"Mbuzi wa Vingunguti" Bungeni...

"Mbuzi wa Vingunguti" Bungeni...

Mbowe leo amedhihirisha kwa mara nyingine kuwa wabunge wa Chadema ni kama mbuzi wa Vingunguti...
 
Yaani bora wewe umewaita mbuzi wa vingunguti,maana jina ambalo ningewaita mimi we acha tu.Ashakum si matusi,hawa wapumbavu ndani ya siku mbili tena zisizokamilika vizuri wametoka nje mara mbili.Mpaka sasa bado najiuliza kwa nini wanatabia za kuzira zira?Maana tabia hizi ni za jinsia ya KE na wala sio Me?Je hawa CDM wanazira ili wabembelezwe au watongozwe?Kura za huruma zitabaki Arusha tu,nyambaf!
 
Kuwa na watu wenye mtazama kama mleta mada ni janga kwa taifa.Hii inaonyesha jinsi mtu anaweza kutumika bila yeye kujiuliza.Haki haiombwi,inadaiwa kwa nguvu zote.Usipotenda haki basi ujue iko siku wataidai.Tumefika hapa kutokana na kuwa na viongozi wasiokuwa na dira na wanaojali maslahi ya wananchi.Haki ni tunda la amani.Pia maandiko matakatifu yanasema,haki huinua taifa.
 
Eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam ni maarufu kwa uwepo wa mbuzi ambao wanatembea bila kuwa na mchungaji.

Kila mbuzi pale Vingunguti anazunguka anavyotaka, wakati anaotaka na popote anapotaka. Kwa kiasi fulani mbuzi wale wametumika kama utalii wa ndani kwa sababu aghalabu watu hutembelea Vingunguti kujionea mbuzi wa Vingunguti.

Katika Bunge la vyama vingi kuna nafasi ya Uongozi wa Upinzani Bungeni ambao jukumu lake ni kuratibu shughuli na hoja za Upinzani ndani ya Bunge na kwenye Kamati za Bunge pamoja na kuunda "baraza la mawaziri kivuli".

Kwa bahati mbaya Kiongozi wa Upinzani wa Bunge hili la kumi ameshindwa kabisa kufanya kazi ya Uongozi. Tangu amepata nafasi hiyo kitu pekee kinachoweza kumtambulisha kuwa yeye ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni ni gari la serikali landcruiser V8 analotembelea. Zaidi ya hapo hakuna jinsi anavyoongoza wabunge wa upinzani ndani ya Bunge.

Baraza la Mawaziri kivuli lililoundwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni halionekani kufanya chochote. Hata sasa hivi ukimuuliza mwanafunzi wa chuo kikuu ni nani waziri kivuli wa afya hakuna anayemjua! Baraza kivuli limeishia kwenye midomo tu. Kiongozi wa Upinzani Bungeni ameshindwa kuliongoza baraza hili lionekane kutoa huduma kwa wananchi.

Madhara yake tunayaona, hasahasa tabia ya mh. Tundu Lissu ya kuhakikisha wabunge wengine hawapati muda wa kutoa hoja zao kwa kuwaingilia mara kwa mara kwa kuomba mwongozo wa Spika au kutoa taarifa. Inasikitisha pale ambapo mbunge anasalimia tu, kabla hata hajaanza kutoa hoja yake tayari Spika anaombwa mwongozo! Kwa namna hii Bunge litakuwa ni vikao vya miongozo tu.

Hali hii ingeweza kuepukika iwapo Kiongozi wa Upinzani angekaa chini na wabunge wake na kuset standard kama Kiongozi. Awaambie kuwa taifa linaingia gharama kuendesha Bunge na ni wajibu wa kila mbunge kuhakikisha anaipa sababu jamii ya kuridhika na gharama ya uendeshwaji wa Bunge kutokana na umuhimu wa mijadala inayofanywa Bungeni. Kiongozi wa Upinzani pia anapaswa kuwapa mawaziri vivuli specific assignments na kufuatilia wanavyozitekeleza.

Hali hivi sasa Bungeni ni mbaya. Kiongozi wa upinzani ameshindwa kazi!!! Wabunge wa upinzani wanajiendea tu kama mbuzi wa Vingunguti wasiokuwa na mchungaji. Hali hii inasababisha kiti cha Spika kutumia adhabu ili kujaribu kuwakumbusha wabunge wakorofi wajibu wao, jambo ambalo lingeweza kuepukwa kwa Kiongozi wa Upinzani kuonyesha leadership.

Katika hekaheka hizi zote, anayeumia ni mwananchi ambaye hapati uwakilishi unaostahili na pesa za kodi yake zinatumika kuendesha Bunge lisilohudumia wananchi kikamilifu.

Fujo Bungeni HAZIFAI, KUB wafunde wabunge wako na simamia baraza kivuli la mawaziri...

Pumba = Pointless
 
Hili TUTUSA limetoka wapi jamani? mie silielewi kabisa! TASA wa akili kweli wewe.
 
Kwa fujo zimetokea? Nani ailikuwa sahihi?kipi kilikuwa kinalindwa?
 
Mkuu, uko sahihi kabisa, alichokifanya Mbowe ni pumba kuu kuliko zote duniani...

Pumba ni hizi unazozileta hapa Jukwaani.
Jukwaa pekee ambalo hua unalitendeaga haki ni Jukwaa la Biashara hasa kwenye sekta ya Ujenzi wa Ghorofa tu.
 
Pumba ni hizi unazozileta hapa Jukwaani.
Jukwaa pekee ambalo hua unalitendeaga haki ni Jukwaa la Biashara hasa kwenye sekta ya Ujenzi wa Ghorofa tu.

Sugu alikuwa anataka kumlipizia teke askari! alivyoona imeshindikana kaamua avunje microphone ya Bunge!!!

Je nani atalipia microphone.
 
Sugu alikuwa anataka kumlipizia teke askari! alivyoona imeshindikana kaamua avunje microphone ya Bunge!!!

Je nani atalipia microphone.

Kaka,

Unajua exactly what happened. Hivi nikuulize, Mtolewa nje alikua nani pale? Sugu? Kosa la Sugu la kufanya mpaka askari wote wamshambulie yeye ni nini??

Picha zinaonyesha kua Sugu alijishika kwenye Microphone ili asivutwe asiondolewe pale na askari, bali atoke mwenyewe kistaarabu. But ni wazi tu kua angeweza kutembea mwenyewe akatoka bila bughudha.
 
Kaka, ni wazi tu kua angeweza kutembea mwenyewe akatoka bila bughudha.

Ni kweli kabisa Sugu angeweza kutoka kistaarabu ila ameamua kwa makusudi kuvunja microphone ya Bunge. Ndio maana wadau wanapendekeza Sugu akatwe mshahara wake ili kufidia hasara aliyosababisha.
 
Back
Top Bottom