Mbwana Samatta uwezo wake wa kawaida Mno, Anabebwa na bahati tu!

Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa Mbwana Samatta Tangu alivyotua katika Club ya KRC Genk ya Belgium akitokea TP Mazembe ya DRC.

Kiukweli jamaa kiwango chake ni cha kawaida sana na anabebwa sana na bahati kubwa aliyonayo kwani performance yake haitishi sana.

Ukiangalia magoli anayofunga asilimia kubwa ni ya kawaida sana yasiyo na ufundi (hufunga zaidi kwa kichwa na asilimia kidogo kwa mguu na setpieces).

Kwa namna soka la Ulaya lilivyokuwa na ushindani hasa kwa mabeki wakatili (kama akina Pepe) sioni Samatta akifanya lolote mbele yao, kwani mbinu zake mguuni hazitishi mabeki na ni za kawaida sana.

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.....Jamaa some how Anajitahidi na anaendelea kujitahidi kwani ameonesha ujasiri na amekuwa Idol kwa Vijana wengi wenye ndoto za mafanikio kwenye soka kama ya Samatta.

Kama ataweza kuuona uzi huu au aambiwe na mtu wake wa karibu aliyeko humu basi nimwombe ndugu yangu Samatta, aongeze zaidi juhudi na ajifunze mbinu nyingi za kufunga kwani yeye kama forward kazi yake uwanjani ni magoli tu na si vinginevyo. Bila kisahau Kujisahau na Kuvimba kichwa akuepuke sana kwani magazeti ya bongo yanapamba wachezaji hadi wanakuwa under pressure na mwishowe huharibu carrier yao.
Mwenye bahati, habahatishi mkuu
 
hakuna anayediss, shabiki LAZIMA atashabikia tu no matter what....kwa hiyo Usishangae wazungu wa RKC Gent kumshangilia Samata, wanampa motisha wa kufunga. Ukweli ni kwamba Samatta ana mpira wa kawaida tu, hii wala si kudiss.
Mkuu naamini wewe utakuwa unajua soka. Namba nijuze thamani ya jezi namba 10 katika timu, namaanisha ni watu wa namna gani hupewa jezi hiyo? Pia unijuze kwanini Samatta mwanzo alikuwa anavaa jezi namba 77 pale Genk ila baadaye wakampa namba 10 ambayo anavaa hadi sasa.

Mwisho timu yake inaitwa KRC Genk, maana nahisi hata timu yake inakusumbua kidogo. Pia sio kila mchezaji anashangiliwa kwa kutungiwa nyimbo, wengine ni kwa kuwakuna mashabiki
 
Hili ni tatizo la kuanza kuangalia mpira ukubwani, kiwango cha samatta kinatisha kaka na ninakuhakikishia muda si mrefu utasikia ameenda premier league

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
MTU anayemponda Samatta ukimwambia yeye acheze utafikiri unaangalia futuhi. Wabongo tuna tabia ya kuponda na kuwa na negative mindset. Ndo maana Mimi hata biashara ya urafiki nilishaikataa muda sana. Naona unafiki tu.
 
Mkuu naamini wewe utakuwa unajua soka. Namba nijuze thamani ya jezi namba 10 katika timu, namaanisha ni watu wa namna gani hupewa jezi hiyo? Pia unijuze kwanini Samatta mwanzo alikuwa anavaa jezi namba 77 pale Genk ila baadaye wakampa namba 10 ambayo anavaa hadi sasa.

Mwisho timu yake inaitwa KRC Genk, maana nahisi hata timu yake inakusumbua kidogo. Pia sio kila mchezaji anashangiliwa kwa kutungiwa nyimbo, wengine ni kwa kuwakuna mashabiki

Dogo sikia, kuvaa jezi namba 10 haimaanishi chochote, anybody can wear it. Hata kama wewe unataka sema tu nikupe ya taifa Stars.
 
Tatizo kubwa la TZ, wachezaji na makocha ni consistency ya ubora
Kocha na wachezaji wakimaintain ubora wa jana Afcon 2019 ni yetu na makubwa zaidi tutarajie
Tatizo la kushindwa kwetu sijui itakuwa ni viongozi bila kupepesa macho
 
Na kuendelea hapana sasa majungu tu kila siku
MTU anayemponda Samatta ukimwambia yeye acheze utafikiri unaangalia futuhi. Wabongo tuna tabia ya kuponda na kuwa na negative mindset. Ndo maana Mimi hata biashara ya urafiki nilishaikataa muda sana. Naona unafiki tu.
 
Ndiyo hivyo, kwa majungu usiseme utasikia hafiki mbali huyo si wauswahilini , unajiuliza huyu Vipi. kumbe wivu
Roho mbaya,husda,chuki na wivu ndo vijana wengi wa Tanzania tunajua.Kwanza wakati anahangaika mwenyewe hakuna hata aliyemsaidia leo kawa maarufu basi kila mtu anajidai kumkosoa huo ndo unafiki mim siupendi.
 
Dogo sikia, kuvaa jezi namba 10 haimaanishi chochote, anybody can wear it. Hata kama wewe unataka sema tu nikupe ya taifa Stars.
Hakika hapa nimeamini kuna watu hawajui soka. Sasa anza kufuatilia jezi namba 10 huvaliwa na watu gani kwenye timu
 
Back
Top Bottom