Mch. Lusekelo na siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mch. Lusekelo na siasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LE GAGNANT, Sep 19, 2012.

 1. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mchungaji Antony Lusekelo kwenye kipindi chake cha chanel ten usiku huu, kasema CCM ni chama cha ukombozi. Ameonesha kujipendekeza sana kwenye chama hiki. Aidha amedai mvua za el nino zilizotabiriwa na mamlaka ya hali ya hewa hazitakuwepo, kwa mujibu wa maono yake.
   
 2. B

  Bob G JF Bronze Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kuitetea ccm kunakuhitaji uwe na akili ya kiwenda wazimu, na ndio maana hata yeye kachanganyikiwa na ccm anayoitetea kuona inamuulia Homeboy wake. Mi ninachokiona kwa Mzee wa Upako ni Matumizi mabaya ya Sadaka zetu na kujipendekeza kwa wakubwa 2
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kwani hamjamjua hadi leo kuwa anaongea mambo yale tu anayotambua kuwa yanatisha kama vile polisi wetu wanavyoongelea vitu vyenye NCHA KALI?
   
 4. E

  E K N Member

  #4
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM ni chama cha ukombozi katika lipi? Kilimo siyo, elimu nayo inadidimia, afya nayo ni yaleyale. Labda kuleana kwa kupeana vyeo vya kuteuliwa vya ufisadi. HUO NDIYO UKOMBOZI!!!
   
 5. t

  tenende JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Analinda maisha yake kwakuwa anajua Chama cha mabwepande kina allegy nao na tena anaifahamu orodha ya wahanga wote, Uli + mwa - kyembe; ndosya; ngosi, ikusa. WHO IS NEXT?!
   
 6. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,202
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Huyu tapeli anaangalia upepo.
  1. Anaona CCM madarakani na anachokifanya ni utapeli, hivyo lazima awe na strategy ya kutozuiwa utapeli wake
  2. Anaona kabisa kuwa mwelekeo ni kuwa mvua hazipo. na historia inaonyesha kuwa watu wa Meteorology utabiri wao haujawahi kuwa kama wanavyotabiri, hivyo he is banking on makosa ya met.
   
 7. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Anajipendekeza huyu kwa hawa Magamba
   
 8. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naomba tumtendee haki Mchungaji Lusekelo, nimeangalia kile kipindi tangu mwanzo mpaka mwisho. Mbali na kuongelea mvua za elnino ambazo ameziongelea mwisho wa kipindi, yeye alitumia muda wake mwingi kuwaasa watawala wanaotumia vyombo vya dola kuua raia wasio na hatia. Pia amesema jambo hilo la mauaji kwenye mikutano ya siasa kama watawala wanalitumia ili kuwatisha wananchi basi mbinu hiyo haijafanikiwa na badala yake wanawajengea usugu watanzania. Ametolea mfano wa Maandamano ya wana habari na kufukuzwa kwa waziri mwenye dhamana na jeshi la polisi, pia ameongelea umati wa watu uliohudhuria mapokezi ya viongozi wa BAVICHA Morogoro kwamba pamoja na mauaji haya yanayofanywa na vyombo vya dola bado wananchi hawaogopi kukusanyika na wanakuwa sugu zaidi.

  Akasema viongozi wa sasa wanakidhalilisha CCM na kusahau kuwa ni CHAMA kilichoasisi UKOMBOZI wa bara la Afrika na kuwataka viongozi hao waende na wakati kwa kuzingatia mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa yanayoendelea duniani na wasiwe na FIKRA mgando za kukandamiza mabadiliko haya na wakubali ukweli juu ya uwepo wa DEMOKRASIA nchini na duniani. Aliwataka pia watawala kuwa wabunifu ili kuendeleza mipango ya maendeleo ya nchi na wananchi wake badala ya kuwa wauaji.
   
 9. N

  NICE LAMECK JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mchungaji mjinga na asiyekuwa na akili mifugo hukimbia na kula mazao bila yeye kujua ndiye Lusekelo siku hizi watu wamemdharau hana jipya wala biblia haijui.
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mtajuta mno kwa pesa zenu eti kwa wana maombi wote ni wahuni tu akina Lwakatare na kampuni ya simu ya Sasatel .They are just rats
   
 11. WISE BOY

  WISE BOY JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 787
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kwa kuwa ni Mtumshi wa Mungu, sihoji wala kuuzungumzia Utumishi wake, maana mimi ni nani hata niwahukumu Watumishi wa Mungu?, Mungu mwenyewe atajua.
  Lakini kwa suala la CCM simwelewi kabisa, maana kipindi cha nyuma, hasa wakati wa ishu ya loliondo, alikuwa akihojiwa na waandishi wa habari Arusha kupitia Chanel ten kuhusu mustakabali wa nchi, aliiponda sana CCM na kukiita chama cha majambazi
   
