Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
Kuna kaka mmoja wa Kichaga alikuja kumtembelea ndugu yake hapo Zurich.
Kukaa pale kama siku tatu akaanza kuzoea na kuamua kutoka siku moja kwenda kutembea peke yake mjini. Jamaa kwa kuwa alikuwa mcha Mungu sana basi kabla ya kuondoka akasali kwanza na ndipo akaanza matembezi. Ila akajisahau kuwa huku magari yanaenda kwa kutumia mkono wa kulia. Akiwa hajui hili wala lile alibebwa na gari na mkanda wa film ukakatika. Ambulance ilikuja na kumchukua kumpeleka hospital.
Mangi kaamka baada ya kama siku mbili. Akafungua macho na anashangaa kuwa kila kitu ni cheupe. Mashuka meupe, kuta nyeupe, kimya kabisaaa. Akaanza kujikumbusha nini kilitokea mara ya mwisho. Ndipo akakumbuka kuwa aligongwa na gari na ahhhh.................................
Akaanza kusikia njaa kali na kwa mbali akamuona mwanamke kavaa nguo nyeupe na mwenyewe mweupeeeeeee...... Mangi akafahamu kuwa huyo ndiyo atakuwa mmoja ya wale alikuwa akiwasoma kwenye biblia.
Akaamua kumwita : "Aiseee dada Malaika, hebu n-patie sahani ya mto..? mtori kweliii.........."
Weekend nje? njema kweli.