Mbwembwe za ndege zimeishia wapi?

Corona imeanza juzi hebu tupe faida ya ndege zetu kuanzia 2016 hadi 2019 kabla ya corona.
Hawawezi kukupa jibu mkuu! Ule mradi wa ndege ulikua ni wa kukurupuka na kutafuta sifa tu. Hauna faida yoyote kwa Watz
 
Kuna kitu kinaitwa Corona, umeshawahi kukisikia? Nauliza tu
 
Daah naunga mkono hoja mzee mataga alikurupuka sana.
 
Tanzania hatuna vipaumbele. Tulitakiwa kumaliza kwanza madarasa na barabara na vituo vya afya..
 
Ndege anapanda mwenyewe kwenda kwake
 
Utakufa na stress wewe vipi Mwenyekiti amepona na Faru John?
 
Tanzania hatuna vipaumbele. Tulitakiwa kumaliza kwanza madarasa na barabara na vituo vya afya..
Hangaika na Faru John. Leo WB wameitangaza TZ ni nchi yenye Kipato cha Kati. Pole sana!
 
COVID19 subiri huyu mdudu akidhibitiwa na anga za dunia zikifunguka ndio utajua ile midege ni asset au liability. Kwa sasa dunia karibu yote inalia na wale wasio na uwezo wa kusaidia airlines zao ndio zinaelekea kuzimu. Tanzania tuna utajiri wa kutosha ATCL lazima itaibuka tu.
 
Corona huioni wewe eeeh..
 
Nilifurahi sana serikali ilipofufua shirika hili, hata kama linaenda kwa hasara, tuwe na shirika letu
Safi mkuu, tunahitaji uwekezaji huu sana na ni kwa manufaa yetu sote, tunasema tuna vivutio vya utalii lakini means of transport ni poor, usafiri wa anga rais wangu aliona mbali sana,

wengi hawawezi kuliona hilo, na wala hawawezi kuona faida mapema baadae watakuja kuelewa, na watakuja kwenye huu uzi wakijutia walichokua wakipinga, ukijaribu kuonyesha tija wa huu uwekezaji watu wanatamani hata kukutoa roho,
 
Ndege hazina faida mkuu, hatuwezi kukejeli maendeleo kwa maana halisi ya maendeleo lakini hatuwezi kuunga mkono miradi tunayojua wazi itatutia hasara.
Baba yako akianzisha biashara ya barafu Makete utamuunga mkono?
Bila bila [emoji41][emoji41]
 
Naoana post yangu imefutwa, narudia tena hivi unaweza ukafurahi baba yako kufeli, utakua mzima kweli, hizi ndege ni kwa faida ya nani? Ni yetu sote watanzania lilifanyika jambo hili kwa manufaa yetu lakini watu mnakejeli sana uwekezaji huu.
Sema kwa faida ya wachache,ni lini masikini anayehangaikia mlo mmoja kwa siku atapanda ndege?hata hesabu za manunuzi yake zimefichwa au we unazo?
 
Naoana post yangu imefutwa, narudia tena hivi unaweza ukafurahi baba yako kufeli, utakua mzima kweli, hizi ndege ni kwa faida ya nani? Ni yetu sote watanzania lilifanyika jambo hili kwa manufaa yetu lakini watu mnakejeli sana uwekezaji huu.
Hazina faida yoyote, mlikurupuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…