Mbwana Samatta uwezo wake wa kawaida Mno, Anabebwa na bahati tu!

Louis II

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
3,030
4,645
Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa Mbwana Samatta Tangu alivyotua katika Club ya KRC Genk ya Belgium akitokea TP Mazembe ya DRC.

Kiukweli jamaa kiwango chake ni cha kawaida sana na anabebwa sana na bahati kubwa aliyonayo kwani performance yake haitishi sana.

Ukiangalia magoli anayofunga asilimia kubwa ni ya kawaida sana yasiyo na ufundi (hufunga zaidi kwa kichwa na asilimia kidogo kwa mguu na setpieces).

Kwa namna soka la Ulaya lilivyokuwa na ushindani hasa kwa mabeki wakatili (kama akina Pepe) sioni Samatta akifanya lolote mbele yao, kwani mbinu zake mguuni hazitishi mabeki na ni za kawaida sana.

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.....Jamaa some how Anajitahidi na anaendelea kujitahidi kwani ameonesha ujasiri na amekuwa Idol kwa Vijana wengi wenye ndoto za mafanikio kwenye soka kama ya Samatta.

Kama ataweza kuuona uzi huu au aambiwe na mtu wake wa karibu aliyeko humu basi nimwombe ndugu yangu Samatta, aongeze zaidi juhudi na ajifunze mbinu nyingi za kufunga kwani yeye kama forward kazi yake uwanjani ni magoli tu na si vinginevyo. Bila kisahau Kujisahau na Kuvimba kichwa akuepuke sana kwani magazeti ya bongo yanapamba wachezaji hadi wanakuwa under pressure na mwishowe huharibu carrier yao.

NB: Kama itaonekana sina haki ya kumkosoa Huyu dogo Basi no one has the right to critisize my opinions too.
 
Wakati wazungu wanaimba SamaGoal...SamaGoal. Wabongo tunadis.

Sent using Jamii Forums mobile app
sijadis mkuu...ukisoma uzi vizuri utagundua kuwa niliousema ni ukweli mtupu...labda tatizo lako ni kuwa huangalii mechi za Genk live sansana unaangalia updates na clips kwa akina Shaffii Dauda na Millard Ayo!.... Jaribu kuangalia mechi za KRC Genk utarudi kunipa tawile!
 
sijadis mkuu...ukisoma uzi vizuri utagundua kuwa niliousema ni ukweli mtupu...labda tatizo lako ni kuwa huangalii mechi za Genk live sansana unaangalia updates na clips kwa akina Shaffii Dauda na Millard Ayo!.... Jaribu kuangalia mechi za KRC Genk utarudi kunipa tawile!
Lukaku anafunga magoli ya ufundi?... Mwisho wa siku kinachotakiwa ni magoli...haijalishi hata kama yamefungwa kwa mkono au kiuno
 
Kwasababu wewe sio kocha wa Genk au timu yoyote ya soka ndio maana umemuona wa kawaida na utaendelea kumuona wa kawaida.
Halafu unaomuona wa kawaida sana na hatishi ukimlinganisha labda na nani anayetisha au ulitaka atishe kwenye nini zaid ili ufikie uamuzi wa kumuona anatisha?
Aliyemsajili anaijua kazi yake na ndiye ayemtuma afanye hayo unayoyaona miguuni mwake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lukaku anafunga magoli ya ufundi?... Mwisho wa siku kinachotakiwa ni magoli...haijalishi hata kama yamefungwa kwa mkono au kiuno
Tofauti ya Lukaku na Samatta ni kwamba, Lukaku anafunga magoli mazuri na ya kiufundi na pia anakosa magol magoli mepesi...Samatta yeye anafunga magoli mepesi yasiyo na ufundi
 
Back
Top Bottom