Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,208
- 4,406
MBWA AMEKATA KAMBA.
1)waondoke na waende.
Vibwengo hawa vimende.
Wale wachukia tende.
Wapenda nchi umande.
Mbwa amekata kamba,bada ya kunyimwa nyama.
2)waende na waondoke.
Waache kimya tucheke.
Japo natuhangaike.
Kwa malengo tupigike
Mbwa amekata kamba,bada ya kunyimwa nyama.
3)wamezweya vya kunyonga.
Leo walishwa vinyonga.
Mengine wanayalonga.
Ukweli kwao ni janga.
Mbwa amekata kamba,bada ya kunyimwa nyama.
4)vibonge wawa machizi.
Wanywa mchungu mchuzi.
Wa nyama ya sisimizi.
Waziandaa nyambizi.
Mbwa amekata kamba,bada ya kunyimwa nyama.
5)nasi tumtupe kando.
Tujipe moyo wa jando.
Waje wapate kipondo.
Tupande vyetu vipando.
Mbwa amekata kamba,bada ya kunyimwa nyama.
6)akija shika jambia.
Mbwa atakukimbia.
Asije najiwazia.
Japo ajua zushia.
Mbwa amekata kamba,bada ya kunyimwa nyama.
7)inawatoka mimate.
Yanadondoka yao kete.
Mtego uje wanate.
Japo twakula matete.
Mbwa amekata kamba,bada ya kunyimwa nyama.
Shairi=MBWA AMEKATA KAMBA.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255642010160.
iddyallyninga@gmail.com