili uwepo wake haukunishtua mara kadhaa huwa anakuja kucheza nao, lakini tukio lililokuwa linaendelea ndio liliniacha kwenye mataa nisijue kitu sahihi cha kufanya lakini baada ya sekunde kadhaa nikaamua kujikoholesha ili mladi watambue nipo ili ule mchezo uishie hapo.

Mtoto wangu mkubwa wa miaka mitano alikuwa juu ya tenki la maji ni kawaida yake licha ya kumkanya mara kadhaa, hakuwahi kuacha kucheza pale. Alikuwa bize hajui hata kinachoendelea, shida ni kwa huyu mwenye miaka mitatu, mtoto wangu mdogo maskini alikuwa juu ya pikipiki akicheza kama dereva kwa mbwembwe nyingi na kutoa sauti kama mlio wa pikipiki.

Akiwa hana habari kabisa nyuma yake yule mtoto wa jirani alikuwa kapanda kama abiria lakini abiria huyu alikuwa na lake jambo. Jambo lililoniacha katika mshangao mkubwa. Mtoto yule alikuwa nusu uchi, maungio yake ya kiume yanatazamana na mgongo wa mtoto wangu.

Niliganda kwa sekunde kadhaa!
Wakati yeye akijikoki nyuma ya mwanangu, yeye mtoto yule wa miaka mitatu hakujua linaloendelea. Aliendelea kuendesha pikipiki yake huku anapiga makelele.

Sio siri niliogopa sana sijui hata nisimulie vipi hali niliyokuwa nayo kwa sekunde kadhaa niliganda na kulazimisha macho yangu yaangalie kwa makini huenda nilichokiona ni tofauti.

Na baada ya kujiridhisha ni kweli nikakohoa ili ashtuke na kuhailisha mashambulizi yake, nilifanikiwa aliacha na kujifanya kama hakuna kilichokuwa kinaendelea.

Tumbo la uzazi halikuishia kunicheza peke ake bali vyote vilivyokuwa tumboni vilitikisika kwa nguvu, niliishiwa nguvu na kama kuna mtu mzima angekuwepo karibu yangu ningeuruhusu mwili wangu uzimie kwa muda alafu nikishtuka niwe nimepoteza kumbukumbu za tukio lile iwe kama halikuwahi kutokea, lakini nilijizuia kwasababu nilihisi labda angefika mbali zaidi.

Na mimi sikumuonyesha kama nimeona chochote, nilichofanya nikatoka nje nikatafuta fimbo matata sana, ingawa haikuwa tabia yangu kuadhibu watoto wa watu lakini woga na hasira viliujaza moyo wangu nikaamua kufanya maamuzi.

Nikamuita kistarabu kabisa kama nataka kumtuma na sikuruhusu aone fimbo niliyoandaa nadhani angetafuta pakutokea kitambo sana na kuniachia vumbi.

Alisogea karibu yangu nilikuwa natetemeka midomo nashindwa hata nianzie wapi kumuhoji. Nilimtazama kwa dakika kadhaa nikimtafakari hakuwa mjinga tayari aligundua kuna tatizo nae hakuwa na amani kabisa.

Niliyatafakari mazingira anayoishi yule kijana mdogo mwenye umri kati ya miaka tisa hadi kumi na moja , aliishi na bibi na mama yake ambao walikuwa bize na vibarua huko mjini, waliondoka asubuhi na kurudi usiku, kwa maana hiyo huyu mtoto anajilea mwenyewe ni kama mtoto wa mtaani anazunguka kila mahali atakavyo na kujichanganya na makundi tofauti tofauti, hana uangaliazi wowote wa mzazi na anaenda shuleni atakavyo.

Baada ya kumtafakari hasira zikapungua sikuwa na nguvu za kumchapa tena nilimuonya ili ajue alichokuwa anafanya ni kosa kubwa sana.

Sikuishia hapo nikamtafuta bibi yake, sikutaka kumwambia mama yake namjua ni mkorofi ingekuwa ngumu kunielewa, nilifanikiwa kuongea na bibi yake na kitu cha kwanza nilitaka kujua kama anaifahamu hiyo michezo ya mjukuu wake. Yule bibi alinichanganya kwa sababu hakuonyesha kushtushwa hata kidogo na swali langu, lakini sikusita kumshauri namna yakumuonya mtoto kwa kumwambia ukweli wa athari, madhara na matokeo ya vitendo hivyo na kumfatilia kwa karibu mjukuu wake.

Sijui kama alifanya vyote nilivyomwambia lakini alinifurahisha baada ya kumleta ndugu yao mwingine atakaeshinda pale nyumbani ili amdhibiti huyo mtoto anapotoka shule asishinde mtaani.

