Mchaga apelekwa Moshi na fisi

Mchaga apelekwa Moshi na fisi

salito

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2011
Posts
1,406
Reaction score
734
wadau wazima?

Leo bwana nimekaa mtaan kwangu na jamaa zangu wa mtaani ndio wakaanza kunipa habari hii ambayo siwezi kuthibitisha ukweli wake ila nimeona nishee na nyie wakuu.

Ni hivi kuna babu mmoja hapa mtaani kwetu huwa anapika chips na mishkaki,sasa inasemekana takriban miezi miwili imepita babu huyu ametoweka na yupo kwao Moshi,ambapo siku ya tukio babu alitoka hapa eneo lake la biashara na kwenda Buguruni kununua viazi kwa ajili ya chips,akapanda daladala ambayo ilimshusha Buguruni Rozana,cha ajabu babu akawa halioni soko la Buguruni akazunguka sana kulitafuta mwisho wa yote akaamua kumsimamisha binti na kumuuliza lilipo soko ambapo binti alimshangaa lakini akaamua kumuonyesha babu soko lilipo tena kwa kidole tu,lakini babu kila alikuwa akiangalia haoni soko anaona nyumba tupu za watu,mwisho yule binti akaamua kumpeleka babu mpaka sokoni maana ni hapo hapo walipokuwepo.


Kufikishwa sokoni babu anaambiwa "haya babu sokoni ndio hapa" lakini babu akawa haoni chochote yeye akaona amepelekwa kwenye nyumba ya mtu,akabishana sana na yule dada mwisho dada wa watu akamuona babu tapeli labda akaamua kuondoka.

Hapo ndio kasheshe ilipoanza,

Babu akapoteza fahamu akawa haelewi hata kilichomtokea na alikaa katika hali hiyo kwa muda usiofahamika,lakini alipopata fahamu akajishangaa kujikuta yupo kwenye gari la mkoa,alipomuuliza abiria mwenzake tunaenda wapi,abiria akamwambia Arusha mzee,alipotaka kumuuliza hili ni basi gani akapitiwa na usingizi mzito sana,alipokuja kuamka akajikuta yupo katikati ya pori ambalo halieleweki ni pori gani,ila babu alianza kusikia harufu ya ubwabwa na mara akaanza kusikia sauti ya mziki mkubwa sana,alipotaka kukimbia miguu yote ikaisha nguvu na mara akaanza kusikia sauti za vicheko,zilipotulia sauti hizo ndio akasikia sauti ikimwambia "wewe si unajifanya mjanja hutaki kurudi kwenu??sasa unataka utaenda au hutaki utaenda tu",babu akapoteza fahamu tena.

Alipozinduka akajikuta yupo juu ya fisi,na fisi anatembea taratibu sana kwenye shamba la nyumbani kwao huko Moshi,mara fisi akafika kwenye uwanja wa nyumba yao na kusimama ambapo walitoka ndani ndugu zake na watoto wa kaka yake na wa kwake na kuanza kumuangalia kwa kutoamini,ndipo fisi alipomtua babu chini kwa kuanza kukaa chini taratibu huku akirudi kinyume nyume mpaka babu alipomaliza kumshusha babu,kisha fisi akaanza kurudi kinyume nyume na mwisho akayeyuka.

Stori iliiyopo nyuma ya pazia ni kwamba babu amekaa zaidi ya miaka 10 bila kwenda kwao na aliacha mke na watoto,na kwao walikufa ndugu zake wengi ambapo kila walipokuwa wanamtafuta babu hakuwa tayari kwenda kwao kuhudhuria mazishi,mpaka mama yake mzazi alikufa lakini hakwenda,kaka yake alimtumia ujumbe mpaka akachoka na ndio mwisho akamwambia amemchoka kumvumilia na ndipo siku hiyo alipokuwa analetwa na fisi,huyu kaka yake aliwaambia ndugu zake waliokuwa ndani tokeni mkampokee mgeni wetu,na walipotoka ndio wakamkuta babu juu ya fisi.

