Mch. Mtikila apata pigo kubwa sana

sijafulia

Member
Mar 26, 2010
86
2
Mchungaji Mtikila apata pigo


na Datus Boniface


amka2.gif
MWENYEKITI wa Chama cha Kidemokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, amepata pigo baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Wanawake wa chama hicho kujivua uanachama.
Mwanachama huyo ni Elizabeth Masanja ambaye alijiunga na chama hicho mwaka 2004; ametangaza kujivua uanachama Machi 26 mwaka huu, bila kueleza sababu zilizomfanya achukue uamuzi huo.
Elizabeth aliliambia Tanzania Daima Jumapili, kuwa alikuwa akikaimu wadhifa huo tangu mwaka juzi hivyo amemua kuachia wadhifa huo pamoja na uanachama.
“Nimeamua kujivua wadhifa huo na uanachama wa DP, kwa ridhaa yangu kama nilichukua fomu mwaka huo pia nimeamua kujivua mwaka huu,” alisema Elizabeth.
Aliongeza kwamba amefanya hivyo ili kukilinda chama hicho na pia kuongeza demokrasia nchini, ambapo ana mpango wa kuingia kwenye chama kingine cha siasa. Mwanachama huyo, alisema DP ni chama anachokipenda na kimemfanya kuwa na ujasiri wa kufanya maamuzi mazito lakini ameamua kukiacha ili akaendeleze vuguvugu la mabadiliko katika chama kingine
Mwanaharakati huyo, aliongeza kuwa mwanaharakati yeyote mwenye kupenda mabadiliko chanya ya kisiasa kamwe hawezi kurudi nyuma katika kile anachokiamini hasa katika kuwaletea maendeleo Watanzania.
 
Back
Top Bottom