Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,238
- 12,753
SIKU moja mbwa wa mwitu alikuja anywe katika kijito cha maji, akamkuta mwana kondoo mchanga akasimama karibu na kijito. Mbwa wa mwitu akataka kugombana naye apate kumua. Akamwambia, “Mbona unaborugaboruga matope nisipate maji safi?” Kondoo mchanga akamwambia. “Gissi gani nikutilie taka majini, yakiwa yanashuka kwako kunifikia mimi?” Mbwa wa mwitu akamwambia, “Uthubutuje kunywa wewe, kabla sijanywa mimi?” Akamwambia mwana kondoo. “Mimi sinywi maji, maziwa ya mamangu yanitosha.” “Bassi,” akamwambia mbwa wa mwitu, “mbaya wee, mwaka jana umenitukana.” Eeh Bwana” akamwambia mwana kondoo, “Mwaka jana nalikuwa sijazaliwa.”
Mbwa wa mwitu akakasirika sana akamwambia, “Kama si wewe, ndiye baba yako, sijui kuwapambanua, mmestahili kufa wote.” Akamkakata, akamue, akamla.
Mbwa wa mwitu akakasirika sana akamwambia, “Kama si wewe, ndiye baba yako, sijui kuwapambanua, mmestahili kufa wote.” Akamkakata, akamue, akamla.