"Mbuzi wa Vingunguti" Bungeni...

"Mbuzi wa Vingunguti" Bungeni...

Ndugu zangu hapa mtaangaika na akina makopolo na wengine wenye kufananishwa nao rangi za miwani. The root of evil ni kiti cha spika baaaaas. Kiti cha spika ni turufu ya ccm!
 
Kiti cha Spoka kimevaa miwani ya mbao, Mama utafikiri kigagula hana huruma kabisa na wananchi, yaani taabu zote hizi tuzionazo ameruhusu wabunge wa CCM kuendesha Bunge Jazz yenye melody zisizo toka duh
 
Ushatengeneza Fallacy of Generalization tangia mwanzo,hivyo hata nisiposoma hitimisho lako...Mbuzi hata angalikuwa wa Masaki hawezi kwenda KILA MAHALI...Unamaanisha hadi kwenye SEBULE za watu wanaingia?!Wanaenda hadi baa, hotelini, makanisani, misikitini....Japo ni mbuzi nini uhakika wana RESTRICTION OF ACCESS kwa baadhi ya sehemu!Hivyo umekosea katika comparison na possibilities of the possibles.
 
Ungekuwa sawa zaidi ungezungumzia pia matusi ya akina serukamba na wenzenu wote wa ccm ukapendekeza na hatua za kuchukuliwa dhidi yao. Tatizo kubwa kwako, unataka kunya anye kuku, akinya bata kaharisha. Posti yako imwkaa ki-bias zaidi. Hao unaowaita mbuzi wa vingunguti leo wapo bungeni kesho watakuwa IKULU hiyo hiyo ya magogoni. Umaarufu wanu CCM unashuka kila siku, aangalia mikutano yenu mmekuwa wakurudishiwa kadi mikutanoni! Nawashauri jitazameni upya.
 
mleta uzi umeandika makala ndefu. Lakini mawaziri vivuli si watendaji, kuwajua au kutowajua si muhimu, wao wanaishauri serikali na kutoa mapendekezo. Mnadhimu mkuu ndie anayesimamia na kutetea wabunge wake, kuwa na macho uone lukuvi anavyosimama. Ifike mahali ufikirie.
 
Ushatengeneza Fallacy of Generalization tangia mwanzo,hivyo hata nisiposoma hitimisho lako...Mbuzi hata angalikuwa wa Masaki hawezi kwenda KILA MAHALI...Unamaanisha hadi kwenye SEBULE za watu wanaingia?!Wanaenda hadi baa, hotelini, makanisani, misikitini....Japo ni mbuzi nini uhakika wana RESTRICTION OF ACCESS kwa baadhi ya sehemu!Hivyo umekosea katika comparison na possibilities of the possibles.

Hakika bado hujawafahamu mbuzi wa Vingunguti. Ungeafahamu usingeandika hivi...
 
mleta uzi umeandika makala ndefu. Lakini mawaziri vivuli si watendaji, kuwajua au kutowajua si muhimu, wao wanaishauri serikali na kutoa mapendekezo. Mnadhimu mkuu ndie anayesimamia na kutetea wabunge wake, kuwa na macho uone lukuvi anavyosimama. Ifike mahali ufikirie.

Kiongozi wa Upinzania kazi yake ni kutembea na landcruiser tu?

Unamjua waziri kivuli wa ardhi ni nani?
 
Eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam ni maarufu kwa uwepo wa mbuzi ambao wanatembea bila kuwa na mchungaji.

Kila mbuzi pale Vingunguti anazunguka anavyotaka, wakati anaotaka na popote anapotaka. Kwa kiasi fulani mbuzi wale wametumika kama utalii wa ndani kwa sababu aghalabu watu hutembelea Vingunguti kujionea mbuzi wa Vingunguti.

Katika Bunge la vyama vingi kuna nafasi ya Uongozi wa Upinzani Bungeni ambao jukumu lake ni kuratibu shughuli na hoja za Upinzani ndani ya Bunge na kwenye Kamati za Bunge pamoja na kuunda "baraza la mawaziri kivuli".

Kwa bahati mbaya Kiongozi wa Upinzani wa Bunge hili la kumi ameshindwa kabisa kufanya kazi ya Uongozi. Tangu amepata nafasi hiyo kitu pekee kinachoweza kumtambulisha kuwa yeye ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni ni gari la serikali landcruiser V8 analotembelea. Zaidi ya hapo hakuna jinsi anavyoongoza wabunge wa upinzani ndani ya Bunge.

Baraza la Mawaziri kivuli lililoundwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni halionekani kufanya chochote. Hata sasa hivi ukimuuliza mwanafunzi wa chuo kikuu ni nani waziri kivuli wa afya hakuna anayemjua! Baraza kivuli limeishia kwenye midomo tu. Kiongozi wa Upinzani Bungeni ameshindwa kuliongoza baraza hili lionekane kutoa huduma kwa wananchi.

Madhara yake tunayaona, hasahasa tabia ya mh. Tundu Lissu ya kuhakikisha wabunge wengine hawapati muda wa kutoa hoja zao kwa kuwaingilia mara kwa mara kwa kuomba mwongozo wa Spika au kutoa taarifa. Inasikitisha pale ambapo mbunge anasalimia tu, kabla hata hajaanza kutoa hoja yake tayari Spika anaombwa mwongozo! Kwa namna hii Bunge litakuwa ni vikao vya miongozo tu.

Hali hii ingeweza kuepukika iwapo Kiongozi wa Upinzani angekaa chini na wabunge wake na kuset standard kama Kiongozi. Awaambie kuwa taifa linaingia gharama kuendesha Bunge na ni wajibu wa kila mbunge kuhakikisha anaipa sababu jamii ya kuridhika na gharama ya uendeshwaji wa Bunge kutokana na umuhimu wa mijadala inayofanywa Bungeni. Kiongozi wa Upinzani pia anapaswa kuwapa mawaziri vivuli specific assignments na kufuatilia wanavyozitekeleza.

Hali hivi sasa Bungeni ni mbaya. Kiongozi wa upinzani ameshindwa kazi!!! Wabunge wa upinzani wanajiendea tu kama mbuzi wa Vingunguti wasiokuwa na mchungaji. Hali hii inasababisha kiti cha Spika kutumia adhabu ili kujaribu kuwakumbusha wabunge wakorofi wajibu wao, jambo ambalo lingeweza kuepukwa kwa Kiongozi wa Upinzani kuonyesha leadership.

Katika hekaheka hizi zote, anayeumia ni mwananchi ambaye hapati uwakilishi unaostahili na pesa za kodi yake zinatumika kuendesha Bunge lisilohudumia wananchi kikamilifu.

Fujo Bungeni HAZIFAI, KUB wafunde wabunge wako na simamia baraza kivuli la mawaziri...

Huduma mnatoa nyie mnaokusanya kodi zetu, Lissu anafanya kazi yake kama anavyofanya lukuvi hivi haukuona lema alivyokuwa anakatishwa na lukuvi.........unasema hawafanyi kazi wakati wanawapa jambajamba hadi mnaita polisi
 
Dah ! ZeMarcopollo umeshuka kiwango kiasi hiki , mbona umeporomoka kwa kasi sana , Nini kimetokea ? Pesa ya Research haijatoka , au wamekuchinjia Baharini ?
 
Kama huna la kuwaambia wana jf c bora unyamaze kuliko kuanzisha uzi usio na mbele wa nyuma.
Chizi sio lazima aokote makopo.
 
ZE MARCOPOLO hebu jaribu kufanya utafiti yawezekana sio wao ni ule mti maarufu ambao kule Arusha wameugeuza chakula.
Mwenye akili hawezi babaika bungeni kama anavyofanya Lissu au Lema .

Kama unatilia shaka uwezo wa Lissu na mchango wake katika kutetea watanzania basi eidha wewe sio mfuatiliaji wa mambo, au umenunuliwa ukaacha kutumia akili au hauna akili kabisa.
Wabunge wote wa chama cha magamba wanamugopa huyo mtu kwa hoja makini na kama ungepata nafasi ya kuongea na jaji Werema kama sisi ambao tunaongea naye katika maongezi yasio rasmi ungejua jinsi ambavyo yeye werema na serikali wanavyomuogopa Tundu Lissu.
 
wewe mleta uzi umelaniwa kuanzia kwako hadi kwa vizazi vyako vyote vilivyopo na vijavyo kwa kuwa msaliti wa kila anayetetea mauwaji na uchafu wote uliomo ccm
 
Hivi Ndugu,

Ni kipi ni ahueni kati ya Mbuzi na Mbwa? Yule Mtangazaji Mbunge anasema hawa watu ni Mbwa na ZeMalcopolo anasema siyo Mbwa bali ni Mbuzi wa Vingunguti. Sasa tujue lipi? Au tuwape majina kulingana na vyama vyao so kuwepo na Mbwa, Mbuzi n.k? Matusi gana haya jamani kwa viongozi wetu? Tunajenga taifa la aina gani lisiloheshimu viongozi wake? Pengine no bora kuelewa kuwa hawa watu pa1 na kuwa ni viongozi, lakini pia ni wazazi; ni waume au wake za watu; ni wajomba na mashangazi za watu ambao kwa vyovyote vile wasingependa kusikia ndugu zao wanahusishwa na majina ya wanyama waliolaaniwa katika jamii kama mbuzi, mbwa na bila shaka mwingine ataleta mengine muda mfupi ujao. Chakujiuliza ni kuwa, mbona haya majina hayakuwepo wakati wa utawala wa bunge lililopita chini ya Samuel Sitta?

Yani wewe badala ya kuandika hoja ukaona utukane wabunge wetu na kuwafananisha na mbuzi!

Busara zako ziko wapi we mzee marcopolo? Hivi mwaka 2015 ukifanikiwa kuingia bungeni mzee wangu ndio haya majina utawaita wabunge wenzio kama ulivyo onesha kwenye title?

Hebu onesha tofauti yako na hao unao waita mbuzi!

Wewe mzee hufai hata kulisogelea au kugusa ukuta wa bunge bora tubakiwe na lusinde kuliko kuongeza wewe ukaenda kutukana namna hii!
 
Hivi Ndugu,

Ni kipi ni ahueni kati ya Mbuzi na Mbwa? Yule Mtangazaji Mbunge anasema hawa watu ni Mbwa na ZeMalcopolo anasema siyo Mbwa bali ni Mbuzi wa Vingunguti. Sasa tujue lipi? Au tuwape majina kulingana na vyama vyao so kuwepo na Mbwa, Mbuzi n.k? Matusi gana haya jamani kwa viongozi wetu? Tunajenga taifa la aina gani lisiloheshimu viongozi wake? Pengine no bora kuelewa kuwa hawa watu pa1 na kuwa ni viongozi, lakini pia ni wazazi; ni waume au wake za watu; ni wajomba na mashangazi za watu ambao kwa vyovyote vile wasingependa kusikia ndugu zao wanahusishwa na majina ya wanyama waliolaaniwa katika jamii kama mbuzi, mbwa na bila shaka mwingine ataleta mengine muda mfupi ujao. Chakujiuliza ni kuwa, mbona haya majina hayakuwepo wakati wa utawala wa bunge lililopita chini ya Samuel Sitta?

Kwani kuna mtu wa nje amewatukana?!,si nao wenyewe na uheshimiwa wao wameamua kuchagua kutukanana?!,mi sioni tatizo wacha watukanane na ikibidi wachapane makonde kwa sababu hapo pote kinachotafutwa ni hicho tu kwa sababu watu wanataka kutafuta umaarufu wa wakina Chieu,isipokuwa itakuwa kasheshe tu siku ambayo watamtukana mtu wa nje ya Bunge ambaye sio mbunge,hapo ndo nitawaona hawafai,lakini wao kwa wao,tumeshawazoea.
 
Ni sawa Mku ila kwa vile mambo haya hayakuwepo chini ya uongozi uliotangulia, ni dhahiri kuwa kuna udhaifu mkubwa sana kwenye kiti ambao ndio chanzo cha yote haya. Kiukweli inasikitisha kwa watoto wao kusikia baba zao ni mbuzi wa vingunguti au ni mbwa au wanatukana hovyo kama vile f--- you! Haya mambo mku siyo bahati mbaya. Ni matokeo ya maisha yeo ya kila siku.

Kwani kuna mtu wa nje amewatukana?!,si nao wenyewe na uheshimiwa wao wameamua kuchagua kutukanana?!,mi sioni tatizo wacha watukanane na ikibidi wachapane makonde kwa sababu hapo pote kinachotafutwa ni hicho tu kwa sababu watu wanataka kutafuta umaarufu wa wakina Chieu,isipokuwa itakuwa kasheshe tu siku ambayo watamtukana mtu wa nje ya Bunge ambaye sio mbunge,hapo ndo nitawaona hawafai,lakini wao kwa wao,tumeshawazoea.
 
Mtoa mada ulisema Mbowe Ana v8 si ameikataa ya kifahari Ina maana ameichukua kinyemela
 
Mh. Mbowe kama hataki kuuachia huo wadhifa aliopewa na wabunge wenzake wa Vyama vya upinzani basi wabunge wenzie wa vyama vya upinzani waangalie uwezekano wa kumuImpeach Mh. Mbowe.

Mdau punguza jaziba na husuda .Mbowe kakukosea nn?hakuna upinza wa dhati kama wa chadema.Kuna CUF wao wamekuwa upande wa CCM japo wapinzani.wanakuja kusemea kwenye majukwaa wakiwa nje ya ukumbi wa bunge.kama mbowe hafanyi kazi kiti cha spika kisingeonekan kinapwaya.Kuonekana wai kuwa hayupo kulinda katiba, kanuni, wala hana hekima , chanzo ni uthabiti wa wabunge wa chadema kutoa hoja mtambuka ambazo counter ya wabunge wa ccm nikupiga propoganda na kutukana utafikiri NAPE MNAUYE.Punguza jazba na punguza wivu wakuna mapambano yenye hoja zenye mshiko hata kama umetumwa na ccm lumumba.
 
Mtoa mada ulisema Mbowe Ana v8 si ameikataa ya kifahari Ina maana ameichukua kinyemela

Aliikataa mbele ya kamera za waandishi wa habari lakini baadae akaenda kwa katibu wa Bunge kumwambie "aisee yale mambo ya siasa yaache kama yalivyo aisee, nipatie V8 na dereva aisee, maisha yenyewe ndio hayahaya aisee..."
 
Back
Top Bottom