Wakuu stori hii ni babu mwenyewe ndio alipiga simu kwa kijana aliekuwa anasaidiana nae kupika chips na ndio akampa mkasa huu wote.

Dunia inamambo wakuu..samahani kwa uandishi mbaya maana natumia simu,naomba mvumilie tu.
 
mmmh, kama Riwaya vile .... ngoja tupate ushuhuda kutoka Rukwa, tanga na Ruvuma wazee wa kusafirisha ....
 
Hujasema kwa sasa babu huyo yuko wapi? Moshi au yu njiani kurudi kijiweni kwake? Akirudi mwambie aje atoe ushuhuda hapa jf!!!!!!!
 
Hujasema kwa sasa babu huyo yuko wapi? Moshi au yu njiani kurudi kijiweni kwake? Akirudi mwambie aje atoe ushuhuda hapa jf!!!!!!!

babu bado yupo moshi hajarudi.
 
Huo ni uongo mtakatifu Kamwe hiyo haiwezi kutokea wala kufanywa na Wachagga, hiyo ni kwa watu wa Tanga au Sumbawanga.
Hakuna mchagga anayeweza kufanya hayo mambo.
 
Huo ni uongo mtakatifu Kamwe hiyo haiwezi kutokea wala kufanywa na Wachagga, hiyo ni kwa watu wa Tanga au Sumbawanga.
Hakuna mchagga anayeweza kufanya hayo mambo.

Ni kweli.. yesu na maria hakuna muchagha ya ivyo puu
 
Huyo babu ni mchaga wa moshi ipi.Sibishani na hiyo story kwani zamani kuna kabila moja Arusha walikuwa wanafuga na kupanda fisi usiku nilishawahi kwenda kuyachungulia dereva anageuka nyuma anaangalia walipotoka ila babu atakuwa amefanyiziwa na watu wa huko Dar sio wa moshi
 
hayo ni mambo tu hata kama natoka usingizini siwezi kuamini,ila itasaidia kunitoa usingizi!
 
wadau wazima?

Leo bwana nimekaa mtaan kwangu na jamaa zangu wa mtaani ndio wakaanza kunipa habari hii ambayo siwezi kuthibitisha ukweli wake ila nimeona nishee na nyie wakuu.
Ni hivi kuna babu mmoja hapa mtaani kwetu huwa anapika chips na mishkaki,sasa inasemekana takriban miezi miwili imepita babu huyu ametoweka na yupo kwao moshi,ambapo siku ya tukio babu alitoka hapa eneo lake la biashara na kwenda buguruni kununua viazi kwa ajili ya chips,akapanda dalax2 ambayo ilimshusha buguruni rozana,cha ajabu babu akawa halioni soko la buguruni akazunguka sana kulitafuta mwisho wa yote akaamua kumsimamisha binti na kumuuliza lilipo soko ambapo binti alimshangaa lakini akaamua kumuonyesha babu soko lilipo tena kwa kidole tu,lakini babu kila alikuwa akiangalia haoni soko anaona nyumba tupu za watu,mwisho yule binti akaamua kumpeleka babu mpaka sokoni maana ni hapox2 walipokuwepo.
Kufikishwa sokoni babu anaambiwa "haya babu sokoni ndio hapa" lakini babu akawa haoni chochote yeye akaona amepelekwa kwenye nyumba ya mtu,akabishana sana na yule dada mwisho dada wa watu akamuona babu tapeli labda akaamua kuondoka.hapo ndio kasheshe ilipoanza.
Babu akapoteza fahamu akawa haelewi hata kilichomtokea na alikaa katika hali hiyo kwa muda usiofahamika,lakini alipopata fahamu akajishangaa kujikuta yupo kwenye gari la mkoa,alipomuuliza abiria mwenzake tunaenda wapi,abiria akamwambia arusha mzee,alipotaka kumuuliza hili ni basi gani akapitiwa na usingizi mzito sana,alipokuja kuamka akajikuta yupo katikati ya pori ambalo halieleweki ni pori gani,ila babu alianza kusikia harufu ya ubwabwa na mara akaanza kusikia sauti ya mzik mkubwa sana,alipotaka kukimbia miguu yote ikaisha nguvu na mara akaanza kusikia sauti za vicheko...
Zilipotulia sauti hizo ndio akasikia sauti ikimwambia "wewe si unajifanya mjanja hutaki kurudi kwenu??sasa unataka utaenda au hutaki utaenda tu",babu akapoteza fahamu tena.
alipozinduka akajikuta yupo juu ya fisi,na fisi anatembea taratibu sana kwenye shamba la nyumbani kwao huko moshi,mara fisi akafika kwenye uwanja wa nyumba yao na kusimama ambapo walitoka ndani ndugu zake na watoto wa kaka yake na wa kwake na kuanza kumuangalia kwa kutoamini,ndipo fisi alipomtua babu chini kwa kuanza kukaa chini taratibu huku akirudi kinyumex2 mpaka babu alipomalixa kumshusha babu,kisha fisi akaanza kurudi kinyumex 2 na mwisho akayeyuka.
Stori iliiyopo nyuma ya pazia ni kwamba babu amekaa zaidi ya miaka 10 bila kwenda kwao na aliacha mke na watoto,na kwao walikufa ndugu zake wengi ambapo kila walipokuwa wanamtafuta babu hakuwa tayari kwenda kwao kuhudhuria mazishi,mpaka mama yake mzazi alikufa lakini hakwenda,kaka yake alimtumia ujumbe mpaka akachoka na ndio mwisho akamwambia amemchoka kumvumilia na ndipi siku hiyo alipokuw analetwa na fisi,huyu kaka yake aliwaambia ndugu zake waliokuwa ndani tokeni mkampokee mgeni wetu,na walipotoka ndio wakamkuta babu juu ya fisi.

