Mbwembwe za ndege zimeishia wapi?

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Tulikuwa hatulali kila kukicha kesho angalieni mawinguni, Serikali nzima ilikuwa inakesha airport kusubiri Bombardia, kila hotuba hata iwe kanisani lazima izungumzie ununuzi wa ndege, faida ya ndege, na majigambo kede kede, zile ahadi za kuifanya Dar hub of Afrika zimeishia wapi.

Sisi wachache kina Quinine, barafu, kina Zitto tuliwatahadharisha mapema, tuliwaambia MATAGA biashara ya ndege ni ngumu sana inahitaji back up kubwa ya Serikali hatukueleweka, OK, sasa midege haina route za nje imepaki tu airport mingine ikiishia kuzunguka Kibondo - Ngara kwa hasara, tumebaki kuzindua Rwandair ikibeba mizigo ya samaki Mwanza kupeleka Ulaya.

MATAGA tupeni mrejesho, Msemaji Mkuu wa Serikali lini tena tuangalie mawinguni.
 
Naoana post yangu imefutwa, narudia tena hivi unaweza ukafurahi baba yako kufeli, utakua mzima kweli, hizi ndege ni kwa faida ya nani? Ni yetu sote watanzania lilifanyika jambo hili kwa manufaa yetu lakini watu mnakejeli sana uwekezaji huu
Kama baba yako unamshauri usipite njia hii ina simba hataki utafanyaje kama siyo kumkumbusha si nilikwambia.
 
Nyie watu hakika kuna mahali mnalipwa, huwezi kushupaza shingo namna hii.

Tatizo la usafiri wa anga halijaikumba TZ peke yake, ingekuwa nchi yetu ndio pekee imeumia hapo ungekuwa na hoja, lakini hili janga ni la dunia nzima. Unataka serikali ifanyaje hapo?
 
Naoana post yangu imefutwa, narudia tena hivi unaweza ukafurahi baba yako kufeli, utakua mzima kweli, hizi ndege ni kwa faida ya nani? Ni yetu sote watanzania lilifanyika jambo hili kwa manufaa yetu lakini watu mnakejeli sana uwekezaji huu

Ni vema umekiri kuwa ZIMEFELI, hayo mambo ya baba usimtumie kwenye mifano ya hovyo. Inategemea pia ulimshauri nini kabla.
 
Naoana post yangu imefutwa, narudia tena hivi unaweza ukafurahi baba yako kufeli, utakua mzima kweli, hizi ndege ni kwa faida ya nani? Ni yetu sote watanzania lilifanyika jambo hili kwa manufaa yetu lakini watu mnakejeli sana uwekezaji huu
Baba akifeli watoto wenye akili lazima wamwambie ukweli. Ila mitoto ya mama inakaa kimya au inasifia ujinga wa baba...

Nikimwona baba yangu anafanya mambo ya kipuuzi inayokwamisha maendeleo ya familia, namwambia ukweli. Akileta ujinga naweza kumkwida...

Bahati nzuri baba yangu hajawahi fanya hayo, na hivi sasa nimekuwa baba tayari. Siwezi kufanya ujinga pia...

Baba unanunua magari ya kifahari, tunaishi kwenye nyumba ya kupanga unanisomesha shule ya kata, unaendekeza nyumba ndogo... ukikaa vibaya nakucharaza bakora
 
Nyie watu hakika kuna mahali mnalipwa, huwezi kushupaza shingo namna hii.

Tatizo la usafiri wa anga halijaikumba TZ peke yake, ingekuwa nchi yetu ndio pekee imeumia hapo ungekuwa na hoja, lakini hili janga ni la dunia nzima. Unataka serikali ifanyaje hapo?
Usafiri wa anga haujawahi kuwa kipaumbele kwa taifa letu. Baba akichemka lazima aambiwe ukweli. Mandege yanaoza eapoti pale... Hospitali zisingeoza, shule zisingeoza, barabara zisingeoza...
 
Nyie watu hakika kuna mahali mnalipwa, huwezi kushupaza shingo namna hii.

Tatizo la usafiri wa anga halijaikumba TZ peke yake, ingekuwa nchi yetu ndio pekee imeumia hapo ungekuwa na hoja, lakini hili janga ni la dunia nzima. Unataka serikali ifanyaje hapo?
Sijui kama wanatambua corona imeleta athari kubwa sana, hasa kwenye sekta ya utalii na vivyo hivyo usafiri wa anga, watu wanasahau haraka sana, na kupandisha uzi wa namna hii
 
Ni vema umekiri kuwa ZIMEFELI, hayo mambo ya baba usimtumie kwenye mifano ya hovyo.... inategemea pia ulimshauri nini kabla.
Hivi janga la Covid-19 hujui kama limeleta athari kubwa sana, na kuathiri usafari wa anga pia, unachokosoa hapo ni nini, usomi wenu huwa mnasomea nini huko mashuleni mnashindwa hata kutoa tasmini za hapa na pale
 
Endeleeni kutumia kovidi kama kivuli cha kujificha, muda utaongea tu!

Siku hizi kila kitu kovidi, hata mdeni wangu hanisumbui tena... namwambia tu hali ni mbaya si unaona!!!
 
Kama ilivyo kosa matumizi Quinine baada ya ugonjwa wa malaria kutokomezwa na serikali ya awamu ya 5 na ndivyo wana ufipa mmekosa kabisa muelekeo, hamjitambui kabisa na hamjui vipawa mbele vyenu kwenye huu uchaguzi ni vitu gani. Wewe endelea kutafuta wagonjwa wa Malaria ili waitumie hiyo Quinine wakati wadudu wanaosababisha Malaria hawapo
 
Back
Top Bottom