Mbwana Samatta uwezo wake wa kawaida Mno, Anabebwa na bahati tu!

Samatta ni mmoja kati ya washambuliaji bora Afrika kuwahi kuwaona wakitandaza gozi. Ni mshambualiaji anayeweza kukupatia magoli kutoka miguu yote, kwa mashuti makali na kudokoa. Anakupatia magoli ya kutosha kwa kichwa na anapiga vizuri mipira ya kutenga. Ana kasi, chenga na udhibiti wa kutosha wa mpira (ball control)

Nilianza kumfuatilia tangu akiwa African Lyon jinsi mabeki walivyopata shida kuutoa mpira miguuni pake licha ya kuwa na umbo dogo. Nakumbuka mechi moja kati ya Simba isiyofungika na African Lyon alivyoweza kuongoza eneo la ushambuliaji akiwa almost peke yake dhidi ya mabeki katili Kelvin Yondani, Juma Nyoso na Jerry Santo. Kilikuwa ni kipaji kisicho cha kawaida.

Hata hivyo, nadhani Samatta amebadilisha mtindo wake wa kusakata soka. Amejifunza kucheza kiulayaulaya, yaani kama ni chenga basi lazima iwe na sababu. Siku hizi habebi tena kijiji kama zamani. Ninaamini mpira anaocheza ni ule anaofundishwa kutimiza majukumu kwa ajili ya timu.
 
Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa Mbwana Samatta Tangu alivyotua katika Club ya KRC Genk ya Belgium akitokea TP Mazembe ya DRC.​
Kiukweli jamaa kiwango chake ni cha kawaida sana na anabebwa sana na bahati kubwa aliyonayo kwani performance yake haitishi sana.​
Ukiangalia magoli anayofunga asilimia kubwa ni ya kawaida sana yasiyo na ufundi (hufunga zaidi kwa kichwa na asilimia kidogo kwa mguu na setpieces).​
Kwa namna soka la Ulaya lilivyokuwa na ushindani hasa kwa mabeki wakatili (kama akina Pepe) sioni Samatta akifanya lolote mbele yao, kwani mbinu zake mguuni hazitishi mabeki na ni za kawaida sana.​
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.....Jamaa some how Anajitahidi na anaendelea kujitahidi kwani ameonesha ujasiri na amekuwa Idol kwa Vijana wengi wenye ndoto za mafanikio kwenye soka kama ya Samatta.​
Kama ataweza kuuona uzi huu au aambiwe na mtu wake wa karibu aliyeko humu basi nimwombe ndugu yangu Samatta, aongeze zaidi juhudi na ajifunze mbinu nyingi za kufunga kwani yeye kama forward kazi yake uwanjani ni magoli tu na si vinginevyo. Bila kisahau Kujisahau na Kuvimba kichwa akuepuke sana kwani magazeti ya bongo yanapamba wachezaji hadi wanakuwa under pressure na mwishowe huharibu carrier yao.​
Punguza roho, mbaya in wangapi wachezaji was mpira was miguu ,toka Tanzania iumbwe wamefikia Mafanikio ya samata hata robo?

OK , hana kipaji

1. Alishinda kuwa mfungaji bora ligi ya Kongo DR

2. Mchezaji Bora Afrika kwa wachezaji was ndani

3. Kaenda Genk kapewa jezi namba 77 akitokea benchi ,Leo anavaa jezi ya heshima namba 10 na anauwezo wa kubadili matokeo dakika yoyote Genk ikiwa jahaz linazama

4. Ndiye tegemeo la kocha na mashabiki wa Genk

5. Katika historia ya Genk haijawahi mchezaji kuimbiwa wimbo na mashabiki hata kelvin De Bruyne akufanyiwa hivyo

NB 1: usifikiri wewe ndio unakisumbuzi cha Dstv peke yako hadi useme tunaangalia kwa Shaffih dauda

NB2 : Kama ulishindwa kucheza mpira na kupata mafanikio , acha uchawi kwa waliofanikiwa ,mpira unaongozwa na Nidhamu

NB3: Miongoni mwa watanzania na wazalendo wanaolitangaza hili Taifa ni mbwana samata

Heko our Hero mbwana samata ,songa mbele na kilinde kipaji chako adhimu
 
sijadis mkuu...ukisoma uzi vizuri utagundua kuwa niliousema ni ukweli mtupu...labda tatizo lako ni kuwa huangalii mechi za Genk live sansana unaangalia updates na clips kwa akina Shaffii Dauda na Millard Ayo!.... Jaribu kuangalia mechi za KRC Genk utarudi kunipa tawile!
Hebu niambie hawa washambuliaji walikuwa/wana ufundi gani zaidi ya kufunga tu..
1. Philipo Inzaghi
2. Javier Hernandez (Chicharito)
3. Olegunar Solkerjaer (sina uhakika na spelling)
4. Ruud Van Nestrolooy.

