Mambo vp wadau, mimi kazi zangu zipo mkoani, ila familia yangu inaishi Dar, wiki iliyopita nimerudi kusalimia familia nimekuta kuna mbuyu umeota pembeni ya Nyumba yangu ambapo kuna kiwanja nimepanga kujenga lakini kila nikipanga kuanza ujenzi mambo yanavurugika pesa inasambaratika na umeota kwenye dirisha la watoto, mke wangu alikua aujui ndo akauacha nami nilikua siujui piano nilifikiri mti wa kawaida ndo maana sikuwekea maanani, leo vibarua wangu walikuja nyumbani ndio wakaniambia ni mbuyu, no umekua una urefu wa futi 18, je nikiukata utaniletea madhara? naomba ushauri wadau.