Wakuu stori hii ni babu mwenyewe ndio alipiga simu kwa kijana aliekuwa anasaidiana nae kupika chips na ndio akampa mkasa huu wote.
Dunia inamambo wakuu..samahani kwa uandishi mbaya maana natumia simu,naomba mvumilie tu.


ccm hivi chadema imewashinda mmeamia kwa wachaga na propaganda chafu


asante kwa hadithi
 
Huo ni uongo mtakatifu Kamwe hiyo haiwezi kutokea wala kufanywa na Wachagga, hiyo ni kwa watu wa Tanga au Sumbawanga.
Hakuna mchagga anayeweza kufanya hayo mambo.

Ni kweli.. yesu na maria hakuna muchagha ya ivyo puu

uchawi upo kila mkoa hauna cha kabila wala nini as wote sie hapa Tanzania ni binadamu. hata mie nilizaniaga tangu nikiwa mdogo kuwa ni mikoa hiyoo miwili tu ndo kumekucha sikuamini kuwa hata mkoani mwangu ni kama kawa na ndugu wengine ndani ya mambo hayo.

Cha muhimu duniani ni kuwa na Mungu kwanza kama mtu upo clean.
 
Huo ni uongo mtakatifu Kamwe hiyo haiwezi kutokea wala kufanywa na Wachagga, hiyo ni kwa watu wa Tanga au Sumbawanga.
Hakuna mchagga anayeweza kufanya hayo mambo.

Umdhaniye siye kumbe ndiye,
Mbona wanaomba ujuzi wa biashar kwa wakinga?
Wao si ndio sasa wameamua kuvuka hadi Nigeria,
au hilo nalo geni?
 
Mbona wanaomba ujuzi wa biashar kwa wakinga?
Mchagga hafundishwi biashara, hiyo ni natural iko damuni, kwamba fani zote zikicheua akijikita kwenye biashara anatoka.

Wao si ndio sasa wameamua kuvuka hadi Nigeria,
au hilo nalo geni?
Naamini wamekwenda huko kufanya biashara na si vinginevyo.

Ukiona mahali wachagga wapo ujue sehemu hiyo pesa inapatikana.
 
Back
Top Bottom