mchana mwema

Menu ni ya kiti moto tu. mwenye picha aweke tu-contrast
 
Kumbikumbi wanakuwepo ikiwashwa taa ya tubelight,ukiwa msimu wa mvua...wanakaangwa hao na kuliwa kama bisi!!

hahah kwa jibu hili utamfanya mwenzako hata wale nondo awaite kumbikumbi...
 
wanaliwa sana tu watu8 ndo mlo wako anaopendelea huo haswa akichat hapa JF!!Wamejaa protein!!

Hahaha kumbikumbi wanakinai sana hivyo huwezi wala mara kwa mara....btw huku nilipo hawapo hao wadudu....
 
Hahahahaha eti kweli watu8? Wana taste gani?

Mmmh!! sina ladha ya kukufananishia lakini ladha yake ni nzuri tu maadam wawe wamekaushwa kwa uzuri.

Kuna wakati nilikuwa naishi vijijini mwa Tanzania na msimu wa kumbikumbi ukiwadia ilikuwa ni ahueni kwetu.

Ukiwakamata wengi na kuwakausha katika moto huwa wanakaa muda mrefu sana pasipo kuharibika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…