Mbwana Samatta avunja rekodi kedekede

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,823
109,109
Ma Shaa Allah.

Kijana wetu amevunja rekodi zifatazo mpaka sasa.

1) Mtanzania wa kwanza kucheza Premier League ya Uingereza.

2) Mtanzania wa kwanza kufunga goli la Premier League.

3) Mtanzania wa kwanza kufunga goli la Premier League kwenye mechi ya kwanza.

4) Mtanzania wa kwanza kufunga goli la kichwa la kwanza la Aston Villa toka msimuu huu uanze.

5) Mchezaji wa kwanza kupanda thamani ndani ya Premier League msimu huu ndani ya mechi mbili tu.

Ongezea...

Samatta anatarajiwa kucheza tena tarehe 16-02-2020 wakati timu yake itapopambana na Tottenham (timu ya Uingereza anayoshabikia Kikwete).

Tumuombee dua njema kijana wetu, anatupeperushia bendera yetu ya Tanzania vizuri kabisa huko Uingereza.

Allah amuondolee na amuepushe na hassad zote. Amiiin.

Samatta.jpg


Mtanzania wa kwanza kuwa Mchezaji bora + Top score Caf Champions League.
Mtanzania wa kwanza Kucheza UEFA CL + Kuscore.
 
Utaharibu uzi sasa hivi.

Samatta ni kijana wa mfano kwanza hana maringo na mstaarabu sana ukitaka kuthibitisha angalia pesa anayolipwa na maisha anayoishi. Pia, angalia lile sakata alivyokua anashambuluwa na sisi watanzania kwa kucheza vibaya timu ya taifa angalia jinsi alivyojibu jwa utulivu na upole.
Waislam tuna vipaji sana Allah mkubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mtazamo wangu mimi namba 4 ndio kavunja rekodi sababu aliwakuta watu tayari wanacheza yeye kafanya yake!! Na tena sio mtanzania, nina wasiwasi goli lake ndio goli la kwanza la kichwa kwa Aston Villa toka msimu huu uanze kama sijakosea.

Sasa 1 mpaka 3 kavunja rekodi ya nani! Mie naona tuseme kuwa ndugu yetu samatta kaweka rekodi!

Na nadhani rekodi yake namba 1 ngumu kuja kuvunjwa, atakaejaaliwa kwenda kucheza EPL hatovunja rekodi ya Samatta ila atakuwa kaweka rekodi yake kuwa Mtanzania wa pili kucheza EPL.
 
Kichwa cha habari ulipaswa kutumia neno "aweka rekodi" na si "avunja rekodi" kwa maana hapo kabla yake hakukuwa na mtanzania aliyeshikiria hizo rekodi.

Sent using Jamii Forums mobile app

= Aliyeshikilia

Wapo (yupo) aliye/waliokwisha cheza ligi zingine za Ulaya, hata yeye mwenyewe kishacheza ligi nyingine Ulaya.

Hapa amevunja rekodi na ndiyo kaweka hiyo rekodi mpya. Huwa sikisii.
 
Utaharibu uzi sasa hivi.

Samatta ni kijana wa mfano kwanza hana maringo na mstaarabu sana ukitaka kuthibitisha angalia pesa anayolipwa na maisha anayoishi....pia angalia lile sakata alivyokua anashambuluwa na sisi watanzania kwa kucheza vibaya timu ya taifa angalia jinsi alivyojibu jwa utulivu na upole.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa kasema ukweli unadhani faiza angeandika kama huyu mchezaji angekuwa anaitwa Patrick?
 
Mechi za Aston Villa za EPL zijazo,

Villa vs Spurs
Southampton vs Villa
Leicester vs Villa
Villa vs Chelsea
Newcastle vs Villa
Villa vs Wolves
Liverpool vs Villa
Villa vs Manchester utd
Villa vs Palace
Everton vs Villa
Villa vs Arsenal
Westham vs Villa,

Hapa Aston villa lazima wakaze, mechi ni ngumu, Samatta apige kazi ili hata kama Villa itashuka Championship, yeye asajiliwe na team nyingine inayoshiriki EPL.

Good luck MBWANA SAMATTA
Good luck ASTON VILLA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom