"Mbuzi wa Vingunguti" Bungeni...

"Mbuzi wa Vingunguti" Bungeni...

ZeMarcopolo

Platinum Member
Joined
May 11, 2008
Posts
14,279
Reaction score
7,681
Eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam ni maarufu kwa uwepo wa mbuzi ambao wanatembea bila kuwa na mchungaji.

Kila mbuzi pale Vingunguti anazunguka anavyotaka, wakati anaotaka na popote anapotaka. Kwa kiasi fulani mbuzi wale wametumika kama utalii wa ndani kwa sababu aghalabu watu hutembelea Vingunguti kujionea mbuzi wa Vingunguti.

Katika Bunge la vyama vingi kuna nafasi ya Uongozi wa Upinzani Bungeni ambao jukumu lake ni kuratibu shughuli na hoja za Upinzani ndani ya Bunge na kwenye Kamati za Bunge pamoja na kuunda "baraza la mawaziri kivuli".

Kwa bahati mbaya Kiongozi wa Upinzani wa Bunge hili la kumi ameshindwa kabisa kufanya kazi ya Uongozi. Tangu amepata nafasi hiyo kitu pekee kinachoweza kumtambulisha kuwa yeye ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni ni gari la serikali landcruiser V8 analotembelea. Zaidi ya hapo hakuna jinsi anavyoongoza wabunge wa upinzani ndani ya Bunge.

Baraza la Mawaziri kivuli lililoundwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni halionekani kufanya chochote. Hata sasa hivi ukimuuliza mwanafunzi wa chuo kikuu ni nani waziri kivuli wa afya hakuna anayemjua! Baraza kivuli limeishia kwenye midomo tu. Kiongozi wa Upinzani Bungeni ameshindwa kuliongoza baraza hili lionekane kutoa huduma kwa wananchi.

Madhara yake tunayaona, hasahasa tabia ya mh. Tundu Lissu ya kuhakikisha wabunge wengine hawapati muda wa kutoa hoja zao kwa kuwaingilia mara kwa mara kwa kuomba mwongozo wa Spika au kutoa taarifa. Inasikitisha pale ambapo mbunge anasalimia tu, kabla hata hajaanza kutoa hoja yake tayari Spika anaombwa mwongozo! Kwa namna hii Bunge litakuwa ni vikao vya miongozo tu.

Hali hii ingeweza kuepukika iwapo Kiongozi wa Upinzani angekaa chini na wabunge wake na kuset standard kama Kiongozi. Awaambie kuwa taifa linaingia gharama kuendesha Bunge na ni wajibu wa kila mbunge kuhakikisha anaipa sababu jamii ya kuridhika na gharama ya uendeshwaji wa Bunge kutokana na umuhimu wa mijadala inayofanywa Bungeni. Kiongozi wa Upinzani pia anapaswa kuwapa mawaziri vivuli specific assignments na kufuatilia wanavyozitekeleza.

Hali hivi sasa Bungeni ni mbaya. Kiongozi wa upinzani ameshindwa kazi!!! Wabunge wa upinzani wanajiendea tu kama mbuzi wa Vingunguti wasiokuwa na mchungaji. Hali hii inasababisha kiti cha Spika kutumia adhabu ili kujaribu kuwakumbusha wabunge wakorofi wajibu wao, jambo ambalo lingeweza kuepukwa kwa Kiongozi wa Upinzani kuonyesha leadership.

Katika hekaheka hizi zote, anayeumia ni mwananchi ambaye hapati uwakilishi unaostahili na pesa za kodi yake zinatumika kuendesha Bunge lisilohudumia wananchi kikamilifu.

Fujo Bungeni HAZIFAI, KUB wafunde wabunge wako na simamia baraza kivuli la mawaziri...
 
Itabidi tumtafute Mshauri wa chadema Shida Binti Salumu amuweke sawa hivi Naibu Kiongozi Upinzani bungeni alishakufa au yupo kwenye mtandao kupiga vita ofisi ya KUB kama alivyokuwa akitamba kuchukua kiti hicho wewe acha porojo za kijinga unadhani sisi ni vipofu tunakufahamu ni sehemu ya mwigulu,january makamba lakini wanachi tunajua Spika ni bogus kiti kimemshinda
 
Kwaio viongozi vivuli ni sawa sawa na mbuzi wa vingunguti ?
 
Yani wewe badala ya kuandika hoja ukaona utukane wabunge wetu na kuwafananisha na mbuzi!

Busara zako ziko wapi we mzee marcopolo? Hivi mwaka 2015 ukifanikiwa kuingia bungeni mzee wangu ndio haya majina utawaita wabunge wenzio kama ulivyo onesha kwenye title?

Hebu onesha tofauti yako na hao unao waita mbuzi!

Wewe mzee hufai hata kulisogelea au kugusa ukuta wa bunge bora tubakiwe na lusinde kuliko kuongeza wewe ukaenda kutukana namna hii!
 
Unaweza ukawa una pointi kwa mbaaaali lakini kutokana na ujinga wako wa kufanya kazi lumumba mimi sikubaliani na wewe. Umezungumzia upande mmoja tu je, kiti cha spika mbona hujasema jinsi kinavyopwaya? Je, ni sahihi mbunge kumwita mbunge mwenzie mbwa? Je ni sawa mbunge kumtukana mwenzie fuc* you? Je ni sawa mbunge kutolewa nje kwa sababu ya kuomba miongozo zaidi ya mara moja? Je ni sahihi mbunge kusema kwamba mbunge mwenzie anawakilisha nguruwe?
 
Mh. Mbowe kama hataki kuuachia huo wadhifa aliopewa na wabunge wenzake wa Vyama vya upinzani basi wabunge wenzie wa vyama vya upinzani waangalie uwezekano wa kumuImpeach Mh. Mbowe.
 
Hapaswi kujibiwa huyo ni mwanachadema tena kiongozi msaidizi wa huyo anayesema kawaacha mbuzi ni hovyo kijana roho mbaya kama sura lake haya kalete ma ID yako mia ujijibu mwenyewe
 
Mh. Mbowe kama hataki kuuachia huo wadhifa aliopewa na wabunge wenzake wa Vyama vya upinzani basi wabunge wenzie wa vyama vya upinzani waangalie uwezekano wa kumuImpeach Mh. Mbowe.
Masalia at work ulileta barua,, ukaandika thread ,ukamtukana facebook bado yupo na atakuwepo kwa sababu anasimamia maslahi ya taifa huu uzi ni wa kiouuzi kupata kutokea mtu yumo ndani ya nyumba anatoboa kwa suluhu hana tofauti na joka la mdimu wenzake wanatandaa nchi nzima yeye kanda yake kaisusa anasema eti anakazi ngumu kuendesha kamati yake lakini anshinda hapa kushabikia ujinga wa Makinda na ndugai wanaotaka wizi utamalaki wa mali za umma nchini
 
Masalia at work ulileta barua,, ukaandika thread ,ukamtukana facebook bado yupo na atakuwepo kwa sababu anasimamia maslahi ya taifa huu uzi ni wa kiouuzi kupata kutokea mtu yumo ndani ya nyumba anatoboa kwa suluhu hana tofauti na joka la mdimu wenzake wanatandaa nchi nzima yeye kanda yake kaisusa anasema eti anakazi ngumu kuendesha kamati yake lakini anshinda hapa kushabikia ujinga wa Makinda na ndugai wanaotaka wizi utamalaki wa mali za umma nchini

Hueleweki mkuu, nenda kalale upumzike. Kama unahitaji hela ya supu kesho asubuhi niPM, ukiniQuote haitasaidia.
 
kwahiyo unamaana tatizo la wanafunzi wa chuo kutomjua waziri wa afya kivuli ni la kiongozi wa upinzani??????
hebu wewe niambie unamjua waziri kivuli wa kilimo wa bunge la Tisa????
 
ZE MARCOPOLO hebu jaribu kufanya utafiti yawezekana sio wao ni ule mti maarufu ambao kule Arusha wameugeuza chakula.
Mwenye akili hawezi babaika bungeni kama anavyofanya Lissu au Lema .
 
ze marcopolo hebu jaribu kufanya utafiti yawezekana sio wao ni ule mti maarufu ambao kule arusha wameugeuza chakula.
Mwenye akili hawezi babaika bungeni kama anavyofanya lissu au lema .
lema ndo mnamwogopa sana kila mkilala lazma awajie ndotoni. Tapenitapeni tu mwsho wenu 2015
 
Fujo Bungeni HAZIFAI, KUB wafunde wabunge wako na simamia baraza kivuli la mawaziri...
Bila shaka haujajua ulinganifu wa majukumu ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Vs Waziri Mkuu na Mnadhimu Mkuu wa Serikali.
 
ulivyo lalamika nikana kwamba cdm sichama cha upinzani bali wanaongoza nchi.mshauli fastjet astep down cdm waongoze basi.
 
Bila shaka haujajua ulinganifu wa majukumu ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Vs Waziri Mkuu na Mnadhimu Mkuu wa Serikali.

Ndio maana nasema KUB ameshindwa kazi. The fact kwamba mpaka wewe unadhani kuwa majukumu ya KUB yanaweza kutenganishwa na majukumu ya Chief Whip ni wazi kuwa KUB amekuwa non existent. Chief Whip yuko chini ya KUB kama jinsi Lukuvi alivyokuwa chini ya Pinda. Lukuvi akifanya mambo ndivyo sivyo, Pinda anawajibika kumuweka sawa. Hivyo hivyo Chief Whip akifanya tabia kama za Tundu Lissu KUB anayejua kazi yake alipaswa kumfunda. Mbowe ameshindwa hilo...
 
Sio bure, kiongozi wa upinzani bungeni ana walakini... na siku zote amekuwa nyuma ya katibu wake chamani, na sasa anaonyesha wazi juu ya udhaifu wake bungeni kwa kuburuzwa na baadhi wa wabunge, ambao kiuzoefu bungeni ni wachanga zaidi yake. Huu ni udhaifu mkubwa wa kiongozi huyo.
 
Back
Top Bottom