Ule mtaa nilishahama lakini huwa namkumbuka yule mtoto kwa sababu namba ya bibi yake ninayo basi huwa ninamtumia ujumbe wa tahadhari asiache kumfatilia mtoto maana si rahisi huyo mtoto kuacha.

Hofu yangu kama mtoto yule akikutana na wababe zaidi yake wakaamua kumgeuza yeye sasa akawa kitoweo cha wahuni, nitajisikia vibaya akiwa kama wale wa mtandaoni tunaodai kuwapoteza kutoka katika kundi la wanaume.

Hili ni tukio la kweli kabisa unaweza kudhani ni tukio la kawaida lakini lina maana kubwa sana. Namshukuru Mungu kwa kunionyesha tukio lile ni kama aligonga kengele ya tahadhali kichwani kwangu imesaidia sana tangu hapo nimekuwa makini sana na mienendo ya watoto wangu.

Ingawa watoto wangu bado ni wadogo lakini nawaambia mara kwa mara wasiruhusu mtu yoyote kushika sehemu zao za siri na sehemu ya haja kubwa na yeyote atakae wagusa wanishtakie. Kama mama bado sina amani wakiwa mbali na uwepo wa macho yangu lakini kinachonitia moyo kila wakitoka shule au sehemu nyingine watanihadithia kila kitu wanachokumbuka wamefanya na mimi najitahidi kuwasikiliza.

Mwenyezi mungu atutie nguvu wazazi wenye watoto wa kiume. Matukio ya ulawiti yanayoripotiwa siku hizi unaweza ukakaa chini ukalia ila haisaidii kitu hata kama hauna wa kiume ombea hiki kizazi hao ndo waume wa watoto wako wa kike baadae.

Niambie mwenzangu ni mbinu gani unatumia kuwafundisha wanao kuepukana na vitendo hivyo? karibu tupeane darasa kwa ajili ya watoto wetu.
SEMA KWA AJILI YA WASIOWEZA KUSEMA!
KARIBU!
 
Ulawiti umeongezeka sana, wazazi tuko busy sana na maisha kiasi kwamba watoto tunakutana nao usiku mwingi,au wengine wako boarding kinachoendelea huko Mungu pekee ndio anajua..

Kimsingi hali ni mbaya sana, binafsi huwa nakaa nao na kuwaambia ukweli..ni kuvunja tu ukimya..usiwaonee aibu kusema nao.
 
Kweli kabisa
 
Wanawake ni wanafiki sana mi mwanamke akishaandika tu neno tumbo la uzazi na mu underestimate wanajifanya wana huruma ila unyama wanaowafanyia watoto wa mama wengine walio zaa na wanaume wengine wanaoishi pamoja kwenye ndoa mungu ndo anajua hukumu yao ila ukiwaona mitandaoni wanajifanya sijui tumbo la uzazi kumbe hakuna katili kama mwanamke kwenye uso wa dunia hata shetani kuna mda anachukua kozi kutoka kwao.
 
Wanawake ni wanafiki sana mi mwanamke akishaandika tu neno tumbo la uzazi na mu underestimate wanajifanya wana huruma ila unyama wanaowafanyia watoto wa mama wengine walio zaa na wanaume wengine wanaoishi pamoja kwenye ndoa mungu ndo anajua hukumu yao ila ukiwaona mitandaoni wanajifanya sijui tumbo la uzazi kumbe hakuna katili kama mwanamke kwenye uso wa dunia hata shetani kuna mda anachukua kozi kutoka
 
Sikulaumu kaka angu huwez elewa kabsa tunachopitia leba.
Alafu nenda kachunguze mwanamke yoyote anaemtesa mtoto wa mwenzie utagundua kwamba hata yeye anapitia wakat mgumu, Kuna vitu mnasababisha nyinyi wanaume unakuta mwanaume anamnyanyasa mke wake na hata tumiz ni shida alafu unamtegemea huyo akulelee mwanao vizuri hv huo upendo anautoa wapi? Kulea mtt wa mtu ni kaz sana na wapo tunaoweza licha ya matatzo tunayopitia.
 
Umeandika upuuzi,kwa jini hukumchapa huyo dogo na kumpiga marufuku kukanyagw hapo nyumbani,kwa nini hukumuelewesha mwanao kuhusu huyo kijana,we ni popoma

Hayo ni maoni yako lakn huu upuuzi Kuna wengine wanajifunza alafu siwez kuandika Kila kitu nilichowambia Watoto wangu.
 
Back
Top Bottom