By the way kazi yake ni kufunga. Hayo magoli ya vichwa wewe unaona kama rahisi lakini ni kazi kubwa sana kama hujui kujiposition na kutoroka mabeki. Unakumbuka kilicho mpa umaarufu Patrick Kluivert?
 
Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa Mbwana Samatta Tangu alivyotua katika Club ya KRC Genk ya Belgium akitokea TP Mazembe ya DRC.​
Kiukweli jamaa kiwango chake ni cha kawaida sana na anabebwa sana na bahati kubwa aliyonayo kwani performance yake haitishi sana.​
Ukiangalia magoli anayofunga asilimia kubwa ni ya kawaida sana yasiyo na ufundi (hufunga zaidi kwa kichwa na asilimia kidogo kwa mguu na setpieces).​
Kwa namna soka la Ulaya lilivyokuwa na ushindani hasa kwa mabeki wakatili (kama akina Pepe) sioni Samatta akifanya lolote mbele yao, kwani mbinu zake mguuni hazitishi mabeki na ni za kawaida sana.​
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.....Jamaa some how Anajitahidi na anaendelea kujitahidi kwani ameonesha ujasiri na amekuwa Idol kwa Vijana wengi wenye ndoto za mafanikio kwenye soka kama ya Samatta.​
Kama ataweza kuuona uzi huu au aambiwe na mtu wake wa karibu aliyeko humu basi nimwombe ndugu yangu Samatta, aongeze zaidi juhudi na ajifunze mbinu nyingi za kufunga kwani yeye kama forward kazi yake uwanjani ni magoli tu na si vinginevyo. Bila kisahau Kujisahau na Kuvimba kichwa akuepuke sana kwani magazeti ya bongo yanapamba wachezaji hadi wanakuwa under pressure na mwishowe huharibu carrier yao.​
Duuh
 
Nawaza tyuuu.. Mchezaji wa tz aliyeshinda tuzo ya best player based in Africa ww wasema wakawaida??? Unataka magoli au magoli ya kiufundi????... Coz mm naamini hayo magoli anafunga coz anajua namna ya kujiposition katika nafasi na kuweza kufunga ...inamaana wale mascout wa genk walipoint kwa mchezaj wa kawaida??? Vp kuhus hao wa levante???

Mkuu jaribu kumwangalia vizur sama goal....unaangaliaga magoli ya chicharito????
 
Nadhani amefocus kwenye Belgium league ili asiumie,kwa waliojituma leo Msuva kajituma hata ulimwengu kuliko Samata,Samata asingeingia hata pengo lisingeonekana
 
hata leo nimemwangalia hana jipya
 
Nadhani amefocus kwenye Belgium league ili asiumie,kwa waliojituma leo Msuva kajituma hata ulimwengu kuliko Samata,Samata asingeingia hata pengo lisingeonekana
Kweli kabisa..jamaa leo kaigharimu timu...
 
Mkuu mi nimekuelewa mm mwenyewe nimeligundua hili
Sasa wewe unaweza kucheza japo dakika 10 kwa hiyo bahati ya samatta?,kama huwezi funga mdomo wako acha kumsema kijana wetu ambae hatua as liyofikia ni kubwa mno,kwani huko kwenye timu yake mwenye bahati ni samatta tu?wengine hawana?,vipi kwani siku hizi bahati ni sehemu ya sifa au vigezo vya kusajili wachezaji?
 
Sifa ya namba 9 ni kufunga tu na si kingine....kufunga si kitu kirahisi jamani...drogba zaidi ya kufunga alikuwa na nini??harrry kane tisa bora sasahivi zaidi ya kufunga ana nini???mwacheni samatta aendelee kuperfom
 
Uzuri wa soka la ulaya hawaangalii huyu ni nani wanaangalia miguu inasemaje kama samatta miguu yake iko smart kihivyo dau litapanda mabig watazidi kumgombania kama akina dembele kama wa kawaida napo tutamwona akitafutwa na mameneja wanaouza wachezaji malysia huko.
 
Back
Top Bottom