Mbwa mwitu aliyepoteza makali ya meno yake?

Mbwa mwitu aliyepoteza makali ya meno yake?

Yussufhaji

Member
Joined
Sep 9, 2018
Posts
35
Reaction score
28
Maoni

Mtoto wa Mkulima
02/02/2021

Katika kuperuzi peruzi mtandaoni, nikakutana na habari ya kushtusha japo sio ya kushangaza, kupitia ukurasa wa facebook wa Jamiiforum juu ya nchi ya Rwanda kutaka Ufafanuzi wa kina kutoka Uengereza kwanini raia wa nchi hiyo wasiingie nchini Uengereza? Ikiwa ni hatua iliyofuata baada ya Uengereza kuiorodhesha nchi ya Rwanda kuwa miongoni mwa nchi zilizo pewa zuio la raia wake kuingia nchini Uengereza kwa kisingizio cha ugonjwa wa Covid-19.

Wengi wetu tunajiuliza ujasiri wa nchi ya Rwanda kuweza kuihoji nchi ya Uengereza, kuhusu zuio la wananchi wa Rwanda kutokuruhusiwa kuingia nchini Uengereza kwa kisingizio cha ugonjwa wa Covid-19.

Uengereza ni miongoni mwa nchi wanachama 5 wenye kura ya turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Ujasiri huu wa Rwanda unatokana na nini? Au Uengereza kwa sasa ni sawa na Mbwa mwitu aliyepoteza makali ya meno yake?

Kwanini najiuliza au najaribu kuifananisha Uengereza na Mbwa mwitu aliyepoteza makali ya meno yake?

Hii ni kwasababu ya tabia Mbwa mwitu ya kupenda kutembea kwa makundi wakati wa mawindo, mbwa mwitu ni mnyama anaesifika kwa umoja haswa katika mapambano ya uwindaji.

Imezoeleka pia kwa nchi ya Uengereza, kujifunganisha na nchi kadhaa katika kulinda maslahi yake mbalimbali, kwa mfano Uengereza kwa miaka 47 imekuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya, ikipigania kutetea na kulinda maslahi yake na ya Ulaya kwa ujumla ndani na nje ya Ulaya.

Kujitoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya kumeacha athari kubwa kisiasa haswa kwa kuzingatia utamaduni wa Umoja wa Ulaya wa kufanya maamuzi ya masula ya muhimu kwa pamoja. Uengereza inahitaji kuungwa mkono.

Sisemi kama Uengereza haina uungwaji mkono, Uengereza ndio kiongozi wa Jumuiya ya Madola yenye idadi ya nchi wanachama zaidi ya 50 ikiwemo Rwanda yenyewe, pia ni Mwanachama wa NATO kwa uchache.

Malkia wa Uengereza ndiye kiongozi mkuu katika nchi takribani 16, mfano Uengereza yenyewe Australia, Canada na New Zealand.

Kujitoa kwa Uengereza katika Umoja wa Ulaya kumezua tabia ya kutunishiana misuli baina ya Uengereza na Umoja wa Ulaya wenye nchi wanachama 27.

Tukio la hivi karibuni kabisa ni hadhi ya kidiplomasia ya balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Uengereza na nafasi ya Scotland na Ireland ya Kaskazini katika Umoja wa Ulaya.

Ndani ya Uengereza penyewe panafukuta, kutoka Ireland ya Kaskazini hadi scotland.

Bila ya shaka Uengereza inaonekana isingetamani mgogoro mpya, tena ndani ya Bara la Afrika. Ambako Uengereza ina maslahi mengi.

Kwa kulijua hilo, nafikiri huenda Rwanda ikawa imepata ujasiri wa kutoa tamko walilolitoa.

Na ndio maana nataka kuifananisha Uengereza na Mbwa mwitu aliyepoteza makali ya meno yake, kwa maana purukushani za mawindo hataziweza au kuzitamani, hata kama ana njaa, nguvu na hasira.

Hayo ni maoni binafsi ya Mtoto wa Mkulima.

Mawasiliano:
Email: hajjyussuf2@gmail.com
Simu: +255777158131

Fb: Yussuf Haji Khatib

FB_IMG_16121807487123846.jpg
 
Wazee wa Forex Signal hiyoo sio mpaka muambiwe hayaaa

Sell EUR Buy USD Press Order

EUR/USD Selliiiiiiiiiiiiiiiiii

NB Trade Psychology your key.
 
Back
Top Bottom