Mbuyu umeota nyumbani kwangu

Mbuyu umeota nyumbani kwangu

Kama ni mambo ya kiimani sitachangia, lakini kama ulitaka kufahamu madhara ama faida ya kuwepo kwenye compound yako, ningekudadavulia vzuuuri!

Itoshe tu kusema huo mti kama upo kwako na unaishi maeneo ya Dar uukate hima haufai kuwepo 'site'.

Maana mibuyu ya Dar, aidha kutokana na hali ya hewa ama udongo hukua kupitiliza, waweza kutoboa katikati ukapitisha barabara ya gari.

Na kutokana na ufinyu wa viwanja vyenu, waweza ukajaa mti mmoja ukavunja hata nyumba iliyojengwa.

Ingawa miti hiyo hukua kidogokidogo lakini ina maisha marefu sana kuzidi aina nyingine ya miti hapa Afrika.
Unakadiriwa life span yake ikazidi miaka 1000!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani toka nchi 1 mpaka futi 18 msijue kama ni mbuyu, uliota siku moja tu au ilikuwaje, maana ni miaka hapo.
Mambo vp wadau, mimi kazi zangu zipo mkoani, ila familia yangu inaishi Dar, wiki iliyopita nimerudi kusalimia familia nimekuta kuna mbuyu umeota pembeni ya Nyumba yangu ambapo kuna kiwanja nimepanga kujenga lakini kila nikipanga kuanza ujenzi mambo yanavurugika pesa inasambaratika na umeota kwenye dirisha la watoto, mke wangu alikua aujui ndo akauacha nami nilikua siujui piano nilifikiri mti wa kawaida ndo maana sikuwekea maanani, leo vibarua wangu walikuja nyumbani ndio wakaniambia ni mbuyu, no umekua una urefu wa futi 18, je nikiukata utaniletea madhara? naomba ushauri wadau.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mtu alikula ubuyu akatupa mbegu ikaota, simple! acha kujipa stress
 
Kuna watu mnaishi maisha ya tabu sana. Yaani mbuyu tu uote kwenye eneo langu nishindwe kuukata? Inaonekana mtoa mada unaishi kwa imani kali za mambo ya giza, na unazisadiki sana hata pasipokuwepo.

Nini mbuyu, mimi niliwahi kuona chungu na sahani vimetupwa njia panda karibu na nyumba yangu ilikua usiku natoka harusini. Nikavibeba nikatia kwenye fence. Asubuhi nikaviosha vikaanza matumizi. Uchawi hauendi kwa mentali.

Sent using my Nokia Torch
hiyo chai mzee!
 
Mambo vp wadau, mimi kazi zangu zipo mkoani, ila familia yangu inaishi Dar, wiki iliyopita nimerudi kusalimia familia nimekuta kuna mbuyu umeota pembeni ya Nyumba yangu ambapo kuna kiwanja nimepanga kujenga lakini kila nikipanga kuanza ujenzi mambo yanavurugika pesa inasambaratika na umeota kwenye dirisha la watoto, mke wangu alikua aujui ndo akauacha nami nilikua siujui piano nilifikiri mti wa kawaida ndo maana sikuwekea maanani, leo vibarua wangu walikuja nyumbani ndio wakaniambia ni mbuyu, no umekua una urefu wa futi 18, je nikiukata utaniletea madhara? naomba ushauri wadau.

Duh! pole sana story yako sijaielewa, mbuyu umeota umefikia futi 18 na kwa ukuaji wa mbuyu ni miaka kadhaa mpaka kufikia urefu huo, la pili kwann unaruhusu ubongo wako kutafsiri mambo yasiyokuwepo na ambayo unayajua kuwa hayapo? mbuyu lazima uote hasa ukizingatia watu wanavyopenda kula ubuyu na katika miche rahisi sana kuota ni mibuyu, me nina binti yangu hapa anapenda ubuyu akila zile mbegu anazitupa tupa tu karibu na bustani so mara nyingi kuna vimche vingi vidogo vinaota vya mbuyu, tatizo umejaza FEAR yaani kipindi unakua toka utotoni kuingia utu uzima ulibeba na story zoooote za utotoni kifupi ulikubali kukua baadhi ya sehemu na sehemu zingine uliziacha hayo ndo madhara yake sasa umetengenezewa FEAR (False Evidence Appear Real) na zile story za utotoni, unataka kusema ugumu wa mambo unaletwa na mbuyu? mara ngapi mambo yako yamevurugika na hakukuwa na mbuyu? kikubwa tafuta shoka ukate na miti yake itakufaa kwa kuni au matumizi mengine ila kikubwa nakushauri KUA kwa upande huo pia!
 
Msanii mkubwa wewe! Mbuyu hadi futi 18 uliota kwa siku 3? acha kutuona sie maamuma!
Na kama ni kweli ni ishara mbaya sana hameni la sivyo mtakufa wote!
 
Hamisha nyumba iweke pembeni Acha mbuyu wa watu uote mwaya...😀😀
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom