Abdulhalim
Platinum Member
- Jul 20, 2007
- 17,193
- 3,011
Kijana hii kauli imetulia. Kwa kweli hata mimi nilishaamua...ikitokea hiyo harusi ikawepo..MC asahau pesa yangu. I agree..ni vema kutafuta mtu anayeweza kuchangamsha ukumbi kwa kutoa utani wenye message..Lakini mbona watu wa kawaida wanaweza? Lakini bongo bwana..harusi zimeshakuwa shughuli pevu inayohitaji substantial investment of resources..wanaogopesha vijana kuoa sasa..unakuta mdada/mkaka anataka harusi bab kubwa..kijana ndo akina Masanja hapa..choka mbaya.....Inabidi uingie mitini tuu...
Ndo maana nimemuomba Fundi aniambie anapatikana vipi. Fundi hope hutaingia mitini na kumtuma mwakilishi....I dont want "tired and recycled packaged jokes" za akina Chitanda, chumvi chumvi et al!
Tunawakodi wangoni kuja kutuimbia kwa vile kila mtu anafanya hivyo.
Amandla..........
Tatizo la bongo ni mob mentality. Watu wakianza kupelekana baharini basi wote wataenda huko. Tumefika mahali ambapo tunakodisha watu wakutuombolezea kwenye misiba. Tunawakodi wangoni kuja kutuimbia kwa vile kila mtu anafanya hivyo. Tunakodisha watu wa kutupikia kiasi kwamba tunakula chakula kile kile kila tuendapo! Kwa kufanya hivyo tunapoteza identity zetu. Kwa nini tusisherehekee na kuomboleza kivyetu? Kama ukoo una makabila mengi basi tuenzi kabila zote hizo na si hii biashara ya kuiga.
Amandla..........
Mkuu Fundi Mchundo,
Napingana na wewe kwenye hii hoja ya kuwa kwa kukodisha wapishi chakula huwa kinakuwa ni kile kile...!!! Mkuu, ukipata mpishi mzuri nina uhakika ataweza kuongeza au kupunguza "viungo" kwenye menu unayotaka. Sasa tatizo nyumbani wengi wakimpata mpishi wanasema tupikie chakula kama kile ulichopika kwenye harusi ya fulani..!! Kwa nini chakula kisifanane mkuu?
2.Sitaacha kumfagilia mwana mama ambaye anakuja kwa kasi hasa kwa beg part na kitchen part na hata harusi si mbaya anaitwa Jemima one-number yake ni 0784349570...huyu anajua kufunda nishawahi kuona akimfunda mwana mmoja jinsi ya kumtreat mke wake.
Mwanzo wake ndiyo huo. Ninavyojua mimi hao wapishi wakukodi wanakuwa na standard menu zao. Na hizi hazitofautiani. Kutokana na hili, ofa ya vyakula inakuwa limited. Lakini wakati tulipokuwa tukijipikia, tulikuwa tukipika chakula tulichozoea na chenye heshima katika jumuia au kabila letu. Ilikuwa vigumu wakati ule mtu kusema nataka chakula kama nilichokula kwenye harusi fulani maana wapishi walikuwa wengi! Hii vile vile ilijenga familia. Maana ni familia ndiyo ilihusika kuanzia kupanga menu, kuazimana masufuria na sahani, kwenda kununua chakula na viungo, kuchambua mchele au kumenya ndizi, kupika, kugawa, kukusanya vyombo na kuviosha. Mote humu tulishirikiana na tulifanya kwa kadri ya uwezo wetu. Huku kuiga mambo ya wenzetu ndiko ninakopinga.
Amandla..........
Mwanzo wake ndiyo huo. Ninavyojua mimi hao wapishi wakukodi wanakuwa na standard menu zao. Na hizi hazitofautiani. Kutokana na hili, ofa ya vyakula inakuwa limited. Lakini wakati tulipokuwa tukijipikia, tulikuwa tukipika chakula tulichozoea na chenye heshima katika jumuia au kabila letu. Ilikuwa vigumu wakati ule mtu kusema nataka chakula kama nilichokula kwenye harusi fulani maana wapishi walikuwa wengi! Hii vile vile ilijenga familia. Maana ni familia ndiyo ilihusika kuanzia kupanga menu, kuazimana masufuria na sahani, kwenda kununua chakula na viungo, kuchambua mchele au kumenya ndizi, kupika, kugawa, kukusanya vyombo na kuviosha. Mote humu tulishirikiana na tulifanya kwa kadri ya uwezo wetu. Huku kuiga mambo ya wenzetu ndiko ninakopinga.
Amandla..........
Mkuu, haya ya kuajiri wapishi na wataalamu wa menu ndio maendeleo yenyewe haya.
Hayo yote uliyasema hapo juu "kuazimana masufuria na sahani, kwenda kununua chakula na viungo, kuchambua mchele au kumenya ndizi, kupika, kugawa, kukusanya vyombo na kuviosha" yamepitwa na wakati. Tena, ili mradi uchumi unaruhusu nisingependa turudi huko.
Yote yaho yalikuwa yanafanywa na kina mama, matokeo yake wakina mama ambao walitakiwa wakae wajumuike kwenye sherehe ya binti yao kuolewa wanakuwa wako busy kazini kuhudumia wageni wengine hasa wa kiume...hilo mimi nalipinga kabisa.
Wakina mama nao wanatakiwa watumie muda huo wa kupika kujipamba na kuburudika kwa nguvu badala ya kuwa wako kazini.
Mimi nilimwamini sana MC Chitanda. Kwani mavazi yake yanavutia awpo kwenye kazi yake. Huwa anapendelea kuvaa kama Mnaigeria. Nashukuru kwa kunipa alivyo Mc huyu. Inabidi tumuogope na kumwepuka kama ukoma.
Angalia basi tunavyo-complicate mambo. Kuna sherehe ya kuposa. Halafu sherehe ya kutambulishana. Halafu sherehe ya kupokea mahari. Hizi kwa bahati nzuri sehemu nyingi bado hazijawa corrupted.Baada ya tarehe ya harusi kutajwa ndipo fujo zinapoanza.
Tunaanza na Kitchen Party. Hii imekuwa corrupted. Badala ya kuwa ya kifamilia, kumfunda mwanao, kumpa vifaa vya nyumbani n.k. sehemu kubwa imewekwa kwenye mafunzo ya kujamiana. Imefika mahali tunakaribisha mashoga kutoa shule! Mafunzo yaliyokuwa na umuhimu katika jamii sisi tunayafanyia mas'hara! Hii vile vile imekuwa sehemu ya wakina mama kutambiana. Na kwenyewe tunakodi kila kitu maana hakuna mwenye sherehe, wote ni waalikwa wasiotaka kuchafuka siku ya sherehe.
Halafu tuna send-off. Hii nayo imekuwa corrupted. Badala ya kuwa sehemu ya ndugu za binti kumuaga ndugu yao imekuwa siku ya kuwaonyesha wanaotaka kuoa jinsi alikotoka binti kulivyo maji marefu. Hizi nazo zimekuwa ni reception bila harusi. Na kwenyewe hakuna mwenye shughuli. Wote ni waalikwa wasiotaka kuchafua pamba zao! Wazazi wakiwa na bahati wanapewa nusu dakika kumuasi binti yao maana MC anaenda na time na watu wengi walichofuata ni ulabu, muziki na vichekesho vya Mc na si nasaha za wazazi.
Siku ya harusi, ndiyo tusiseme. Hasira zote za kunyimwa kadi kwenye send-off tunamalizia hapa. Na penyewe cha muhimu ni kuwaonyesha watu jinsi tunavyoweza kula, kunywa na kusaza. Sifa imekuwa ni ufunguaji wa champeni na si nasaha za wazazi. Ndugu ambao hawakuwa na uwezo wa kuchanga ndiyo walie. Viti vya heshima vinapewa kwa hao wenye deep pockets, hata kama uhusiano nasi ni mdogo. Hapa tena mkazo si kwenye kushiriki bali ni kuonekana. Na penyewe hamna mwenye shughuli. Wote ni wageni. Wote wanaingia kwa kadi maana kamati ya harusi haina mashara. Hela zote zilizochangwa ni lazima watu wagide. Hakuna free loaders hapa hata kama wanaooana ni wapwa wao. Ngoma za asili nazo zinapewa dakika mbili maana ratiba ilichelewa kwa sababu maharusi walienda kupiga picha bich au Mlimani City! Maharusi wanatangulizwa na matarumbeta. Chakula ni kile kile, chips kidogo, wali, shingo la kuku, kipande cha chapati, mboga zilizochoka na ndizi zisizojulikana zilikotoka! Tunajipanga kupeleka hzawadi zetu za bilauli zilifungwa kwenye mabox na makaratasi mazuri. Maharusi wanacheza rumba moja kutoka katika muziki kutoka ughaibuni. DJ kuonyesha uzalendo anapiga Chakacha, bongo flava n.k. Wacheza ngoma za kitamaduni wako hoi maana hakuna aliyekumbuka kuwapa chakula. Watu wanatapika, wanajisaidia hovyo halafu wanaondoka wakisifia harusi.
Baada ya wiki mbili, tunavunja kamati. Hapo napo tunaelezwa kuwa kuna mbinamu wa Bwana harusi nae anakusudia kuoa hivi karibuni. Kamati inaundwa upya. Mchezo unaanza tena. Ndiyo maisha yetu. Ndiyo maendeleo yetu.
Count me out!
Amandla........
Kumbe Chihanda alipendwa kwa vile anavaa kama wanaijeria? Nazidi kusononeka.