 12. A

  Anold JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,374
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Kunawakati nishawahi kueleza kuwa kama huna hoja ya maana ni afadhali unyamaze mpaka utakapopata kitu cha maana ndiyo uwasilishe. Mimi binafsi sina kadi ya chama chochote hivyo silazimiki kupepesa macho na kujaribu kutetea chama chochote, siamini kuwa ccm ni kibaya kiasi hicho, ccm sio mashine ccm inaongozwa na watu ambao watu hao wako ndani ya jamii tunayoishi, siamini na sitalazimishwa kuamini kuwa vyama vingine vina jipya zaidi ya ccm, ingekuwa nchi inaongozwa kwa mashine na kuwa vyama hivyo vinamashine zenye ziada ya kiufundi kuliko ccm ningeelewa, sioni jipya kwenye nchi za Africa zaidi ya wanasiasa kutafuta mbinu za kuwahadaa wananchi ili kupewa ridhaa ya kuongoza dola. sio siri ccm imefanya mengi tena makubwa, ni aibu kwa watu, au wanasiasa kujaribu kutamka kuwa hakuna lolote ccm imefanya, hizi ni chuki na niabu ya wazi kwa watoa hoja. Sioni kosa la Lusekelo kutetea chama chenye historia, Vyama vingine vyote hivi hata ofisi ni utata pamoja na kupewa mafungu makubwa ya kuendesha vyama. Sioni jipya. Kwa mimi itanichukuwa muda mrefu sana kuharibiwa ufahamu wangu kuwa ccm inatatizo kubwa, ni kweli kuna mambo ya kurekebisha ila kwa sasa hakuna kama ccm.
   
 13. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ahhh kumbe wamemwekea maneno mdomoni. Uzi Mbovu huu.


  wewe uliye tuma hii thread una akili kweli au unakurupuka tu......... unatumia kichwa chako kufikiri au kufugia nywele tu...... uliangalia kipindi chote au hadithiwa na mtu.......... tatizo watu wengi walio kama wewe hawapendi kufuatilia jambo kwa undani ila wanakurupuka tu..........yeye kaeleza wazi that hawa ccm wengi wao wana mawazo mgando...... as wanafananisha nyakati hizi na zile za 1980's....... wanawatia usugu wa tz kwa kutumia polisi in siasa badala ya kujibu hoja za siasa kwa kutumia hija nzito zaidi mwisho akasema ukweli that ccm kilisaidia kupigania uhuru wa Africa kipindi hicho kilikuwa kinaitwa TANU sa wewe unabisha nini au unakurupuka tu.............. jipange mjombaaaaaaa acha paparaaaaaaaaaa
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,259
  Trophy Points: 280
  kilolambwani hafadhali umemaliza kusema kile nilichotaka kusema, hata mimi nimeangalia kile kipindi mwanzo mwisho sioni tatizo la Mchungaji Lusekelo, natowa mwito kwa wana JF tuache Inferiority complex kwamba mtu kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa kipindi awe anaiponda CCM na serikali yake tu bila hata kukumbusha kwamba asili ya CCM ni chama cha ukombozi na huu ni ukweli.

  Anayebishana na ukweli huu hawandio mimi nawaita Chadema viwavi wanaoshabikia kila kitu na wanasahau ugomvi wetu sisi na CCM siyo kwamba hakina sera nzuri, bali CCM imeacha misingi yake na CCM sasa haiongozwi na wale waliokifanya CCM wakati huo kiwe chama cha ukombozi bali sasa hivi inongozwa na majambazi na matapeli ya kisiasa. lakini hilo haliondoi ukweli kwamba Tanzania tumeshiriki kwa kiasi kikubwa kwenye ukombozi wa nchi nyingi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,259
  Trophy Points: 280
  Huna tofauti na wale wanaopinga filamu na cartoon ya kumdhalilisha mtume wakati hata hawajaiona. hear saying ni mbaya sana, unaweza kulishwa sumu kwa mtazamo wa mtu mmoja binafsi.

  Chadema kama ndio ina watu wenye mtazamo huu tukiwapa nchi mtageuka madikteta kama hamtaki kusikia habari kinyume na matakwa yenu. Lusekelo hana tatizo lolote kwa kipindi chake cha jana licha ya kwamba hata mimi najuwa fika yeye ni mganga njaa tu.
   
 16. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 280
  CCM inamkomboa mtanzania kutoka makuchani mwa CCM ha ha ha!
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,259
  Trophy Points: 280
  Pole sana endelea kulala unono na usingizi mzito, kwa sababu kwa sasa hakuna Mtazania makini mwenye mawazo kama yako.
   
 18. H

  Hume JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Tatizo watu wanasoma mikono yao ikiwa kwenye keyboard, wakati hata hawajajifikirisha juu ya kile anachosoma tayari ashaandika.
   
 19. Ndoa

  Ndoa JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kasema kutumia polisi kuzuia mikusanyiko ya wananchi ni kuwafanya wawe sugu. Katoa mfano wa maandamano ya waislamu na kusanyiko la mkutano wa CUF jangwani.
   
 20. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #20
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,259
  Trophy Points: 280
  Upuuzi mtupu watoto show wamejaa hapa wanashusha credibility ya JF kuwa kama reliable source ya habari nyingi, haiwezekani mtu anaangalia taarifa ya habari kabla msomaji wa habari ile hajaimaliza unakuta huku JF mtu kashaianzishia thread!!

  Nadhani mods sasa wawe na msako wa kuisafisha na kuondowa uchafu wote uliojaa hapa jamvini, haiwezekani mtu hujajipa hata muda wa kuelewa mtu alichoongea wewe unakimbilia JF kuanzisha thread. huu ni utoto kupindukia.
   
Loading...